Mkuu wa Wilaya ya Temeke Bi Sofia na ulevi wa madaraka

Saint Ivuga

JF-Expert Member
Joined
Aug 21, 2008
Posts
55,024
Reaction score
59,684
Gazeti la majira limeleta taarifa huyu mama akisema na kuamuru eti watu wapigwe bakora kisa wamevaa nusu uchi.
Kweli hapa ndio kafikiria sana na akili yake imemtuma huko?
Ningetegemea angesema mtu akitupa takataka ovyo apigwe bakora ila yeye hajaona hili.
Barabara za tandika nilitegemea angezipigania ziwekwe lami, achana na lami huku ni mbali sana na urefu wa kamba yake.
Basi ningetegemea huyu mama akiamuru na kusafisha barabara za temeke na hata kufanya mpango wa kuongea na meya wa eneo lake na kushauriana na kuweza kununua magari ya kusafisha barabara na kumwagia maji barabarani kuondoa vumbi ambalo ni kero kubwa kuliko hata hivyo vimini ambavyo kaviona yeye akiwa madarakani.
Tuseme kuwa yeye toka azaliwe hajawahi kuvaa kimini? Mbona anapaka wanja? Na akitokea mtu ama kiongozi kidume ambaye anakerwa na wanawake wanaopaka wanja akadai nao wapigwe bakora huyu mama atajiskiaje?
Maadili ya Tanzania anayoyapigania ili yasivunjwe ni vimini?
Wakishaanza kuvaa maoverall na magauni makubwa makubwa kwenye jiji hili lenye joto zaidi ya 27 centigrade unategemea kuwa tutakuwa tunawatendea haki?
Huyu mama ninachoona ni ulevi wa madaraka na kutaka kuandikwa kwenye vyombo vya habari.
Angeifanya temeke iwe safi hapo ndio tungemsifia ila sio kwa kupiga watu bakora.
Kwanza jiji la dsm lina wadada wanaovaa vizuri na kujiheshimu. Kuliko hata baadhi miji mingi duniani nliyoitembelea.
 
naunga mkono hoja nikweli kabisa sijaona kosa lake huyu mama nashangaa kuona eti watu wanamdhihaki namashaka na upeo wenu wa kufikiri mnaodhani huyu mama kapotoka katika hili.
 
Namuunga mkono huyu mama kwa asilimia mia.
Wengi tunaoonekana kumpinga tunataka kujisingizia katika imani fulani lakini sii kweli kuwa kuns imani ya kuruhusu watu watembee nusu uchi labda dini ya shetani maana kusudi lake ni kuhakikisha inakiburuza kizazi chote kuzimu.
WHY NOT Y'OUR GARMENTS BE MODEST AND DECENT?
.
 
Kwa hiyo kuvaa vimini ni marufuku kwa wakazi wa Temeke? (Wilaya ya huyo Mama). Vipi mtu akitokea Ilala akaenda Temeke kutembea naye itabidi alambwe Bakora? Sijasoma hiyo taarifa lakini hwezi kupiga marufuku uvaaji wa vimini kwa ujumla wake bali angekataza labda watu wanaokwenda kwenye maofisi ya serikali na wafanyakazi kwenye hizo ofisi za serikali wasivae vimini ingekuwa sawa. Sasa mtu wa mtaani akivaa kimini wewe anakuhusu nini?

Tiba
 
Hao wanaovaa nusu uchi na yeye anayeshirikiana na Halmashauri kula kodi zetu ni nani anayestaili kuchapwa viboko?
 
Gazeti la majira limeleta taarifa huyu mama akisema na kuamuru eti watu wapigwe bakora kisa wamevaa nusu uchi.
Kweli hapa ndio kafikiria sana na akili yake imemtuma huko?
Ningetegemea angesema mtu akitupa takataka ovyo apigwe bakora ila yeye hajaona hili.
Barabara za tandika nilitegemea angezipigania ziwekwe lami, achana na lami huku ni mbali sana na urefu wa kamba yake.
Basi ningetegemea huyu mama akiamuru na kusafisha barabara za temeke na hata kufanya mpango wa kuongea na meya wa eneo lake na kushauriana na kuweza kununua magari ya kusafisha barabara na kumwagia maji barabarani kuondoa vumbi ambalo ni kero kubwa kuliko hata hivyo vimini ambavyo kaviona yeye akiwa madarakani.
Tuseme kuwa yeye toka azaliwe hajawahi kuvaa kimini? Mbona anapaka wanja? Na akitokea mtu ama kiongozi kidume ambaye anakerwa na wanawake wanaopaka wanja akadai nao wapigwe bakora huyu mama atajiskiaje?
Maadili ya Tanzania anayoyapigania ili yasivunjwe ni vimini?
Wakishaanza kuvaa maoverall na magauni makubwa makubwa kwenye jiji hili lenye joto zaidi ya 27 centigrade unategemea kuwa tutakuwa tunawatendea haki?
Huyu mama ninachoona ni ulevi wa madaraka na kutaka kuandikwa kwenye vyombo vya habari.
Angeifanya temeke iwe safi hapo ndio tungemsifia ila sio kwa kupiga watu bakora.
Kwanza jiji la dsm lina wadada wanaovaa vizuri na kujiheshimu. Kuliko hata baadhi miji mingi duniani nliyoitembelea.

Ww ndo mlevi. umeandika uharo wako hapa kutetea ujinga. Huyo mama right kabisa. au ww ndo mkuu wa wavaa vimini na kata kei. we umeona kuvaa overlory ndo nguo pekee ya kustri mwili. Hapa umetumia masaburi zaidi kuliko akili.
 
inawezekana yuko sahihi ila huwezi kumpa mtu adhabu kwakuwa yeye sio mahakama hata jambazi akikamatwa anaiba kabisa utasikia wanasema anayeshukiwa kuwa jambazi na mahakama mpaka ihakikishe kuwa ni jambazi not otherwise.
 
Easy easy. Ndugu yangu kaa chini ufikirie vizuri. Suala la mavazi ni la mzazi na mwanae huko nyumbani unless kama tunatumia sharia.
Vipi vumbi ambalo limejaa kwenye barabara za Temeke na vibaka wa Tandika huyu mama ana mkakati gani?
 
gazeti la majira limeleta taarifa huyu mama akisema na kuamuru eti watu wapigwe bakora kisa wamevaa nusu uchi.
Kweli hapa ndio kafikiria sana na akili yake imemtuma huko?
Ningetegemea angesema mtu akitupa takataka ovyo apigwe bakora ila yeye hajaona hili.
Barabara za tandika nilitegemea angezipigania ziwekwe lami, achana na lami huku ni mbali sana na urefu wa kamba yake.
Basi ningetegemea huyu mama akiamuru na kusafisha barabara za temeke na hata kufanya mpango wa kuongea na meya wa eneo lake na kushauriana na kuweza kununua magari ya kusafisha barabara na kumwagia maji barabarani kuondoa vumbi ambalo ni kero kubwa kuliko hata hivyo vimini ambavyo kaviona yeye akiwa madarakani.
Tuseme kuwa yeye toka azaliwe hajawahi kuvaa kimini? Mbona anapaka wanja? Na akitokea mtu ama kiongozi kidume ambaye anakerwa na wanawake wanaopaka wanja akadai nao wapigwe bakora huyu mama atajiskiaje?
Maadili ya tanzania anayoyapigania ili yasivunjwe ni vimini?
Wakishaanza kuvaa maoverall na magauni makubwa makubwa kwenye jiji hili lenye joto zaidi ya 27 centigrade unategemea kuwa tutakuwa tunawatendea haki?
Huyu mama ninachoona ni ulevi wa madaraka na kutaka kuandikwa kwenye vyombo vya habari.
Angeifanya temeke iwe safi hapo ndio tungemsifia ila sio kwa kupiga watu bakora.
Kwanza jiji la dsm lina wadada wanaovaa vizuri na kujiheshimu. Kuliko hata baadhi miji mingi duniani nliyoitembelea.

wewe unamshangaa huyo si afadhali kidogo. Mkurugenzi wa wilaya ya serengeti aliamrisha watu wote wenye fenci za michongoma wazikata usawa wa mita moja na nusu kwenda juu.
 
inawezekana yuko sahihi ila huwezi kumpa mtu adhabu kwakuwa yeye sio mahakama hata jambazi akikamatwa anaiba kabisa utasikia wanasema anayeshukiwa kuwa jambazi na mahakama mpaka ihakikishe kuwa ni jambazi not otherwise.

Mama ana apply kitu kinachoitwa SHaria.. Somalia ndio kinatumiwa na al shabib
 
Gazeti la majira limeleta taarifa huyu mama akisema na kuamuru eti watu wapigwe bakora kisa wamevaa nusu uchi.
Kweli hapa ndio kafikiria sana na akili yake imemtuma huko?
Ningetegemea angesema mtu akitupa takataka ovyo apigwe bakora ila yeye hajaona hili.
Barabara za tandika nilitegemea angezipigania ziwekwe lami, achana na lami huku ni mbali sana na urefu wa kamba yake.
Basi ningetegemea huyu mama akiamuru na kusafisha barabara za temeke na hata kufanya mpango wa kuongea na meya wa eneo lake na kushauriana na kuweza kununua magari ya kusafisha barabara na kumwagia maji barabarani kuondoa vumbi ambalo ni kero kubwa kuliko hata hivyo vimini ambavyo kaviona yeye akiwa madarakani.
Tuseme kuwa yeye toka azaliwe hajawahi kuvaa kimini? Mbona anapaka wanja? Na akitokea mtu ama kiongozi kidume ambaye anakerwa na wanawake wanaopaka wanja akadai nao wapigwe bakora huyu mama atajiskiaje?
Maadili ya Tanzania anayoyapigania ili yasivunjwe ni vimini?
Wakishaanza kuvaa maoverall na magauni makubwa makubwa kwenye jiji hili lenye joto zaidi ya 27 centigrade unategemea kuwa tutakuwa tunawatendea haki?
Huyu mama ninachoona ni ulevi wa madaraka na kutaka kuandikwa kwenye vyombo vya habari.
Angeifanya temeke iwe safi hapo ndio tungemsifia ila sio kwa kupiga watu bakora.
Kwanza jiji la dsm lina wadada wanaovaa vizuri na kujiheshimu. Kuliko hata baadhi miji mingi duniani nliyoitembelea.

Mimi siuungi mkono hoja yako, ila kwa wale wenye mtazamo Kama wangu ebu tutafakari kauli ya DC kwa kina na madhara yake.
Hivi nchi hii si inaongozwa kwa utawala wa sheria, ni sheria gani inaruhusu mvaa kimini achapwe viboko? Na atakayemcha ni nani, Hakimu, Polisi au mwananchi atakayekutana naye barabarani? Hivi sio wao ma-DC/RC wanaohubiri kwa wananchi kuacha kujichukuliwa sheria mkononi? Tumeshuhudia pia kuwa suala la mavazi limekuwa likigusa imani za watu, hivi hao watu wakiamua kutekeleza maagizo ya DC na kuumiza watu mtaani patakalika? Au ndio uhamasishaji wa vurugu mitaani? Nina wasiwasi sana na utendaji wa huyu DC hasa ktk suala la sheria. Mi nashauri ni vyema kutafakari kabla ya kutoa maagizo hasa kwa mtu mwenye madaraka Kama DC
 
Viongozi wasimamie masuala muhimu. Ujinga (kupata elimu bora); afya (usafi kuondokana na uchafu); uchumi (kuondokana na umaskini); miundo mbimu nk.
 
Kwa hiyo kuvaa vimini ni marufuku kwa wakazi wa Temeke? (Wilaya ya huyo Mama). Vipi mtu akitokea Ilala akaenda Temeke kutembea naye itabidi alambwe Bakora? Sijasoma hiyo taarifa lakini hwezi kupiga marufuku uvaaji wa vimini kwa ujumla wake bali angekataza labda watu wanaokwenda kwenye maofisi ya serikali na wafanyakazi kwenye hizo ofisi za serikali wasivae vimini ingekuwa sawa. Sasa mtu wa mtaani akivaa kimini wewe anakuhusu nini?

Tiba
Nakuunga mkono kama anazungumzia ofisi za serikali sawa,kinyume cha hapo ni kukaribisha wahuni mtaani kuanza kuwasumbua dada na mama zetu! Kosa ni mtu kutembea uchi,lakini kama amevaa mini yake tatizo nini?! Inawezekana kweli huyu dada toka 4 flats pale Upanga madaraka aliyopewa yamemlevya sasa!
 
wilaya ya temeke ina matatizo chungu nzima....badala ya kuyashughulikia anahangaika na vimini
 
naunga mkono hoja nikweli
kabisa sijaona kosa lake huyu mama nashangaa kuona eti watu wanamdhihaki
namashaka na upeo wenu wa kufikiri mnaodhani huyu mama kapotoka katika
hili.

Unamuunga mkono kwa sheria gani anayotumia inayozuia vimini? aache kujishaua! apambane kubadili mfumo wa sheria sio kupiga watu viboko! ajaribu kwa mke wangu,maana mi namruhusu kuvaa sasa ampige aone!
 
wilaya ya temeke ina matatizo chungu nzima....badala ya kuyashughulikia anahangaika na vimini

Kuvaa kumini kunahusikana na maadili. Huwezi ishi na maadili huku una njaa. Njaa inafanya mtu kumchinja mwanae na kumla nyama. Umaskini unasababisha kuporomoka maadili. Namshauri huyu mama aanze na suala la kushughulikia kuuondoa umaskini ndipo maadili yatajirekebisha yenyewe sio kwa njia ya viboko. Hawa viongozi wetu vipi?
 
Back
Top Bottom