Mkuu wa Wilaya Ukerewe huwatendei haki Wananchi na humwakilishi Rais vizuri

Oct 22, 2020
78
150
Wakuu wa Wilaya hujinasibu kumwakilisha rais lakini baadhi ya watu hawa ni balaa. Nimesimuliwa anayoyafanya mkuu wa wilaya ya Ukerewe, yanasikitisha. Tangu Mkuu huyu wa Wilaya amepelekwa wilayani, Migogoro haiishi. Mgogogro na kanisa katoliki juu ya ardhi, migogoro na wavuvi na matumizi ya nguvu kukusanya pesa na polisi wakati maafisa watendaji wa wilaya wapo. Kukusanya pesa za ujenzi wa madarasa na kuwaahidi Wananchi kuwaletea mabati baadaye kutokomea bila majibu, n.k.

Jipya sasa ni matumizi ya jeshi la polisi ktk kukusanya michango ya ujenzi wa madarasa unaoendelea. Mkuu huyu wa Wilaya Bw. Cornel Magembe amekuwa tena ni mtu wa vitisho na kukusanya pesa za wananchi bila risiti bila kuulizwa. Kinachoendelea ni ushirikiano kati ya mkuu huyu na polisi kuhakikisha watu wanapata taabu na kutoa pesa bila maswali. Wanaouliza maswali juu ya matumizi ya pesa zao, wanakusanywa na kupelekwa polisi kwa kisingizio cha kupinga ujenzi. Huko hawatoki lazima walipe, tena zaidi ya kilichopangwa.

Mkuu huyu hafai. Urafi wa pesa umemzidi. Ujenzi wa mashule ni kujitolea. Kujitolea siyo kazi ya kusimamiwa na polisi na mkuu wa wilaya. Huu ni wizi! Malipo yasiyo na hesabu.
 

ya mufindi

JF-Expert Member
Dec 23, 2014
240
250
wewe mambo ya kusimuliwa ushakuja kulalamika huku,alipojenga shule muelimike utasema mzembe akijenga tena mkali binadamu hatuna jema
 

Zygot

JF-Expert Member
Apr 14, 2016
1,661
2,000
Mbunge wao ni nani vile! Ni yule jamaa bubu? aliondoka CHADEMA mukadhani ni mtaji, ndo mjue ni mwakilishi wa wasiojiweza. Asingeshindwa kudhibiti Mkuu wa wilaya asiyena mwelekeo. Wapo wabunge ambao wamekosana na wakuu wa wilaya kwa tabia kama hizo. Kama yeye ni bubu kama alivyo siku zote, mutalizwa kwa miaka 5.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom