Mkuu wa wilaya Ruvuma afumaniwa akimega

Habri hizi zimethibitishwa pia na kamanda wa polisi wa mkoa wa Ruvuma. Halafu eti bila ya aibu Madaha analalamika jamaa wamekwala simu, na pesa kiasi cha shilingi za kitanzania laki mbili! Bongo bana. Haya JK Tanzania Bila Ukimwi..... Sijui JK hakutoa semina elekezi juu ya hili!
 
Narudia tena acheni unafiki mambo yametokea usiku haukuwa nda wa kazi naomba ieleweke hivyo fanyeni uchunguzi kabla ya kuandika au kutoa maoni yenu. Msihukumu mtu kabla ya kufanya uchunguzi. Madaha atabaki na kuendelea kuwa mkuu wa wilaya kwa taarifa yenu. Ni mtu mmoja muwajibikaji tena mchapakazi.
 
Hapa ndipo pabaya,mtu kama huyu anafanyaje mambo kienyeji kiasi hicho?Inaonysha kuwa huyu mkuu wa wilaya anaendekeza sana chini.
Kwa maana hiyo Tanzania bila ukimwi haiwezekani hadi hivi sasa.
 
Mkuu wa Wilaya katika fumanizi tata




Na Gideon Mwakanosya



15th September 2009





headline_bullet.jpg
Akutwa na mwandishi wa habari wa kike
headline_bullet.jpg
Avamiwa hotelini, apigwa, aporwa fedha
headline_bullet.jpg
Kamati ya usalama yakutana kujadili





[FONT=ArialMT, sans-serif]Jeshi la Polisi mkoani Ruvuma linafanya uchunguzi wa kina kuhusiana na tukio lililotokea usiku wa kuamkia jana katika Hoteli ya Angoni Arms ambako Mkuu wa Wilaya ya Tunduru, Madaha Juma Madaha, akiwa amepumzika na mwandishi wa habari wa kike chumbani kwake alivamiwa na 'wahuni' na kisha kupigwa na kunyang'anywa simu, pete na fedha.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif] Habari zilizopatikana jana mchana ambazo zimethibitishwa na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ruvuma, Michael Kamuhanda, zilisema tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia jana majira ya saa 4 usiku katika hoteli hiyo.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif] Kamuhanda alisema kwa sasa polisi wanafanya uchunguzi ili kuwabaini watu waliohusika na tukio hilo ambalo alidai kuwa linaonekana kuwa la kupangwa.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif] Hata hivyo, aliongeza kuwa jitihada zinafanywa za kutafuta ukweli wa jambo hilo na kwamba mpaka sasa hakuna mtu aliyeshikiliwa na polisi na hakutaka kumtaja kwa jina mwandishi wa habari ambaye alikuwa amepumzika na Mkuu wa Wilaya.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif] Akizungumza na Nipashe, Mkuu wa Wilaya Madaha, alikiri kuvamiwa na watu asiowafahamu ambao walimpiga sehemu mbalimbali za mwili na kumsababishia mchubuko karibu na jicho la kulia.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif] Akijiandaa kurudi wilayani kwake majira ya saa 9:30 alasiri, Madaha alifafanua kuwa watu hao baada ya kumpigwa walimyang'anya Sh. 200,000, simu aina ya Nokia N78 yenye thamani ya Sh. 500,000 na pete ya dhahabu aliyokuwa ameivaa kwenye moja ya vidole vyake mkono wa kulia yenye thamani ya Sh. 300,000.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif] Alisema baada ya tukio hilo, alitoa taarifa polisi kwa njia ya simu na muda si mrefu polisi walifika kwenye eneo la hoteli, ingawa hawakufanikiwa kuwanasa wahusika.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif] Mkuu wa Wilaya Madaha alikiri kuwa akiwa kwenye chumba namba 109 katika hiyo alikuwa na mwandishi wa habari aliyemtaja kwa jina mwandishi huo, jina tunalisitiri kwa sasa kwa sababu hakuweza kumpata jana kuthuibitisha.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif] Madaha alisisitiza kuwa tukio hilo ni la kupangwa kwa sababu mwandishi huyo aliyekuwa naye ana rafiki yake ambaye pia ni mwandishi wa habari ambaye alikuwa ni mpenzi wake wa muda mrefu, pia jina tunasitiri kwa sasa kwa sababu ya kushindwa kumpata, hivyo anaamini kuwa mpenziwe huyo wa zamani alikuwa njama na waliomvamia kwa lengo la kutaka kumfedhehesha.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif] Katika hali isiyo ya kawaida Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Ruvuma chini ya Mwenyekiti Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Dk. Christine Ishengoma, ilikutana majira ya asubuhi.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif] Baada ya mkutano huo kamati hiyo iliwaita viongozi wa chama cha waandishi wa habari akiwemo Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Ruvuma, Juma Nyumayo, kwa lengo la kutaka taarifa hiyo isitolewe kwenye vyombo vya habari.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif] Nipashe ilimtafuta Nyumayo ili kupata ufafanuzi juu ya uongozi huo kuitwa na Kamati ya Ulinzi na Usalama ambaye alieleza kuwa ni kweli kwamba waliitwa na kuelezwa juu ya tukio lililotokea juzi la kuvamiwa kwa Mkuu wa Wilaya na kupigwa na watu wanaodhaniwa kuwa ni majambazi, lakini si kweli kwamba taarifa hiyo walikuwa hawataki kuitoa.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif] Aidha jitihada za kumtafuta Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Dk. Ishengoma kwa ufafanuzi juu ya tukio hilo na kutaka kujua ni hatua gani amezichukua kuhusiana, ziligonga mwamba.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif] Mapema Dk. Ishengoma aliiambia Nipashe kwa njia ya simu kwamba alikuwa akihudhuria kikao na akaahidi apigiwe baada ya muda. Hata hivyo, alipopigiwa jana saa 12:30 jioni simu yake ilikuwa imefungwa.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif] Kwa mujibu wa vyanzo vyetu vya habari, baadhi ya waandishi wa habari wanashikiliwa na polisi na baadhi ya watu wengine wanaodhaniwa kuwa ni majambazi waliohusika kupanga njama, kumjeruhi pamoja na kumnyang'anya fedha, simu na pete ya mkononi Madaha.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif] Hili ni tukio la aina yake kutokea mjini hapa likihusisha mahusiano ya mapenzi kati ya wanahabari na watendaji wa serikali, huku ikidaiwa kwamba wapo wanahabari wanaotumia miili yao kupata habari hali inayoweza kutafsiasriwa kama rushwa ya ngono.[/FONT]




CHANZO: NIPASHE
 
Narudia tena acheni unafiki mambo yametokea usiku haukuwa nda wa kazi naomba ieleweke hivyo fanyeni uchunguzi kabla ya kuandika au kutoa maoni yenu. Msihukumu mtu kabla ya kufanya uchunguzi. Madaha atabaki na kuendelea kuwa mkuu wa wilaya kwa taarifa yenu. Ni mtu mmoja muwajibikaji tena mchapakazi.

una uhakika bana???, au ndo ulikua unashikilia mapaja ya paparazi??
aaaarrrrrrggggghhh
 
Fidel80,
Huyu bwana katoa habari na kukimbia kwa sababu anajua alichokifanya,nahisi ndio ulieandaa mpango mzima.
 
Huyu mkuu wa wilaya na demu ndani ya chumba cha hotel du kazi kweli kweli labda kama hajaoa na si mkristo
 
Katika hali isiyo ya kawaida mkuu wa wilaya moja mkoani Ruvuma amefumaniwa akimmega {akivunja amri ya 6 na} paparazi jina la mkuu wa wilaya ni Juma Madaha mkuu wa wilaya ya Tunduru.

Jamani mboni hatutajiwi jina la huyo Paparazi, au ndo mambo ya Mapaparazi kufichiana ya kwao huku wakifichua ya wenzao? Tutajiwe tumjue kwani kama kuna kosa basi ni wote wametenda na sio DC peke yake
 
gazeti la kichina hilo, feki.
fidel80 yuko huko ananunua kahawa na kashuhudia timbwili timbwili lote A to Z.
Kama ni fake basi pigania wanyanganywe leseni. Kama ni fake kwanini unalisoma. Ndio walewale mnaolalama kodi zetu wakati mnalipa kodi kwa malkia.
 
Cha ajabu ni kipi? Kaiba mke wa mtu? Kabaka?huyu demu ni under age? Mwanafunzi? Jibu ni hapana sasa cha ajabu ni kipi?
kama hajaoa hakuna noma!ila kama kaoa du kazi kweli kweli maana wasukuma ndo zao nakumbuka babu yangu alikuwa na mke mmoja jirani yetu mzee mmoja msukuma akawa anasema ubize na nkema umo ubizaga mayu wako nai.
 
Jambo la kawaida tu kumega kama anataka kumfanya awe mkewe! Mwache ale raha
 
Hatutafika mbali kama tutakuwa na upeo mdogo wakuelewa mambo.Hili limetokea usiku lilipaswa kuwa ni jambo la kifamilia ingekuwa ni muda wa kazi tungeongea. Lakini watu wamelivalia njuga eti Raisi amtimue kazi kwa lipi tuweni makini sana.
 
Imesemwa siku zote ndege wafananao huruka pamoja, huyu Madaso anavyomtetea huyo mkuu wa wilaya mzinzi ni wazi nae pia ni mzinzi kama Madaha ndio maana haoni ubaya wa jambo hili! Swali zuri sana First lady kauliza Madaha Hajaoa? na kama ameoa anawezaje kusimama na kupinga uzinzi? Hata ukiisugua vipi shaba haiwezi kuwa dhahabu, madaso huwezi badili ukweli madaha juma Madaha ni Mzinzi
 
Back
Top Bottom