Mkuu wa wilaya Hai-Novatus Makunga kafanya alichoshindwa M/kit wa CCM Hai | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mkuu wa wilaya Hai-Novatus Makunga kafanya alichoshindwa M/kit wa CCM Hai

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Nicholas, Sep 15, 2012.

 1. Nicholas

  Nicholas JF-Expert Member

  #1
  Sep 15, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 25,132
  Likes Received: 2,355
  Trophy Points: 280
  Baada ya jaribio la kufa na kupona la mwenyekiti wa CCM kutaka kumng'oa mwenyekiti wa Kijiji Kwa-Sadala; hatimaye Novatus Makunga kafanikisha. Mwenyekiti huyo wa CCM ambaye anasemakana kuwa obsessed sana na hali ya raia kuikataa CCM alimfukuza kazi mwenyekiti wa kijiji hicho. Lakini watu wakamuuliza mamlaka kapata wapi? Hakuwa na jibu.

  Mwenyekiti aliyechoka akajaribu tumia msaada wa polisi ila nao wakionekana kuichoka CCM wakampa swali kama hilo.Leo Taarifa ya habari ya ITV inamwonyesha DC Makunga akimfukuza mwenyekiti huyo wa kijiji huku akiwa na watu walioandaliwa kuonyesha kuwa wamepangwa waongee nini. Kama inavyofahamika huyu mkuu wa wilaya aliwahi fanya kazi ITV na atakuwa mwepesi sana kwa mambo yamhusuyo na kisiasa.

  Cha kujiuliza ni kwamba kama mwenyekiti kashindwa kazi kwanini asitolewe kwa kura za wanakijiji kama walivyomchagua? kwani yeye si wa kuteuliwa na serikali.

  Taarifa iliyopo ni kwamba hata polisi wamemchoka huyu m/kiti wa CCM wilaya ya Hai. Amekuwa akiwahemea wamsaidie kuzui nguvu ya CHADEMA bila jijua kuwa yupo katik nyumba ya CHADEMA. Novatus nae akiwa kama makada wengine wa CCM anatafuta njia ya kujijenga kwa nguvu nyingi, mojawapondio hii ya kufanya kazi ya CCM.
   
 2. Ukwaju

  Ukwaju JF Bronze Member

  #2
  Sep 15, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 8,287
  Likes Received: 810
  Trophy Points: 280
  Jamaa yangu haijaeleweka nafuatilia ITV sijui km nitawahi lakini hebu dadavua ni Mwenyekiti wa Kijiji, au Mwenyekiti wa Chama aliyetimuliwa?
   
 3. mpinga shetani

  mpinga shetani JF-Expert Member

  #3
  Sep 15, 2012
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 3,268
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 145
  umeandika kwa lugha gani ?
   
 4. N

  Nova Makunga Verified User

  #4
  Sep 15, 2012
  Joined: Mar 24, 2012
  Messages: 59
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mkorakamili Mbona unachanganya habari ni dhahiri hujui unachoandika ndugu yangu tulia tuingie kwenye mjadala kama ulidanganywa kwamba mimi ni kilaza hapa umefika, soma sheria za mikutano ya vijiji ili nisije kuingia katika mjadala usio nawe usio na tija
   
 5. B

  BigMan JF-Expert Member

  #5
  Sep 15, 2012
  Joined: Feb 19, 2007
  Messages: 1,097
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 135
  Nimeangalia news ya itv kwa uelewa mdogo pale pana makundi lakini pia pana tuhuma ambazo zinaweza kuwa jinai mfano pembejeo za kilimo,hivyo dc makunga katumia busara na akukurupuka,namfahamu ni mtu mwenye uwezo mkubwa na issue hiyo haitamshinda mpeni muda na sidhani Kama ana lengo la kuibeba CCM
   
 6. hovyohovyo

  hovyohovyo JF-Expert Member

  #6
  Sep 15, 2012
  Joined: Jul 8, 2012
  Messages: 540
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Hata mie nashangaa. Anahitaji mhariri.
   
 7. Cha Moto

  Cha Moto JF-Expert Member

  #7
  Sep 15, 2012
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 945
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Duuh,
  Kumbe na mwenyewe yupo na hapa kakujibu,
  Ingawa binafsi hata sijaelewa lugha uliyotumia nadhani sasa mtaelewana
  Ukiandika kiswahili fasaha, tutajua cha kuchangia, kwa sasa pambana na huyu DC mwenyewe
   
 8. Ronal Reagan

  Ronal Reagan JF-Expert Member

  #8
  Sep 15, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,744
  Likes Received: 1,455
  Trophy Points: 280
  Hahaaa!
  Duh, kiswahili lugha pana. Huyu jamaa kaandika lakini kupata ujumbe ktk maandishi yake ni ngumu kweli! Tafadhali andika kiswahili cha kawaida ili tuelewe. Pia DC mwenyewe katia timu so wekeni mboga na ugali kati
   
 9. DALLAI LAMA

  DALLAI LAMA JF-Expert Member

  #9
  Sep 15, 2012
  Joined: Jan 31, 2012
  Messages: 8,617
  Likes Received: 401
  Trophy Points: 180
  Mkuu makunga vp?..
   
 10. Nicholas

  Nicholas JF-Expert Member

  #10
  Sep 16, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 25,132
  Likes Received: 2,355
  Trophy Points: 280
  -mkuu wa wilaya matusi hivyo? mi si mwandishi.

  -Kwani wewe ni mahakama sasa? kama kala pembejeo si angafunguliwa kesi?

  -Au ndio umefuta sera za ccm kuhamisha mhalifu badala ya kuburuzwa mahakamani?

  -Ulimchagua wewe? kwani usiwasaidie kuitisha kura?

  -kuna ubishi ulikuwepo kuhusu mtoa kauli upande wa pili ishara yake nini?

  -umetumia kifungu number ngapi cha sheria? na sheria ipi? tekeleza ilani ya ccm wewe. kwani nani hakujui enzi zile ulikuwa ukivizia offer za ccm katik mikutano na kampeni ndio wakakupa hizo nafasi za kike?
   
 11. Duduwasha

  Duduwasha JF-Expert Member

  #11
  Sep 16, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 5,142
  Likes Received: 2,176
  Trophy Points: 280
  Dah Mkuu Novamakunga Jibu Polepole Unajua Ukiwa unaoga na akija chizi kuchukua taulo lako na kukimia nalo usimkimbize ili kumyanganya kwani nyote mtaonekana Machizi... Mwaga Data polepole... wewe piga kazi wachana namaneno ya kisiasa.... kama semina elekezi inavyotaka... ile usiache kutupa dodoso whats goin on... wengine huwa hatupati muda wa kutizama News za tv so hapa tunadadavua na mtoa mada japo kachanganya maneno yake imekuwa ngumu kumuelewa...

  nilichoelewa CCM walishindwa kumuondoa mwenyekiti wao na wewe umeweza... kama anamakosa sheria ifuatwe tu... ndio cha muhimu
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 12. Nicholas

  Nicholas JF-Expert Member

  #12
  Sep 16, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 25,132
  Likes Received: 2,355
  Trophy Points: 280
  mwenyekiti wa ccm kaenda mtoa kisiasa.nova kama kiherehere kaenda mtoa kwa nguvu kwa vile mwenyekiti kashindwa kwa vile aliulizwa kataka mtoa kama nani?

  novatus kwa vile ana kivuli cha serikali basi akaenda saidia majeshi.Ila naye kwa vile ni kilaza hajui kuwa alipaswa saidia ccm zoezi la kumfungulia mashitaka.Pia asaidie wana kijiji wapige kura za kumtoa. huyo mwenyekiti wa ccm yupo busy sana kupambana na watu wasiopenda ccm.hajui mipaka ya ccm na serikali.hakuna aliyekataa kuwa kosa linaadhibiwa ila hii ndio njia sahihi?

  huyu kilaza hajajibu kama njia aliyotumia ni sahihi.kwa vile hata refresher course hakupewa.na muda wote akifanya kazi ya habari hakuweza hata soma sheria kwa vile alikuwa akitumikia mabwana apate kiti maalumu .mwenzie bisanya alisoma.atafanya sana kazi ya ccm.
   
 13. Nicholas

  Nicholas JF-Expert Member

  #13
  Sep 16, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 25,132
  Likes Received: 2,355
  Trophy Points: 280
  nova makunga
  kesho kamrudishe. wananchi wamkatae kwa kura na wao ndio wampeleke mahakamani. Sasa umeshatoa hukumu? kalipa nini? au kapewa adhabu gani?

  net ni ya watu ningesubiri jibu
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 14. Nicholas

  Nicholas JF-Expert Member

  #14
  Sep 16, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 25,132
  Likes Received: 2,355
  Trophy Points: 280
  nimekumbuka kesho napanda kwasadala mjini tunaandaa maandamano na tunamrudisha mwenyekiti wetu siku yoyote.naomba na hiyo habari uwapigie itv waje wairushe.si ndio kazi yako?umewahi irusha ukadhani umetoka?
   
 15. A

  Africa_Spring JF-Expert Member

  #15
  Sep 16, 2012
  Joined: Jun 16, 2012
  Messages: 428
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hivi vigezo gani vinatumika kuwapa watu ukuu wa wilaya na ukuu wa mikoa....maana sasa hivi kila siku utasikia muandishi flani ameteuliwa kua mkuu wa mkoa......hebu tuwekewe sheria tuzijue vizuri.naionea huruma nchi yangu maana kila kukicha tunaletewa vituko....kuanzia bungeni mpaka wilayani.....kweli tanzania kichwa cha mwenda...........kuzimu
   
 16. N

  Nova Makunga Verified User

  #16
  Sep 16, 2012
  Joined: Mar 24, 2012
  Messages: 59
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mkorakamili

  Ndugu yangu moja sijamfukuza mtu madarakani lakini pia sijaeleza nani kaiba pembejeo,ule ni mkutano wa hadhara kati ya wananchi wa kijiji cha kwasadala na mkuu wa wilaya, wananchi wale wana kero zao kibao za muda mrefu,lakini pia vikao vya vijiji vina sheria na kanuni zake zikiwemo namna ya kuviitisha, uendeshaji na jinsi ya kutoa maamuzi.

  Masuala uliyoongelea bado ni tuhuma mfano la wizi wa pembejeo na mengine mengi yakiwemo ya kukuza maeneo ya ardhi na kadhalika yakiwahusu mwenyekiti wa kijiji na ofisa mtendaji wake.

  Nilichofanya ndugu yangu ni kuwaweka nje ya ofisi viongozi hao ili wataalamu wangu watano ambao ni pamoja mwanasheria wa halmashauri, mkaguzi wa mahesabu,afisa ardhi na katibu tawala wa wilaya watumie muda wa siku Saba kutafuta ukweli wa tuhuma hizo na baada ya hapo tutaita mkutano wa kijiji utakaofuata taratibu na kanuni za kuitisha vikao va vijiji.

  Uamuzi wa mwenyekiti utafikiwa na wananchi wenyewe na la mtendaji wa kijiji ni la mwajiri wake ambapo kiutaratibu ni mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya.

  Kama kutakuwa na suala lolote la kijinai tutapeleka katika mamlaka husika, hayo ndiyo maamuzi yangu katika kikao kile ndugu yangu.
   
 17. N

  Nova Makunga Verified User

  #17
  Sep 16, 2012
  Joined: Mar 24, 2012
  Messages: 59
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ndugu yangu nafahamu sana taratibu na kanuni wenye uwezo wa kumfukuza mwenyekiti wa kijiji ni wana kijiji wenyewe na siyo dc naomba fuatlia vizuri sana kikao changu pale ,mtoa mada amepotosha lakini pia suala la waandishi wa habari liko wazi wanaweza kufuatilia habari kutegemeana na source,mara nyingi ni wananchi wenyewe wanawapa taarifa hata wewe na maandamano unayokusudia watafute mimi nimetoka katika taaluma hiyo naifahamu na siwezi kuwazuia kutimiza majukumu Yao
   
 18. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #18
  Sep 16, 2012
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,822
  Likes Received: 10,120
  Trophy Points: 280
  Nova si ulifanya usaili Mzee? Mbona lugha yako ngumu kumeza?
   
 19. N

  Nova Makunga Verified User

  #19
  Sep 16, 2012
  Joined: Mar 24, 2012
  Messages: 59
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ndugu yangu nipo makini na uwezo ninao lakini ningeshauri hizi taarifa kabla ya kuchangia mada tuwe nasi tunajiridhisha kama ziko sahihi wengi wana post vitu ambavyo si vya kweli na hivyo kuonekana kana kwamba hatufai na wengi wetu tunashindwa kutoa ufafanuzi mfano hii taarifa nafahamu lengo la mtoa mada alitaka katika mkutano ule wa hadhara niamrishe watu wapige kura ya kumuondoa madarakani mwenyekiti lakini jiulinze ndugu yangu huo ni utaratibu wa mkutano wa kijiji ?

  Lakini pia amejichanganya kwa kudhani mimi nimemuondoa nilichofanya ni kuwasaidia ili baadaye waweze kutoa maamuzi sahihi,nawasilisha
   
 20. N

  Nova Makunga Verified User

  #20
  Sep 16, 2012
  Joined: Mar 24, 2012
  Messages: 59
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ndugu yangu fuatilia vizuri mwenyekiti wenu sijamfukuza na mkutano nilizungumza kwamba wenye mamlaka ya kumuondoa mwenyekiti ni wanakijiji wenyewe,tuhuma zimetolewa ebu tupate majibu zitaletwa kwenu mtaamuwe wenyewe.
   
Loading...