Mkuu wa wilaya Hai-Novatus Makunga kafanya alichoshindwa M/kit wa CCM Hai

Mkuu kumbe ukuu wa Wilaya unapatikana kwa interview ya wazi? Unaijua katiba mkuu? Kumbe hata hujui ukuu wa wilaya unapatikanaje! Naona wewe unajua rabbish tu. Jishughulishe basi hata kidogo ili ujue ukuu huo unapatikanaje kisha uende kwenye tume ya katiba ili utusaidie kutoa mawazo ili tuje kupata wakuu wa wilaya kwa vigezo na interview za wazi!
Wee upepo, akili yako umeiacha wapi? Huo ulikuwa ni mfano tu, na wala sikuwa namaanisha hivyo. Kwamba, yeye kateuliwa lakini hajui ni kwanini au kwa vigezo vipi kateuliwa, is that not stupidity?
 
Ndugu yangu nipo makini na uwezo ninao lakini ningeshauri hizi taarifa kabla ya kuchangia mada tuwe nasi tunajiridhisha kama ziko sahihi wengi wana post vitu ambavyo si vya kweli na hivyo kuonekana kana kwamba hatufai na wengi wetu tunashindwa kutoa ufafanuzi mfano hii taarifa nafahamu lengo la mtoa mada alitaka katika mkutano ule wa hadhara niamrishe watu wapige kura ya kumuondoa madarakani mwenyekiti lakini jiulinze ndugu yangu huo ni utaratibu wa mkutano wa kijiji ? Lakini pia amejichanganya kwa kudhani mimi nimemuondoa nilichofanya ni kuwasaidia ili baadaye waweze kutoa maamuzi sahihi,nawasilisha

Bwana Novatus Makunga, wengine tunajua kwanini ulipewa ukuu wa wilaya, just soon baada ya uchaguzi mdogo wa Arumeru Mashariki. Kwahiyo kama unayo nia njema kuitumia fadhila hiyo kwa manufaa ya wananchi bila kujali itikadi zao, well and good. Hatuwezi kukulaumu maana huo ndo mfumo uliopo wa kupata wakuu wa wilaya kwasasa.
 
Wee upepo, akili yako umeiacha wapi? Huo ulikuwa ni mfano tu, na wala sikuwa namaanisha hivyo. Kwamba, yeye kateuliwa lakini hajui ni kwanini au kwa vigezo vipi kateuliwa, is that not stupidity?

Mkuu umetumwa au? Njoo taratibu acha matusi. Kuwa muungwana. Nadhani nimemaliza. Karibu sana JF
 
Salama ndugu yangu tunawatumikia wananchi na wana haki ya kutuhoji,kutushambulia na pia kupata majibu sahihi
aa wapii!!!mnawatumikia wananchi kwa kukaa maofisini!!!..natambua hapo Kwasadala si mbali sana na Boma N'gombe yalipo makao makuu ya wilaya ya Hai ambapo ipo ofisi yako kama dc......Nachotaka kusema ni kwamba nyie ma dc wa JK mmechaguliwa kukidhi matakwa ya kisiasa zaidi ya kuwatumikia wananchi wote bila kujali itikadi zao....na ndio sababu kila kukicha tunasikia mkitoa maamuzi ya ajabu ajabu kwenye kazi zenu.....wewe kama dc wa Hai(wilaya yangu)..

Embu niambie umetembelea kata/tarafa/vijiji vya mbali ya hapo boma lini??? Mfano..ebu niambie ni lini(tangu umeteuliwa)ulitembelea tarafa ya Lyamungo.....Machame.....kwenye vijiji vya Kilanya na Lyamungo Kati..... sehemu ambako hata barabara hazipitiki!!!.....nikukumbushe tu kuwa.... Lyamungo ndiko kwenye shule maarufu ya Lyamungo secondary iliyotoa viongozi wengi nchi hii......na ndiko kuna Lyamungo Coffee Research Institute...

Taasisi pekee makini ya utafiti wa kahawa tz....pia kijiji cha Kilanya...kijiji kinachopakana na mlima kilimanjaro na kina moja ya routes za kupanda mlimani....na ni kijiji ambacho hakijatembelewa na kiongozi yeyote wa serikali(si rais, si PM wala DC)kwa miaka sikumbuki mingapi!...Sasa kwa vile unajifagilia kuwatumikia wananchi...ebu fanya tu safari siku moja ya kutembelea kijiji cha kilanya na lyamungi kati ukajionee hali ya barabara kule...alafu uje hapa ujifagilie......

Hivi vijiji havina hata kituo cha afya....mtu akiugua lazima asafirishwe kwenda Machame hospital au Kibosho hospital au Mawenzi hosp au KCMC.....hospitali ambazo ziko mbali kabisa na katika tarafa nyingine....na hakuna hata chombo cha usafiri kwa wagonjwa.....miaka yoote tangu uhuru hapajawa na kituo cha afya maeneo haya....acheni siasa kwenye shughuli za maendeleo ya watanzania.....

Kumbuka wewe unamwakilisha JK hapo wilayani Hai......tembelea maeneo ya mbali na hapo boma ujionee mwenyewe.......
 
Nova sasa atuletee riport za kwasadala kama kweli ni mwadilifu.Otherwise tutaleta ztu halafu aje piga tumba kuwa kaonewa.
 
Nova si ulifanya usaili Mzee? Mbona lugha yako ngumu kumeza?

teh teh..si alishafanya wakati anachakachua news?Hujui kuwahi toa news za kuwafagilia magamba sana unaukwaa kam betty Mkwasa,huu ukichakachua za wapinzania ili zionekane hazina uzito ni qualificationa mojawapo ya kukusogeza palipo na office ya mkuu wa wilaya ili ukafanye kazi vyema.
 
Mbona hueleweki, ww ni Dhaifu, jipange upya unapoandika hbr. kalale ukiamka andika tena.
Dhaifu ni president wenu mliyemchagua kwa papara zenu peke yenu.Km umeshaniona kuwa president ahsante sana.Mlimchagua kwa sifa duni kama vile nakwenda oa zenj: kama ni handsome, mtu wa watu, naingia disco, anapenda u-miss na ujinga kama huo.Kila kundi lilikuwa na sifa za kijinga kama hizi kumchagua.
 
Nova report ipo wapi .Au ndio ndio ahadi ya kutorudi ktk hii thread ni kubwa kuliko kutatua tatizo la wananchi kwa staili ya wananchi na si ya magamba?
 
kazi kweli
 
mkorakamili

Ndugu yangu moja sijamfukuza mtu madarakani ylakini pia sijaeleza nani kaiba pembejeo,ule ni mkutano wa hadhara kati ya wananchi wa kijiji cha kwasadala na mkuu wa wilaya, wananchi wale wana kero zao kibao za muda mrefu,lakini pia vikao vya vijiji vina sheria na kanuni zake zikiwemo namna ya kuviitisha, uendeshaji na jinsi ya kutoa maamuzi.

Masuala uliyoongelea bado ni tuhuma mfano la wizi wa pembejeo na mengine mengi yakiwemo ya kukuza maeneo ya ardhi na kadhalika yakiwahusu mwenyekiti wa kijiji na ofisa mtendaji wake.

Nilichofanya ndugu yangu ni kuwaweka nje ya ofisi viongozi hao ili wataalamu wangu watano ambao ni pamoja mwanasheria wa halmashauri, mkaguzi wa mahesabu,afisa ardhi na katibu tawala wa wilaya watumie muda wa siku Saba kutafuta ukweli wa tuhuma hizo na baada ya hapo tutaita mkutano wa kijiji utakaofuata taratibu na kanuni za kuitisha vikao va vijiji.

Uamuzi wa mwenyekiti utafikiwa na wananchi wenyewe na la mtendaji wa kijiji ni la mwajiri wake ambapo kiutaratibu ni mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya.

Kama kutakuwa na suala lolote la kijinai tutapeleka katika mamlaka husika, hayo ndiyo maamuzi yangu katika kikao kile ndugu yangu.

Mkuu wa wilaya.... Hiyo mwenyekiti angekua wa chadema ungeingilia kati?
 
Mkuu wa wilaya.... Hiyo mwenyekiti angekua wa chadema ungeingilia kati?

ndugu yangu uliza, kwa matatizo na kero za wananchi nafanya kazi sana na wenyeviti na viongozi bila kujali itikadi zao za vyama kwa bahati mbaya mengi hayatangazwi na wengi hawamo humo ndani,lakini nikirudi kwenye swali lako kwa ufupi Sikutaka kuingia kwa undani kuelezea tatizo lililopo pale kwasadala,Ni kubwa na la muda mrefu na lingeweza kuleta hata umwagaji wa damu na ofisi ya kijiji ilifikia kufungwa hivyo kwa vyovyote vile ilikuwa lazima nichukuwe hatua,lakini la zaidi yule mwenyekiti wa kijiji ni wa ccm lakini kwa kukusaidia kama si mkazi wa hai hii post itakuchanganya sana,mwenyekiti wa ccm hai dr Uronu hajawahi kwenda pale kwa tatizo hili lakini hiyo siyo issue,kubwa ni kuwepo kwa tatizo,Nilichofanya ni kufuata taratibu na sheria za uendeshaji wa serikali za mitaa kuanzia vitongojini hadi kata na wananchi wameshafanya maamuzi yao katika mkutano wao uliofanyika juzi jumatatu.
 
Nova report ipo wapi .Au ndio ndio ahadi ya kutorudi ktk hii thread ni kubwa kuliko kutatua tatizo la wananchi kwa staili ya wananchi na si ya magamba?

sijui na sidhani kama matatizo ya wananchi pale kwasadala yanaweza kutatuliwa humo ndani ya jf,lakini pia nilisikitika sana kuniweka katika mazingira ambayo hayakuwa dhamira yangu ambayo ni kutaka kupata suluhu la kudumu la mgogoro ule,suala la magamba ama siyo magamba halina mantiki kwangu,kwa kifupi sana ndugu yangu nilishakamilisha utaratibu kwa kufuata sheria zinazosimamia uendeshaji wa serikali za mitaa katika ngazi za vitongoji na vijiji na wananchi kupitia mkutano wao wa kijiji uliofanyika juzi jumatatu wameshafanya maamuzi kwa kuwa wewe ni mwenyeji wa hai ni vyema kama ulivyoanzisha hii mada basi ungefuatilia kwa walioshiriki katika mkutano ule ambao ulimalizika saa mbili usiku
 
ndugu yangu uliza, kwa matatizo na kero za wananchi nafanya kazi sana na wenyeviti na viongozi bila kujali itikadi zao za vyama kwa bahati mbaya mengi hayatangazwi na wengi hawamo humo ndani,lakini nikirudi kwenye swali lako kwa ufupi Sikutaka kuingia kwa undani kuelezea tatizo lililopo pale kwasadala,Ni kubwa na la muda mrefu na lingeweza kuleta hata umwagaji wa damu na ofisi ya kijiji ilifikia kufungwa hivyo kwa vyovyote vile ilikuwa lazima nichukuwe hatua,lakini la zaidi yule mwenyekiti wa kijiji ni wa ccm lakini kwa kukusaidia kama si mkazi wa hai hii post itakuchanganya sana,mwenyekiti wa ccm hai dr Uronu hajawahi kwenda pale kwa tatizo hili lakini hiyo siyo issue,kubwa ni kuwepo kwa tatizo,Nilichofanya ni kufuata taratibu na sheria za uendeshaji wa serikali za mitaa kuanzia vitongojini hadi kata na wananchi wameshafanya maamuzi yao katika mkutano wao uliofanyika juzi jumatatu.

thank you Nova
 
mheahimuwa DC,nakuomba utembelee wilaya yako, najua ww n mchapa kaz, uspo fanya kaz utaaibika kama juzi halmashauri ilivyo aibika mbele ya mkuu wa Mkoa Gama kwenye kikao na waalimu.napenda kukumbusha uziangalie shule kongwe kama elyamungo na machame girlys.machame imeoza hata kwenye rank haipo tena,mkurugenzi,makange na Afsa taaluma wawajbike kuuacha uongozi ule pale ile hali umeshindwa ongoza shule na kuweka mikakati ya kufaulisha badala yake kuchonganisha waalimu na almashauri na kuwa hamisha.tafazali mkuu maslahi ya Mtu binafsi yasisababishe watoto wetu kupata sifuri. tembelea shule hii ongea na wanafunzi na waalimu uone uozo.hapoulipo fungua matokeo ujionee ya miaka mitatu mfululizo(09,10,2011).maytake shule kongwe kama machame wapewe wakina mama watu wazima na si sampuli ya materu, kashindwa shule.naomba kuwasilisha.
 
Nashukuru nategemea ni mwalimu nategemea ushirikiano wenu kama jicho la tatu moja kati ya shule hizo nimetembelea sitaongelea kwani kuna kazi inafanyika,naomba ushirikiano
 
Mkuu wa wilaya.... Hiyo mwenyekiti angekua wa chadema ungeingilia kati?

Mimi nilichoongelea ni Mwenyekiti wa CCM kufany ajaribio likagoma,akachukua polisi boma wengine wakagoma.Akamwita Nova ambaye kazi yake rasmi ni kulinda chama ktk wilaya yake.Otherwise sijui kazi nyingine kama zinamsaidia kwa lolote ku survive politically.

Huyu Jamaa kwa vile bado ana influence ktk media kaenda play kamikaze kwa staili yake.Sijasema kwa vile ni CCM ingawa this time CCM ndio wanachanganya office za serikali na utendaji wa magamba.Hata ingekuwa Chadema ningesema the same.
 
sijui na sidhani kama matatizo ya wananchi pale kwasadala yanaweza kutatuliwa humo ndani ya jf,lakini pia nilisikitika sana kuniweka katika mazingira ambayo hayakuwa dhamira yangu ambayo ni kutaka kupata suluhu la kudumu la mgogoro ule,suala la magamba ama siyo magamba halina mantiki kwangu,kwa kifupi sana ndugu yangu nilishakamilisha utaratibu kwa kufuata sheria zinazosimamia uendeshaji wa serikali za mitaa katika ngazi za vitongoji na vijiji na wananchi kupitia mkutano wao wa kijiji uliofanyika juzi jumatatu wameshafanya maamuzi kwa kuwa wewe ni mwenyeji wa hai ni vyema kama ulivyoanzisha hii mada basi ungefuatilia kwa walioshiriki katika mkutano ule ambao ulimalizika saa mbili usiku

Nova usipende ongea kwa style ya ku appease watu wala kujaribu soliciting upendeleo wa watu.Ulikwenda Kwa sadala kujaribu funja mfumo uliopo ili CCM ipate fanya kazi bila kubanwa.Huyo mwenyekiti alionekana vizuri akilia na polisi ili kupata support yao kwenda kumchomoa kwa nguvu.Polisi wengine wakaleta taabu.Kama ni Jumatatu ndio unapata ujasiri wa kujibu leo, hili swali ni la lini?Sasa unataka ondoa nini "utashi wa kisiasa" ulioutumia? .Im happy umejituma ingawaumeweka uongo mwingi sana ila umejituma ukijua kuna watu wanachukia vitabia hivyo.Kwa sadala ni kwangu na masuala ya ujambazi pale ndio "mchangani kwa ma mastaa wa hiyo mambo", sasa ukitaka sema kuwa ingetokea umwagaji damu pale si issue ya leo.Na long time huwa wanakula na watu kama nyinyi na viongozi wa polisi.

Nipo mtwara naganga life nikirudi nitapata majibu mazuri zaidi ya kusoma na kuambiwa ktk simu.Ila ujue siku mwenyekiti wa CCM anaomba polisi waka mwangosi kijiji nilikuwa napata Boma.
 
Mimi nilichoongelea ni Mwenyekiti wa CCM kufany ajaribio likagoma,akachukua polisi boma wengine wakagoma.Akamwita Nova ambaye kazi yake rasmi ni kulinda chama ktk wilaya yake.Otherwise sijui kazi nyingine kama zinamsaidia kwa lolote ku survive politically.

Huyu Jamaa kwa vile bado ana influence ktk media kaenda play kamikaze kwa staili yake.Sijasema kwa vile ni CCM ingawa this time CCM ndio wanachanganya office za serikali na utendaji wa magamba.Hata ingekuwa Chadema ningesema the same.

I think you missed my point... swali lilielekezwa kwa Mkuu wa wilaya sio wewe
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom