Mkuu wa Wilaya ya Busega Mkoani Simiyu aagiza wanaomiliki fisi wawachunge wasidhuru watu

Nyendo

JF-Expert Member
Jun 4, 2017
1,194
4,115
Mkuu wa Wilaya ya Busega Mkoani Simiyu, Faiza Salim amemuagiza Mwenyekiti wa Kijiji cha Nyamikoma, Kata ya Kabita Wilayani humo kuwaita Waganga wa tiba asilia Kijijini hapo ili kuwaomba Wawachunge na kuwadhibiti fisi ili wasidhuru Watu kwakuwa fisi hao inaaminika wanamilikiwa na baadhi ya Watu kijijini hapo ambao huwatumia kwenye masuala ya kishirikina.

DC ametoa agizo hilo wakati akiwa kwenye kikao cha kusikiliza kero za Wananchi Kijijini hapo ambapo Mwananchi Emmanuel Augustine amelalamikia uwepo wa fisi wanaosumbua Watu “Kero yangu ni wanyama wanatusumbua sana, viboko wanatusumbua fisi nao wanaunguruma, mpaka saa moja fisi wapo ndani , kero ya pili ningebanwa haja sidhani kama ningeenda kujisaidia wapi soko hili kubwa lakini hatuna choo, Mh (DC) hata wewe sasa hivi ukibanwa utaenda wapi?, liangalie soko lipate choo, Diwani unaongea mambo mengi hautukumbuki”

Akijibu hoja hizo DC Faiza amesema “Fisi wanamilikiwa na Watu, Mwenyekiti itisha Waganga wako wa tiba asilia wazungumze kuhusu fisi wawalinde fisi wao, lindeni fisi wenu wasidhuru Watu, mkiwaachia hivihivi mnamtisha Mzee Emmanuel anashindwa kufanya kazi nyingine kwasababu ya fisi”

“Mwenyekiti itisha Waganga wako wa tiba asili waambie wachunge fisi wao, Mimi sitaki kuingia mgogoro na wao kuanza kuwaua fisi wasije wakanifuata nyumbani kwangu, maana nikianza kuwaua hapa kuna DC alikuwa anawaua wanamfuata mpaka kwake Mimi sitaki malizana nao ukishindwa niite nije kuwaomba jaman lindeni zana zenu”
 
Huko kuna ma master balaa, kuna gari iligonga fisi, asubuhi kijiji kizima kikatoka mbio kwenda kukata mabaki ya fisi aliyegongwa, waliokosa mabaki wakawa wanazoa damu na mchanga almuradi wasikose.

Nassa ndio baba lao, imetoa akina Chenge, Mkuu wa Majeshi Mabeho, majaji na watu wakubwa, lakini hapaendelei, watu wanakimbilia lamadi wanaogopa uchawi
 
Back
Top Bottom