Mkuu wa shule alisema si muelewane tu! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mkuu wa shule alisema si muelewane tu!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Annael, Sep 20, 2012.

 1. Annael

  Annael JF-Expert Member

  #1
  Sep 20, 2012
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 13,228
  Likes Received: 10,195
  Trophy Points: 280
  Ilikuwa mwaka 1995 nikiwa niko kidato cha nne. Unajua tena shule ambayo nilisoma ilikuwa ya wavulana tu na isitoshe haina A-Level. Mwaka huo mimi nilikuwa kinala hapo shuleni japo shida ya maji ilikuwa inatusumbua. Kila siku asubuhi na jioni tulikuwa tukifuata maji mbali kidogo kwaajiri ya matumizi yetu na ya shule.

  Basi bwana, tukawa tumefunga likizo fupi ya kama wiki moja hivi, aa mimi nikaenda nyumbani kuwasalimia wazazi, unajua wazazi walinipenda sana maana nilikuwa kichwa darasani.

  Tulipofungua bwana ah! ah! ah! tulikuwa tumepata mwalimu wakike dah! alikuwa mzuri bwana, wee acha tu alikuwa anatufundisha biology na chemistry. Yaani alikuwa ametoka chuo, bado mbich kabisa amenona.

  Si unajua tena pale shule! mimi nilikuwa naonekana mkubwa kiasi fulani, ndevu za kiuchokozi nazo zilikuwa zinatokeza!
  Uchu wa njaa ya mda mrefu ukanipanda.

  Mwalimu akiwa anafundisha darasani akili zangu zinahama kabisa, na ninajikuta nimemvua nguo kwenye mawazo yangu. Sauti yake ilinikosha sana na kunifanya niduae, pamoja na hayo kilichoniua ni pale alivyo penda kuniita na kunitaja taja darasani.

  Basi bwana siku moja aliniita maabala akaniambia nimsaidie kufanya usafi. Dah siku ile niliapa hakiani lazima liwalo na liwe kama kufukuzwa shule poa. Wakati tunaendelea na usafi nikamsifia kidogo, si akatabasamu, nikachombeza neno jingine "Mwalimu usiku silali nakuwaza wewe nihurumie nisiferi mtihani" Haa akauliza kivipi? Si nikamsogelea nikajua sasa ameingia mtegoni, Nikamwambia nakutaka wewe uniliwaze. Akawaka akasema atanipeleka kwa mwalimu mkuu.

  Maisha yangu yakawa matatani. Basi bwana mwalimu wa zamu akaja darasani na akasema nimuone mwalimu mkuu.
  Kuingia ofsi ya mwalimu mkuu uso kwa uso na kipenzi changu mwalimu. Mkuu akamuuliza ehe Mwalimu tatizo ni nini/ akaeleza. Mwalimu mkuu akasema kumbe hilo si muelewane tu wewe si mwalimu?

  Unajua baada ya hapo kilitokea nini.......
   
 2. platozoom

  platozoom JF-Expert Member

  #2
  Sep 20, 2012
  Joined: Jan 24, 2012
  Messages: 7,313
  Likes Received: 2,271
  Trophy Points: 280
  Hadithi hii inatufundisha nini?
   
 3. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #3
  Sep 20, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,463
  Trophy Points: 280
  shule hizi zitafunguliwa lini?
   
 4. Bilionea Asigwa

  Bilionea Asigwa JF-Expert Member

  #4
  Sep 20, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 12,627
  Likes Received: 9,838
  Trophy Points: 280
  hii stoei yako inekua ya kweli ingekua inatufundisha nini??
   
 5. bornagain

  bornagain JF-Expert Member

  #5
  Sep 20, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 3,389
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 135
  Kilichotokea unakijua mwenyewe lakini kwa kugues lazima wewe ulifeli mitihani na ulipata zero
   
 6. lara 1

  lara 1 JF-Expert Member

  #6
  Sep 20, 2012
  Joined: Jun 10, 2012
  Messages: 15,444
  Likes Received: 10,121
  Trophy Points: 280
  Umenikumbusha mbaali kweli! Enzi za Shebby Robby kuna ticha flani alikuja PT alikuwa anasoma UDSM, Damu chngaaa kabisa, ndani ya damu mbichi!!! basi bwana akifundisha PHYSICS mimi akili yote ipo kwenye BODY CHEMISTRY, yaani we acha tu, Kama angeomba jimbo nadhani angepita bila KUPIGWA! Walimu ni wito! Physics nilipata D, ushauri kwa WAKUU WA VYUO wasiajiri maticha HANDSOME!!!!!
   
 7. Annael

  Annael JF-Expert Member

  #7
  Sep 20, 2012
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 13,228
  Likes Received: 10,195
  Trophy Points: 280
  Aaa wewe mwaka uliofuata nilijiunga na kidato cha tano.
   
 8. bornagain

  bornagain JF-Expert Member

  #8
  Sep 20, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 3,389
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 135
  Kama ni hivo basi uliambulia za uso
   
 9. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #9
  Sep 20, 2012
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,263
  Likes Received: 21,997
  Trophy Points: 280
  ume sup, sasa wamekurudisha chekechea
   
 10. Annael

  Annael JF-Expert Member

  #10
  Sep 20, 2012
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 13,228
  Likes Received: 10,195
  Trophy Points: 280
  Aaah mpaka sasa mbona niko okey ndio maana nike JF kwa great thinkers!
   
 11. Annael

  Annael JF-Expert Member

  #11
  Sep 20, 2012
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 13,228
  Likes Received: 10,195
  Trophy Points: 280
  Za uso zipi tena wakati nilianza kujilia kiulainiiii.
   
 12. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #12
  Sep 20, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 301
  Trophy Points: 160
  ikatokea baoloji
   
 13. STALLEY

  STALLEY JF-Expert Member

  #13
  Sep 20, 2012
  Joined: May 5, 2012
  Messages: 530
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 45
  sasa huyo alienda kushtaki ili iweje
   
 14. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #14
  Sep 20, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Ikiwa wewe ndiye uliyekuwa "kichwa" darasani, hao miguu sijui walikuwaje?
   
 15. SnowBall

  SnowBall JF-Expert Member

  #15
  Sep 20, 2012
  Joined: Sep 13, 2011
  Messages: 3,067
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  Mkuu toa kwanza boriti jichoni kwako huh!!
   
 16. BHULULU

  BHULULU JF-Expert Member

  #16
  Sep 20, 2012
  Joined: Jun 28, 2012
  Messages: 4,911
  Likes Received: 121
  Trophy Points: 160
  Hahahaha!Umemuweza
   
 17. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #17
  Sep 21, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Mimi sikuwa "kichwa" darasani.
   
 18. Annael

  Annael JF-Expert Member

  #18
  Sep 21, 2012
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 13,228
  Likes Received: 10,195
  Trophy Points: 280
  Si unajua tena bwana mimi sio mzuri wa kiswahili!? Lakini ahsante kwa kunikosoa nitajirekebisha katika kuandika.
   
 19. HorsePower

  HorsePower JF-Expert Member

  #19
  Sep 21, 2012
  Joined: Aug 22, 2008
  Messages: 3,617
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145

  SnowBall umenifurahisha, sijui kwanini baadhi yetu tunashupalia hizi lugha wakati inajulikana wazi kuwa wengi wetu tumeanzia lugha za makabila yetu na kusahau Kisw na Kiingereza tumejifunzi shuleni? Mi nakumbuka wakati nasoma huko vijijini kuna watu hata kuongea kiswahili ilikuwa shida achilia mbali lugha zingine.

  Ni vyema tukajitahidi kuelewa mtoa mada anataka kuleta ujumbe gani then tukauchambua huo.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 20. mtanzania in exile

  mtanzania in exile JF-Expert Member

  #20
  Sep 21, 2012
  Joined: Feb 17, 2012
  Messages: 245
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  ndio, ulizindukana na kugundua kuwa yoote ilikuwa ni ndoto tu!!!!!
   
Loading...