Mkuu wa mkoa wa Mwanza, Jiji limekushinda, Jitafakari! Ni pachafu sana

ngebe

JF-Expert Member
Jun 8, 2020
1,789
5,105
Wakuu,

John Mongella kawa mkuu wa mkoa wa Mwanza kwa muda sasa, lakini cha ajabu hakuna jipya lolote aliloonyesha hususa ni Mwanza jiji ambapo ndio kioo cha Mkoa mzima wa Mwanza.

Jiji la Mwanza kwa sasa lipo hovyo hovyo sana halina mpangilio wowote ukilinganisha na lilivyokua kipindi cha nyuma kabla ya ujio wake.

Mitaa ya jiji sasaivi ni michafu sana inanuka, hadi swala la usafi tu limemshinda Mongella.

Ikumbukwe kipindi cha nyuma mwanza iliwai kuwa jiji la kwanza East Africa kwa usafi, lakini hivi sasa chini ya Mongela mwanza imebadilika sana ndio jiji chafu zaidi Tanzania.

Tembelea maeneo mbalimbali ya jiji mambo ni ovyo barabara nyingi sasaivi hazina Taa ni giza tu,

Bustani za Bismark pale Kamanga zilikuwa ni maarufu sana na zilikua na muonekano mzuri hata kuvutia watalii na watu mbalimbali kuja kufanyia shooting lakini hivi sasa zimekua ni vichaka na madimbwi ya maji.

Maeneo yliyokuwa yanapitiwa na reli kuelekea chakechake sasaivi ni mapoli makubwa wakati yapo jijini kabisa.

Mitaa ya jiji imegeuka dampo kana kwamba mkuu wa mkoa huwa hatembelei hata kuangalia jiji lake, vifusi vya matope na takataka vimetapakaa jijini zaidi ya miezi, mvua inanyesha inasambaza.

Kiufupi Mongella hana jipya aliloleta Mwanza
ubunifu wake ni zero

Heri hata Paul Makonda angeletwa Mwanza akamfundisha Mongella nini maana ya ukuu wa mkoa.

ukiingia Mwanza jijini katikati, mambo ni hovyo na shaghala bagala kabisa...

Ukiachilia uchafu wa taka taka zilizozagaa ovyo, pia kuna ishu ya wachuuzi na wafanya biashara ndogondogo za kupanga barabarani...

Ukiingia ktk barabara za Mwanza kwa sasa, haieleweki magari yatembelee wapi, waenda kwa miguu watembelee wapi na baiskeli na pikipiki zitembelee wapi...

Ni kwamba, hawa wafanya biashara barabara zote zimekuwa ni maeneo ya biashara mpaka inakera kwa kweli...

Imefika mahali hata polisi wa usalama barabarani wanashindwa kufanya kazi yao ya usalama Wa vyombo vya moto, raia na mali zao kwa sababu ya muingiliano huu...

Kuna kila dalili na sababu kuwa, hili Luna kibali cha wanasiasa...

Sasa hii ni mbaya na hatari sana kama tunaweza kuingiza siasa ktk mambo hata yahusuyo usalama na maendeleo ya wananchi...

Kufanya mambo yetu ovyo hovyo bila utaratibu kamwe siyo ustaarabu hata kidogo bali ni ujinga na kichocheo cha umasikini zaidi...

IMG_20210203_172123_5.jpg
IMG_20210203_171854_0.jpg
IMG_20210203_171851_1.jpg
IMG_20210203_171840_9.jpg
IMG_20210203_171838_1.jpg
IMG_20210203_171838_1.jpg
 
Aisee Makonda anavyokumbukwa kazi ipo, matusi yote yale aliyokuwa anatupiwa!, iko siku na CCM itaondoka madarakani usikie bora hata CCM ingekuwepo!!
Makonda kilichomponza ilikua ni dharau zake na majivuno dhidi ya aliowazidi uwezo lakini kwa upande wa kazi alikua mchapakazi na mbunifu
 
Aisee Makonda anavyokumbukwa kazi ipo, matusi yote yale aliyokuwa anatupiwa!, iko siku na CCM itaondoka madarakani usikie bora hata CCM ingekuwepo!!
Inawezekana mleta uzi ni ndugu wa Makonda wanatoka wote koromitje
 
makonda kilichomponza ilikua ni dharau zake na majivuno dhidi ya aliowazidi uwezo lakini kwa upande wavkazi alikua mchapakazi na mbunifu
Toa mfano mmojawapo wa kazi alizofanikiwa akiwa hapa dsm huyo Makonda wako
 
John Mongela alipewa fadhila na yeye ale Kwasababu ya jina la mama yake, Getrude Mongela.

Suala la kufanya kazi ni option. Atakuwa anasaidia saidia tu ili aonekane na yeye yupo lakini siyo kipaumbele.
Getrude Mongela alipigania uhuru wa nchi hii lazima tumuenzi...
 
Nakumbuka kipindi yupo Kagera aliboronga sana,alikuza migogoro anaendekeza makundi hadi manispaa ya Bukoba ikadumaa kimaendeleo
Hao WATOTO wa vigogo wanapeana ajira tu ili wasikae Jobless.

Ingekuwa ni kufanya kazi, wangeweka mtu anayefanya KAZI na siyo kulipa fadhila au kuwapa rushwa watu watulie.
 
Back
Top Bottom