Mkuu wa Mkoa wa Manyara Aingilia eneo la WMA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mkuu wa Mkoa wa Manyara Aingilia eneo la WMA

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Wambugani, Jan 14, 2009.

 1. Wambugani

  Wambugani JF-Expert Member

  #1
  Jan 14, 2009
  Joined: Dec 8, 2007
  Messages: 1,755
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 145
  Mkuu wa Mkoa wa Manyara Henry Daffa Shekifu ameitoa eneo la Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori Burunge (JUHIBU) kwa "Wanakaya" (Dhana Investment) kama wawekezaji pasipo kufuata taratibu za kutengewa maeneo kama ilivyo katika Kanuni za WMAs.

  Wanakaya walipopelekwa mahakamani na JUHIBU, Bwana Shekifu aliamuru kesi hiyo itolewe Mahakamani mara moja na Wanakaya waendelee kujenga Campsite kama walivyoanza.

  Jambo la Mkuu wa Mkoa kutoa amri ya wawekezaji kuingilia maeneo ya Hifadhi ya Jamii ni kukiuka Sheria ya nchi. Hii ikifumbiwa jicho litaleta 'precedent' mbaya katika utaratibu mzima wa Sera wa Wanyamapori ua jamii kunufaika na matunda ya kulinda na kuhifadhi maeneo yaliyo karibu na Ardhi Tengefu.

  Ekadu mosie Shekifu.
   
 2. Kaizer

  Kaizer JF-Expert Member

  #2
  Jan 14, 2009
  Joined: Sep 16, 2008
  Messages: 24,647
  Likes Received: 1,475
  Trophy Points: 280


  Mkuu hii habari ni nzito,, unaweza kutupa hard facts zaidi? manake nadhani enzi za wakuu kutumia madaraka vibaya zimepitwa na wakati, walau kuna guarantee ya kwamba watafikishwa mahakamani siku ya siku kama kina mramba,, sasa anapata wapi nguvu ya kuondoa kesi mahakamai? au hao jamaa wa JUHIBU walirubuniwa wafute kesi? na kama sivyo, si wakate rufaa?

  I mean hizi sera za kuwasaidia wananchi baada ya muda mrefu wa wao kukosa fursa hii, kisha anakuja mtu kuwasabottage namna hii?
   
 3. R

  Riane Member

  #3
  Jan 15, 2009
  Joined: Jan 6, 2009
  Messages: 9
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Pia kuna fununu kuwa huyu mkuu wa mkoa Shekifu ana mpango wa kuuza na kukodisha mashamba ya barley and wheat huko Manyara kwa wawekezaji feki.

  Mashamba haya ya barley/wheat yanaweza kuendelezwa na kutimiza matumizi ya TBL wakipata wawekezaji kwa njia sahihi siyo za maamuzi yake tuu. TBL sasa hivi wanatumia fedha za kigeni kuagiza barley toka nje ya nchi (SA).
   
 4. M

  Mfumwa JF-Expert Member

  #4
  Jan 15, 2009
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 1,456
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Yani mtu anafanya maamuzi kwa maslahi madogo sana anayopata. Hakumbuki wajukuu zake watakuja kuumia na hayo maamuzi. Yani vitu kibao watu wanavunja sheria, na hizi sheria ilikuwa kwa kulinda rasilimali zetu. Kuna sheria huruhusiwi jenga umbali fulani katika fukwe zetu, iwe Bahari ama Maziwa, lakini majumba ndio yanaporomoshwa huko na vigogo.

  Watu wanajenga katika maeneo wazi (open spaces) yaliyotengwa kwa michezo, mapumziko, mikutano nk, hakuna anayefuatilia. Danie Ole Njolay alipokuwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, watu walishangaa, kumbe kuna vichochoro/mitaa kibao watu waliiziba na kufanya maduka, nyumba za kuishi ama maghala. Alipofika Mwanza akaomba ramani ya jiji, mitaa na vichochoro vyote hivyo watu wakavunjiwa vitu walivyojenga, zikapatikana njia.
   
 5. Wambugani

  Wambugani JF-Expert Member

  #5
  Jan 15, 2009
  Joined: Dec 8, 2007
  Messages: 1,755
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 145
  Mgosi Shekifu alimwambia Afisa Maliasili wa Wilaya aondoe kesi Mahakamani ili
  wagosi wenzake (Dhana Investment Ltd) waendelee kujenga pale Kijiji cha Minjingu eneo karibu na Hifadhi ya Tarangire.

  Huyu Mgosi yupo kwa masilahi yake binfasi sio kwa maendeleo endelevu ya jamii.

  __________________________________
  Tiambize Zumbu mwe inu nyika!
   
 6. Kaizer

  Kaizer JF-Expert Member

  #6
  Jan 15, 2009
  Joined: Sep 16, 2008
  Messages: 24,647
  Likes Received: 1,475
  Trophy Points: 280
  Hoja hapa ni kwamba hiyo CBO ya hiyo WMA wanayo haki kwenda mahakamani, huyo afisa mali asili kama ameondoa kesi wao waende mbele kwa sababu wana haki zote za kisheria....huyo sio wa kumwachia hivi hivi la sivyo itaset a bad precedent kwenye haya mambo!
   
 7. Majita

  Majita JF-Expert Member

  #7
  Jan 15, 2009
  Joined: Jan 13, 2008
  Messages: 606
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 45
  Jamani hivi Anatory Tarimo alishaondoka hapo Manyara????Yuko wapi sasa kwa yule ajuae pls
   
 8. Ben Saanane

  Ben Saanane Verified User

  #8
  Jan 15, 2009
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 14,603
  Likes Received: 3,692
  Trophy Points: 280
  Nadhani Yupo Singida
   
 9. Majita

  Majita JF-Expert Member

  #9
  Jan 16, 2009
  Joined: Jan 13, 2008
  Messages: 606
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 45
  Alipotoka Singida ndo akaenda manyara.Karudishwa Singida tena au kastaafu na kwenda kuishi Singida??
   
 10. Wambugani

  Wambugani JF-Expert Member

  #10
  Jan 16, 2009
  Joined: Dec 8, 2007
  Messages: 1,755
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 145
  Kanali Mstaafu Anatoli Tarimo alikuwa RC wa kwanza Mkoa wa Manyara ametupwa Mkoa wa Lindi. Sijui ni adhabu. Heri Shekifu anayekifu angerudishwa huko Lindi.
   
Loading...