Mkuu wa kazi anapokuwa mwanamke kwanini aitwe 'mama'?

Ukiona mtu anahoji vitu vya namna hii ujue huyo mtu ana mojawapo kati ya matatizo yafuatayo:
-Ana mgogoro wa kiutumishi na mwajiri.

-Ana inferiority complex ambayo inamla sana moyoni.

-Ana dharau ya asili ambapo akili zake zinamtuma kubeza kila kitu.

-Ni jamii ya maMachinoo wa maofisini ambao Utawala anajua, Uhasibu anaelewa yeye, Uzalishaji na operational duties anajua yeye.

Watu wa calibre hii hata efficiency yao kazini ni Poor na ni walalamishi.

Aidha watu wa jinsi hii ni propergators wa Grapevine na wazalishaji wa fitna sehemu za kazi.
 
mbona kitu kitu cha kawaida na si lazima tena, si ofisini tu hata nje ya ofisi ukikutana na mwanamke mtu mzima hata kama si kiongozi unaweza kumuita mama si lazima awe wa kwako wa kukuzaa.
ila mahali pa kazi kuitana majina haya pia kunaweza kukusababisha ukashindwa kufanya mambo fulanifulani kwa sababu umeshaweka uheshima wa mama.
 
Mwisho atakuja kuutufwata mbona mtume pdidy mkewe anaitwa appostle pdidy...
Sababu sadaka tunahesabu pamoja natumain huko utofika
 
Kifupi sio kama unavyonidhania. Mie nimehoji kwa nini aitwe hivyo, kama unaona sawa eleza na toa sababu usimuhukumu mtu moja kwa moja

Ukiona mtu anahoji vitu vya namna hii ujue huyo mtu ana mojawapo kati ya matatizo yafuatayo:
-Ana mgogoro wa kiutumishi na mwajiri.

-Ana inferiority complex ambayo inamla sana moyoni.

-Ana dharau ya asili ambapo akili zake zinamtuma kubeza kila kitu.

-Ni jamii ya maMachinoo wa maofisini ambao Utawala anajua, Uhasibu anaelewa yeye, Uzalishaji na operational duties anajua yeye.

Watu wa calibre hii hata efficiency yao kazini ni Poor na ni walalamishi.

Aidha watu wa jinsi hii ni propergators wa Grapevine na wazalishaji wa fitna sehemu za kazi.
 
Katika kushughurikia maswala yangu katika ofisi za umma na katika mabenki nimebaini kuwa baadhi ya wafanyakazi nilio wasikia wanatumia neno "MAMA" wakimaanisha mkuu wao wa kazi, awali ilinipa shida kuelewa ana maana gani katika ofisi fulani lakini baada ya kwenda ofisi nyingine nikakutana tena na msemo huo, nimefika mapokezi nikakutana na mfanyakazi wa kiume nakueleza shida yangu, naye akamuuliza mfanyakazi mwenzake wa kike eti "mama" yupo kuna mteja hapa anashida naye. sasa nikaanza kujiuliza kulikoni mbona mkuu wa ofisi akiwa mwanamme sijasikia akiitwa "BABA" badala yake wanatumia zaidi neno Boss au MKUU. Binafsi imenikera sana tena sana kwani kwangu mie mama ni mama tu na wala mtu mwingine hawezi vaa wasifu huo tena kwa mtu asiye hata na udamu na mama yangu. Au ndio ni aina fulani ya Rushwa ya unyenyekevu maofsini ili mtu kunufaika malupulupu kwa haraka. Nawaulizeni nanyi wanaJF kuitwa "mama" kwa kiongozi mwanamke maofsini je ni sawa kwenu?

hiyo ni title tu labda kutokana na wanavyoonyesha upendo wa mama kwa wa chini yao! Kwani hao wakuu wa kazi uliambia ni 'mama' hata kwako wewe?
 
Back
Top Bottom