Mkuu Allen Kilewela unaweza kutujuza uwekezaji uliokemewa na Waziri Mkuu kwenye shule za Gangilonga na Wilolesi mjini Iringa?

Pamoja na watu wengi kufananisha hili swala la Gangilongag na la maeneo ya kwao, lakini hili lina utofauti sana.

Kwanza shule ya Msingi Gangilonga zamani ilikuwa inamilikiwa na Kanisa la Kilutheri kabla ya kutaifishwa na serikali.

Eneo linalozungumziwa haliko karibu na shule na kwa muda mrefu halikuwa sehemu ya shule wala sehemu ya Chuo cha Ualimu Klerruu bali lilikuwa linamilikiwa na Halmashauri ya Manispaa ya Iringa.

Hilo eneo lilishawahi kutumika kama Karakana ya Kampuni moja ya kichina iliyokuwa inajenga Barabara. Na baadae likaja kutumika tena na Kampuni nyingine ya ujenzi.

Kwa zaidi ya miaka kumi lilikuwa halitumiki na shule ya Gangilonga wala Chuo cha Klerruu. Wengine ambao tuko hapo zaidi ya miaka 30 tunajua kwamba eneo hilo halijawahi kutumika na shule ya Gangilonga zaidi ya kulimwa na Mwalimu mmoja aliyekuwa anaitwa Mwalimu Hassan.

Inawezekana Halmashauri ililiona kama ni eneo linaloweza kugeuzwa kuwa uwekezaji bila ya kuleta usumbufu. Lilipo na lilivyo kwa namna yoyote ile haliwezi kuwa ni usumbufu kwa wanafunzi wa shule ya Gangilonga wala Wakazi wanaokaa kwenye kota za waalimu wa Chuo cha Kleruu.

Lakini labda hoja ya msingi ingekuwa Messy alilipataje hilo eneo?
 
Nimekusoma mwanzo mwisho

Unge declare interest kwanza ili usomeke vizuri mkuu.
 
Sina maslahi yoyote yale na suala hili.

Watu wanatakiwa kutumia akili zao kuhoji mambo ya msingi kwenye jambo hili. Kata yetu ya Gangilonga ni kama Kata za Msasani, Magogoni, Oyster Bay, kwa kule Dar es salaam kwa ivo ni eneo muhimu.

Hii kata ndiko yaliko makao Makuu ya Mkoa, Makazi ya Mkuu wa wilaya na mkoa, Ofisi ya Manispaa, Makao Makuu na Makazi ya Askofu wa Kanisa Katoliki, Anglikana, Orthodox na Lutheran, Makao Makuu ya Manispaa ya Iringa, Mahakama Kuu, Hospitali ya Mkoa, Ofisi ya RPC na makazi yake, na Ofisi nyinginezo kadhaa.

Tatizo watu badala ya kujadili hilo eneo lilitolewaje hadi ukumbi ukajengwa wanajadili tamko kwamba jengo livunjwe!!
 
Asante pureView Zeiss maana watu wa Lumumba mambo mengi badala ya kuyafanya kwa Weledi wao hutumia mitulinga.

johnthebaptist Gangilonga kuna ukumbi unajengwa na Dada yangu Messy Sanga (Mrs. Mshana). Juzi nilipita pale nikasema inawezekana hii ziara ikaleta mambo, na kweli TAMKO limetoka.

Shule ya msingi Wilolesi kuna utata kidogo. Kanisa katoliki kitambo sana lilijenga shule (Saint Dominic) lakini jirani yake ndio kuna shule ya umma ya Wilolesi. Eneo hilo ni "Prime Area".

Sasa kiwanja kilicho pembeni na Saint Dominic ni kiwanja cha shule ya msingi Wilolesi. Kwanza watu wa chuo Kikuu cha Ruaha (RUCU) walilitaka kwa ajili ya kujengea viwanja vya michezo, wakakataliwa.

Na inadaiwa pia (Hili niliambiwa na Mwenyekiti wa mtaa iliko shule ya Msingi wilolesi) Kampuni ya Asas nayo iliwahi kuomba kufanya uwekezaji kwenye eneo hilo la shule nao pia wakakataliwa.

Lakini kati ya eneo la RUCU na RETCO kuna jengo lililokuwa iwe hoteli ya kitalii, nayo ikakataliwa ingawa ilishaanza kujengwa. Ninachokiona mimi ni vita ya kupata maeneo hayo kirahisi.

Hii vita ina zaidi ya miaka 15. Tusubiri tuone.

Poleni sana...

Cc: mahondaw
 
Poleni sana...

Cc: mahondaw
Mimi ninachojiuliza kwa nini anayejenga ndiye alaumiwe wakati yeye aliomba eneo na akapewa. Messy kasoma Gangilonga na ameishi hilo eneo maisha yake yote isipokuwa alipokuwa chuoni, hivyo analijua vizuri sana hilo eneo.

Ninachotaka kujua waliompa hilo eneo hawakujua kama liko karibu na shule, kama walijua ni kwa nini walitoa lijengwe ukumbi? Jee waliokuwa wanatoa vibali vya ujenzi hawaijui shule ya Msingi Gangilonga?

Jee Messy atarudishiwa gharama zake ama ndio atadhulumiwa ili wengine wapone? Maana yeye hakuvunja sheria bali waliompa yeye hilo eneo ajenge.

Kuna eneo la wazi jingine hao hao Manispaa walilitoa limejengwa nyumba za kuishi na nyumba ya Ibada. Leo ikitokea hao watu wa hilo eneo wakiambiwa wabomoe wao ndio wanaokuwa watu wa kulaumiwa?

Gangilonga kuna maeneo mengi sana ya wazi hayalindwi wala kuendelezwa na ndipo mwisho wa siku hutolewa kwa watu wengine kujengwa nyumba za kuishi ama majengo mengine.

Tatizo ni mfumo wa kusimamia matumizi ya Ardhi.
 
Mimi ninachojiuliza kwa nini anayejenga ndiye alaumiwe wakati yeye aliomba eneo na akapewa. Messy kasoma Gangilonga na ameishi hilo eneo maisha yake yote isipokuwa alipokuwa chuoni, hivyo analijua vizuri sana hilo eneo.

Ninachotaka kujua waliompa hilo eneo hawakujua kama liko karibu na shule, kama walijua ni kwa nini walitoa lijengwe ukumbi? Jee waliokuwa wanatoa vibali vya ujenzi hawaijui shule ya Msingi Gangilonga?

Jee Messy atarudishiwa gharama zake ama ndio atadhulumiwa ili wengine wapone? Maana yeye hakuvunja sheria bali waliompa yeye hilo eneo ajenge.

Kuna eneo la wazi jingine hao hao Manispaa walilitoa limejengwa nyumba za kuishi na nyumba ya Ibada. Leo ikitokea hao watu wa hilo eneo wakiambiwa wabomoe wao ndio wanaokuwa watu wa kulaumiwa?

Gangilonga kuna maeneo mengi sana ya wazi hayalindwi wala kuendelezwa na ndipo mwisho wa siku hutolewa kwa watu wengine kujengwa nyumba ana majengo mengine.

Tatizo ni mfumo wa kusimamia matumizi ya Ardhi.

Na kwa nini Messy hakufanya utafiti wake na kujiridhisha kabla ya kuanza harakati za uwekezaji...

Unless kama rushwa ilitembea...

Kwenye mambo ya Ardhi inaruhusiwa kuona eneo na kuulizia kama unaweza kuwekeza. Kwenye hilo eneo mbona kulikuwa na Karakana na kambi ya ujenzi wa Barabara?

Hoja yangu inawezekana Manispaa waliona ni sawa ukumbi ujengwe, hoja labda iwe ya kitaalamu na siyo kusema kama kuna rushwa ilitembea.
 
Diwan wa kata ya gangilonga so ndio huyo adi uko Wilolesi?
1569747443993.png

Leonard Mgina diwani ya Kata ya Gangilonga.

Jamaa amekuwa Diwani kwa kuchaguliwa kwa kura tisa na wana CCM wenzake.

Udiwani wake ulitokana na Mgombea wa CHADEMA kuporwa fomu na pia Afisa Mtendaji wa Kata ambaye ni Kada kindakindaki wa CCM kukataa kutoa fumo nyingine kwa CHADEMA na CHADEMA walipokuja na fumo nyingine zilizokwisha jazwa alizikataa kwa hoja kwamba hakuzitoa yeye.
 
Asante pureView Zeiss maana watu wa Lumumba mambo mengi badala ya kuyafanya kwa Weledi wao hutumia mitulinga.

johnthebaptist Gangilonga kuna ukumbi unajengwa na Dada yangu Messy Sanga (Mrs. Mshana). Juzi nilipita pale nikasema inawezekana hii ziara ikaleta mambo, na kweli TAMKO limetoka.

Shule ya msingi Wilolesi kuna utata kidogo. Kanisa katoliki kitambo sana lilijenga shule (Saint Dominic) lakini jirani yake ndio kuna shule ya umma ya Wilolesi. Eneo hilo ni "Prime Area".

Sasa kiwanja kilicho pembeni na Saint Dominic ni kiwanja cha shule ya msingi Wilolesi. Kwanza watu wa chuo Kikuu cha Ruaha (RUCU) walilitaka kwa ajili ya kujengea viwanja vya michezo, wakakataliwa.

Na inadaiwa pia (Hili niliambiwa na Mwenyekiti wa mtaa iliko shule ya Msingi wilolesi) Kampuni ya Asas nayo iliwahi kuomba kufanya uwekezaji kwenye eneo hilo la shule nao pia wakakataliwa.

Lakini kati ya eneo la RUCU na RETCO kuna jengo lililokuwa iwe hoteli ya kitalii, nayo ikakataliwa ingawa ilishaanza kujengwa. Ninachokiona mimi ni vita ya kupata maeneo hayo kirahisi.

Hii vita ina zaidi ya miaka 15. Tusubiri tuone.
Sanga kaolewa na mshana? Mkinga na mpare wanaweza kutamani kulima bustani hata eneo la jeshi.
 
Katika hili walifuata taratibu zote. Wengeweza wangeifungulia mashtaka Manisapaa ya Iringa kwa kuwatia hasara!!
Mkuu haya ni mambo ya kawaida, usipanik! Mbona nyongeza za mishahara za watumishi (annual increment) na fedha zao za kupanda madaraja ambazo zipo kisheria, zinatumika kujenga standard gauge na wote tunashangilia?
 
Ccm bhana kumbe ndo maana ilikua inafanya biashara ya kuwanunua madiwani ili waanze kugeana viwanja vya shule kishikaji.
 
Sina maslahi yoyote yale na suala hili.

Watu wanatakiwa kutumia akili zao kuhoji mambo ya msingi kwenye jambo hili. Kata yetu ya Gangilonga ni kama Kata za Msasani, Magogoni, Oyster Bay, kwa kule Dar es salaam kwa ivo ni eneo muhimu.

Hii kata ndiko yaliko makao Makuu ya Mkoa, Makazi ya Mkuu wa wilaya na mkoa, Ofisi ya Manispaa, Makao Makuu na Makazi ya Askofu wa Kanisa Katoliki, Anglikana, Orthodox na Lutheran, Makao Makuu ya Manispaa ya Iringa, Mahakama Kuu, Hospitali ya Mkoa, Ofisi ya RPC na makazi yake, na Ofisi nyinginezo kadhaa.

Tatizo watu badala ya kujadili hilo eneo lilitolewaje hadi ukumbi ukajengwa wanajadili tamko kwamba jengo livunjwe!!
[/QUOTE
Gangi longa kweli prime areas naijua vizuri hakina Comfort wamejenga pale kwa juu, hakina makosa nimetoka huko 2001

Lakini dada yako ungemshauri akajenge don bosco, ipogoro, mkimbizi au njia ya kwenda idodi au angevua watu frelimo au ilala mbona ni sehemu nzuri mkuu. Msalimie Kite
 
Katazo la serikali ni la msingi sana kuhusu biashara karibu kuzunguka shule:-
* Kumbi za starehe
* vilabu vya pombe
* Nyumba za kulala wageni
* Maduka ya vitu mbalimbali yanayosababisha kelele
* Nk.

Wanafunzi hupata shida sana kwa shule zenye uwekezaji wa namna hiyo karibu na shule.

Ila viongozi waliopewa dhamana ndo wanaoleta shida yote hii INA sasa wameshamwingiza hasara mwekezaji
Bila sababu, kwa sababu wao ndo walitakiwa wamkatalie kuwa hilo eneo haliruhusiwi ni kwa ajili ya jambo fulani..

Labda Halmashauri itafanya utaratibu wa kumfidia huyo mwekezaji.
 
Back
Top Bottom