Bila shaka wengi wetu hatujui mazingira hasa ya nchi yetu na watu wetu. Ni watanzania hawa hawa, ambao wakipelekewa vyandarua wao wanavulia samaki. Ni watanzania hawa hawa wanao vyua samaki kwa kutumia sumu na mabomu huku wakijua inathiri siyo tu mazingira bali hata afya zao na watoto wao. Ni watanzania hawa hawa ambao wameua mashirika ya umma. ni watanzania hao hao ambao wameua vyama vya ushirika, na Ni watanzania hawa hawa ambao wamekaa na ardhi yooooote hii yenye rutuba siku zote bila kuanzisha kilimo cha kisasa. Niwatanzania hawa hawa ambao wanapewa elfu 10 na kuachia vyocha ya pembejeo. Ni watanzania hawa hawa ambao wanauza shahada ya kupigia kurakwa Tsh 5,000
Mkuu you are missing the plot...!!!, hivi ni watanzania, yaani wakulima ndio waliua vyama vya ushirika, Mkuu ni kwamba hata hiki kilimo kikubwa ni kwamba corporation chache ndio itakifanya ila tofauti ni kwamba watachukua profit kubwa na mara nyingi kwenda kufanya processing huko kwao sasa ni kipi kinashindikana kuunda board / ushirika ambao utakuwepo kwa niaba ya wananchi na kila mwananchi anajua kwamba hili ni shamba letu hivyo basi hii venture itakuwa sio profit based bali service based yaani faida yote itarudishwa kwenye jamii kuendeleza jamii husika na kutoa misaada.., kumbuka pia mpaka sasa hatujashindwa kujilisha ni hao hao watanzania unaosema wenye fikra mbovu ndio wameweza kutulisha tena kwa jembe la mkono tatizo serikali imeshindwa kuleta miundo mbinu ya kutosha hadi mazao yanaozea kwenye mashamba
Hawa ndo watanzinia ambao mnataka serikali iwasaidie ili wawe na kilimo cha kisasa. Watanzania wengi walioko vijijini siyo kwamba wanashindwa kulima kwa kisasa wakiamua. Tatizo la watu wetu ni fikra na siyo mitaji wala uwezeshwaji. Wanacho hitaji ni Elimu.
Mwenye kazi ya kutoa elimu ni nani...?
Alafu narudia tena mambo ya kila mtu kufanya issue kivyake hayafai ni kwamba maeneo makubwa yakichukuliwa na kulimwa kisasa na sio serikali kuwezesha mtu mmoja mmoja bali kama wakitengeneza vyama vya ushirika na kuvipa uwezo na pesa ya kununua machinery za kisasa zinaweza kuzalisha surplus ambao inaweza kuuzwa hata nje kwa faida ya community nzima na nchi (tofauti na wawekezaje watachukua a large chunk of profit na mkulima sidhani kama ataweza ku-compete kwa mazao na hawa watu)
Na serikali tangu uhuru imekua ikitoe elimu ya kilimo cha kisasa, majarida yameandikwa, vipindi vya radio kila wiki vipo, hadi kitengo maalumu cha kutoa elimu ya kilimo cha kisasa kilianzishwa na kimefanya kazi nzuri. Lakini tatizo ni fikra, watu hawabadiliki. Wazee wakivuna mazao hawaonekani nyumbani hadi fedha ziishe, badala ya kuendeleza kilimo wengine wanaoa wake wa 3 n.k
Mkuu unatangaza kilimo cha kisasa alafu unatoa power tillers.., huwezi kumlaumu mkulima mdogo wakati ameweza kutulisha mpaka leo kwa kutumia jembe la mkono na kupinda mgongo wake mpaka amepata kilema cha maisha, unataka fikra zibadilike vipi waende benki wakaibe ili wanunua ma-trekta.., mkuu kama nilivyosema inabidi kutengeneza vyama vya ushirika na ku-inject capital kubwa ili vilime kwa manufaa ya jamii yote husika na kupeleka viwanda vya kusindika huko huko bush ili kuongeza ajira huko na kuongeza value na kuhakikisha kuna usafiri wa kutoka huko mpaka sokoni
Ninachosema njia zote mbili ni muhimu katika kuendeleza kilimo..yani kuleta wawekezaji wakubwa katika kilimo na kuwezesha wakulima wadogo wadogo. Na hili linafanyika. Pembejeo za ruzuku zinatolewa, wataalamu wa kilimo (maafisa ugani) sasa wameajiriwa kwa kila kata na kila wilaya imenunua matreka kwa ajili ya kuwakopesha wakulima wazawa. Kwa hiyo yote mawili yana nafasi yake.
Mkuu acha kujidanganya hata marekani na nchi zote kubwa hakuna nafasi ya mkulima mdogo wakija wakulima wakubwa its simple mathematics hawa wakulima wakubwa wanaweza wakatoa mazao at a lower cost na mwisho wa siku waka-offer at a lower price.., mkulima mdogo atakufa a natural death..., na kumbuka mimi sisemi tubaki na wakulima wadogo bali nasema hao wakulima wakubwa (wawekezaji) viwe vyama vya ushirika kwa manufaa ya wananchi wote wenye ardhi yao kwa faida yao.., Nchi nyingi ni kwamba 10% ndio inalisha 90% sasa hiyo 10% badala ya kuwa foreigner kwanini isiwe vyama vya ushirika vinavyomilikiwa na vipo kwa faida ya wananchi wote..?
Vile vile hakuna mkulima mzawa ambaye amewahi kuomba ardhi ya kilimo akanyimwa. wengi wenu hapo Dar mna mashamba mkoa wa pwani na sehumu nyingine, je ni nani analima kila mwaka hata ekari 10 tu? Mnacho taka ni kushikiria ardhi bila kuitumia ili akitokea mwekezaji nyie mumuuzie.
Mkuu wachukue ardhi walime kwa kutumia nini..?, power tillers au waende msituni walime ambapo hakuna barabara nani atakaeleta mazao sokoni au waache ngedere ndio wayale..., Think Mkuu hiyo ardhi yote ingechukuliwa na vyama vya ushirika sidhani kama mgesema kwamba elimu, na afya bure haviwezekani na vile vile tungeacha kwenda kutembeza bakuli nje.., pia tungeweza kutoa welfare kwa wazee wetu na watu ambao hawana kazi na usitegemee hawa wawekezaji watakubali pesa zao zifanye kazi za charity
Mashamba makubwa yatatoa ajira, yataongeza export na kuongeza chakula. Moja ya sababu zilizofanya mikoa ya kasikazini kupiga hatua kubwa yamaendeleo ukilinganisha na mikoa mingine ni uwepo wa mashamba makubwa. Mashamba ya Ngano, mashamba ya miti na mahindi na maharage. Iringa pale shamba moja tu la miti la sao hill limefanya maisha ya watu wengi yaboreke. Tuache siasa tujaribu kuwa realistic. Tuache kusikiliza wanasiasa wanaotupotosha badala yake tutumie fikra zetu wenyewe.
I 100% support initiatives za mtoto wa mkulima.
Mkuu wewe ndio tumia fikra zako mwenyewe na acha hizi propaganda.., hizi ajira zinazoongezeka ni zipi za kubadilisha oils kwenye tractor..., mkuu acha kutafuta short cuts kwenye hizo export zikiongezeka Tanzania itapata % ngapi, hivi niambie ni nini ambacho anafanya huyo mwekezaji vyama vya ushirika vinashindwa na kubaki na 100% ya profits ? na ni nani amekwambia tunakosa chakula sasa hivi sababu hakuna wakulima wanaozalisha..? issue ni kwamba hakuna miundombinu (hata reli wameshaiua..) ya kuleta chakula sokoni mpaka mazao yanaozea mashambani..
Mkuu acha kabisa hizo porojo kama unataka ukweli kaangalia so called small farmers in UK na USA they are non existent na wengine inabidi wauze ardhi zao sababu they can't compete tena washukuru Mungu wengine huko wana welfare huko Bongo kila mtu atakufa kifo chake na umasikini, wakati kama ingekuwa ni vyama vya ushirika vingehakikisha kila mtu anapata gunia za mahindi hata kama hana pesa au ana pesa kidogo sababu mali ni ya kwao mali ya ushirika