Mkutano wa wawekezaji - Rukwa

hashycool

JF-Expert Member
Oct 2, 2010
6,555
2,829
Mkutano wa fursa za uwekezaji katika ukanda wa ziwa tanganyika live kutoka rukwa sasa TBC1....
Rais kikwete,waziri mkuu,mabalozi na wawekezaji...
 
Eng; Stellah manyanya..mkuu wa mkoani wa rukwa ndo anafungua mkutano kwa sasa......
 
Hata kufuga nyuki wnataka mwekezaji??
Wehu hawa!! kwani wananchi waliopo huko hawawezi kuwezeshwa wakafanya wenyewe??
 
mary nagu anaisifia mikoa hiyo kuunganishwa na reli???!!!!!! reli ipi?????
 
check bob pinda....ndo anaongea sasa na t-shirt lake kuuuuubwa la NMB...
NAONA KATAMBUA UWEPO WA KABWE NA ALFI......ANAMKARIBISHA RAIS!
 
Kikwete vipi?
Mbona anatumia Kiingereza badala ya kiswahili? Mkutano umeandaliwa kwa lugha ya kiswahili
 
Nafikri ni mkutano wa wakwapuaji huo wa rasilimali za Tanganyika
 
Marry nagu anasifia mikoa ya kigoma,rukwa kuwa imejiandaa na miundombinu na wako tayari kwa ajili ya wawekezaji...
hivi barabara za lami zishafika kule? umeme?
 
Kwenye mkutano wa wawekezaji unaorushwa live na tbc kn sharobaro kavaa suti ya dack blue kasimama anasema yeye ataongea kwa kingereza kwani kn wazungu wengi watu wasomi hm kwenye mkutano wanajidai hawajui kiswahili, eti anasema akimaliza kuongea kwa kingereza atatafsiri kwa kishwahili, hii ni sawa jamani? WATU WAPEWE ARDHI YETU, BD NA LUGHA YT NAYO IDHARAULIWE MBELE YAO? kwanini asiongee kiswahili kwanza kingereza kifuate?
 
MH,kikwete antoa hotuba yake kwenye mkutano wa kupata fursa za uwekezaji katika mikoa ya kigoma ,Rukwa na katavi lakini kwa kujua kuwa hii ni nafasi ya kuwa fanya watanzania wengi wa maeneo husika kujua nafasi yao kwenye uwekezaji unaotakiwa kufanyika kwenye maeneo yao je kutumia lugha ya kiingereza eti sababuwawekezaji wengi ni wageni na mabalozi hawatendei haki watanzania wengi jifunze mh jk
 
Kikwete vipi?
Mbona anatumia Kiingereza badala ya kiswahili? Mkutano umeandaliwa kwa lugha ya kiswahili

Kuna dalili ya very poor planning kwenye huu mkutano. Sina hakika kama wote wanajua 'audience' wake ni nani na hii ndio maana wazungumzaji wengine wanaongea Kiswahili, lakini rais anaongea kiingereza. Are they talking to the same people?

Pili, tabia ya 'ku-import' solution ni kilele cha uvivu wa kufikiri. Kwa kuanzia tu, hizi hela zilizotumika kufanikisha hili kongamano zingetosha kununua matreka mangapi na zana zingine za kilimo? Hivi wananchi hii mikoa ya ukanda wa Lake Tanganyika wanahitaji wawekezaji au wanahitahi uwezeshaji? Na kwa historia ya nchi uwekezaji wa aina gani umekuwa na manufaa? Wawekezaji kwenye madini wanatumaliza (hata kutoa uhai) sasa tunataka wachukue ardhi! Ni wapi na lini wananchi waliwezeshwa lakini wakashindwa kulima?
 
kikwete: private sector starts from the hand hoe farmer....
anamponda nyerere hapa.....eti nyerere alishawahi kutoa order ya maduka yote ya binafsi kufungwa....
 
kikwete: world class utility companies failed in TZ because they didnt bring the world class managers in TZ....
 
kikwete: we've made reforms...we are selling shares to the public...kama NMB shares.
Tanzanians should be part of investments ni hatari kutoa kila kitu kwa wawekezaji wa nje...(unafki)
 
Marry nagu anasifia mikoa ya kigoma,rukwa kuwa imejiandaa na miundombinu na wako tayari kwa ajili ya wawekezaji...
hivi barabara za lami zishafika kule? umeme?

ukitokea dar, lami ipo mpaka nzega. kutoka nzega kwenda tabora hakuna lami, ukifika tabora mjini kuna lami pia kutoka tabora kwenda urambo mpaka kigoma hakuna lami.
 
Back
Top Bottom