Dkt. Pindi Chana: Serikali inataka kila Mwananchi awe na amani na furaha sio kuwa na hofu

Nyakijooga

Senior Member
Dec 9, 2018
123
202
Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Pindi Chana amesema Serikali inaunga mkono kauli wadau kuwa utetezi wa haki za binadamu sio uhalifu (Human rights not a crime), ameeleza kwamba kuwa Rais Samia anachukua hatua mbalimbali kwa ajili ya kulinda haki za binadamu nchini.

"Sisi wenyewe tunataka kila mwananchi anayefanya kazi awe na amani awe na furaha sio unafanya kazi una wasiwasi unafanya kazi una hofu hapana"

Ametoa kauli hiyo leo October 19, 2023 akihutubia katika mkutano wa tafakari ya miaka 25 ya tamko la Umoja wa Mataifa kuhusu Watetezi wa Haki za Binadamu na uthibitisho wa sera ya mfano ya Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania uliofanyika jijini Arusha akiwa mgeni rasimi.

Waziri huyo amesema katika jitihada ambazo zimefanywa na Rais Samia ni pamoja na kuanzisha 'Mama Samia Legal Aid Campaign' ambayo imeanzishwa kwa malengo mbalimbali ikiwemo kutoa huduma ya msaada wa kisheria, ambapo amesema kuwa tayari baadhi ya mikoa zimefikiwa.

“Mheshimiwa Rais wetu amefungua huduma ya Msaada wa Kisheria katika Mikoa yote ya Tanzania, ameiagiza Wizara na Idara zetu kushirikiana na wananchi wote wa Tanzania kusikiliza mahitaji yao ya msaada wa kisheria kama chachu ya kupata haki zao, tumeanza kusonga mbele katika baadhi ya maeneo. mikoani na tunatamani kusafiri katika mikoa yote ili kuhakikisha kuwa Watanzania wanafurahia haki zao".

Aidh amesema kuwa jitihada nyingine ni kuwateua majaji wengi kwa siku za hivi karibuni kwenye ngazi za Mahakama Kuu na Mahakama ya Rufani akiwa anazingatia usawa wa kijinsia, ambapo amesema kuwa uteuzi huo ni ishara kuwa anataka haki zitendeke.

"Dk.Samia Suluhu Hassan ameongeza juhudi katika kuajiri majaji nchini Tanzania, cha kufurahisha zaidi anajali sana usawa wa kijinsia kwa kuhakikisha kuwa kunakuwa na viongozi wa kutosha wa Wanawake katika Bunge, Wizara na Mahakama". amesema Waziri huyo.

Aidha kwa upande wa Watetezi wa Haki za Binadamu Wakili Onesmo Olengurumwa amepongeza jitihada mbalimbali ambazo zimekuwa zikifanywa na Serikali ya awamu ya sita hususani mchakato wa kutaka kuirejesha Tanzania kwenye Mpango wa Uendeshaji wa Shughuli za Serikali kwa Uwazi (Open Government Partnership-OGP) pamoja na Serikali kuwa mwenyeji kwenye mkutano wa 77 wa Tume ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu (ACHPR).

Wadau mbalimbali wa kutetea haki za binadamu kutoka kwenye Asasi kiraia tofautiwameshiriki mkutano huo na kuchangia mjadala kwa kuibua baadhi ya masuala na kuyatolea mapendekezo.
 
Back
Top Bottom