Hali ya haki za binadamu Afrika hairidhishi

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,502
9,282
Mkutano wa 77 wa haki za binadamu unafanyika mjini Arusha Tanzania, ambao unataja mapinduzi ya kijeshi na vita katika baadhi ya mataifa ya Afrika kumesababisha ukiukwaji wa haki za binadamu, kando na mambo mengine

Mkutano huo unaotarajiwa kukamilika tarehe tisa ya mwezi huu wa Oktoba unaowakutanisha wadau wa haki za binadamu kutoka nchi mbali mbali za Afrika umezitupia lawama baadhi ya serikali za Afrika pamoja na jumuiya za kikanda, kwa kushindwa kuwajibika kuwalinda raia dhidi ya uvunjifu wa haki za binadamu.

Baadhi ya matukio yaliyobainishwa na mkutano huo ambayo yanaashiria nchi kukwepa uwajibikajiwa kulinda haki za binadamu, ni pamoja na nchi kujitoa katika itifaki ya mahakama ya Afrika ya haki za binadamu, inayoruhusu raia na mashirika binafsi kuwaruhusu watu wake kufungua kesi zinazohusu haki za binadamu.

Tanzania ikiwa ni miongoni mwa nchi nne zilizojitoa katika mkataba huo, imeendelea kushikilia msimamo kuwa inafanya vizuri katika ulinzi wa haki za binadamu.

Matukio mengine ya uvunjifu wa haki za binadamu yaliyotajwa na mkutano huo ni pamoja na migogoro ya ardhi na makazi baina ya serikali na wananchi kama vile mgogoro uliopo kati ya serikali ya Tanzania na jamii ya wafugaji ya Maasai, mapinduzi ya kijeshi yaliyozikumba baadhi ya nchi za Afrika hivi karibuni, pamoja na hali ya kiusalama ya eneo la mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Awali akitoa hotuba kwa niaba ya Rais wa Mahakama ya Afrika ya haki za binadamu na watu msajili wa Mahakama hiyo Dr. Robert Enno alibainisha kuwa serikali za Afrika bado zinasua sua katika ulinzi wa haki za binadamu.

Aidha alihoji juu ya nchi wanachama kuwazuia raia wake na mashirika binafsi kufungua kesi dhidi ya uvunjifu wa haki za binadamu.

"Tunawezaje kusema tunalinda haki za binadamu wakati maamuzi ya Mahakam hii hayatekelezwi nan chi wanachama?” Alihoji Dr. Enno.

Japo kimekuwa ni kilio cha muda mrefu, lakini washiriki wa mkutano huo wameendelea kuzikosoa baadhi ya serikali za nchi za Afrika kwa namna zinavyoshughulikia ulinzi wa haki za binadamu.

Kikao hiki cha kila mwaka kimewajumuisha wadau wa haki za binadamu wapatao 1000 kutoka serikali za nchi mbali mbali za Afrika pamoja na jumuiya ya kikanda na kimataifa.


DW
 
Aya maswala wameyaleta ngozi nyeupe kwa maslai yao ili wapate tu kazi yakuwaingizia kipato kaa wanaweza kuchukua maamuzi mtu kaa Mseveni wanamuona nawanajua kabisa uhuni wake aufanyao
 
Back
Top Bottom