AfCHPR: Serikali nyingi za Afrika bado hazikubali kushtakiwa na kutekeleza hukumu za Haki za Binadamu dhidi yake

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,120
Serikali za Afrika zilizoridhia kuanzishwa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu (AfCHPR) zimeshauri kutekeleza hukumu za mahakama hiyo na kutekeleza itifaki ya kukubali kushtakiwa.

Akizungumza katika Kikao cha 77 cha Tume ya Afrika ya Haki ya Binaadamu na Watu (ACHPR) jijini Arusha leo Oktoba 30, 2023 Rais wa Mahakama hiyo, Jaji Iman Aboud amesema kutotekelezwa kwa maamuzi ya Mahakama hiyo ni changamoto kubwa.

Katika hutuba ya Rais huyo katika kikao hicho, iliyosomwa na Msajili wa Mahakama hiyo, Dk Robert Eno amesema ili kulinda na kuendeleza haki za binadamu barani Afrika ni muhimu viongozi wa Serikali kuwa na utashi wa kisiasa kutekeleza maamuzi ya mahakama hiyo.

Rais Iman Aboud amesema katika hukumu ya kesi zaidi ya 200 ambazo zimetolewa na mahakama hiyo, maamuzi chini ya asilimia 10 ambayo yametekelezwa.

Amesema suala la Haki za Binadamu ni muhimu kuzingatiwa barani Afrika kwani hakuna maendeleo na amani bila kuwepo na haki za binadamu.

Pia serikali za Afrika zinapaswa kuruhusu kushitakiwa na Asasi za Kiraia na watu binafsi katika Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu (AfCHPR).

"Kukubali kushtakiwa ni utekelezwaji wa itifaki ya kuanzishwa mahakama hiyo hivyo," amesema.

Amesema miongoni mwa malengo ya kuanzishwa Mahakama hiyo ni kuwezesha kuboreshwa mifumo ya haki za binadamu barani Afrika hivyo ni muhimu serikali kutekeleza waliyoridhia.

Awali, Akizungumza katika niaba ya asasi za kiraia 300 ambazo zimekuwa na vikao vya ndani 35 kuanzia Oktoba 16-19, Hannah Forster amesema nchi nyingi barani Afrika zinapita katika wakati mgumu kukabiliana na matukio ya ukiukwaji wa haki za binadamu.

Amesema kinachoendelea katika nchi za Sudan, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na nchi za kadhaa za Afrika Magharibi ni kielelezo cha ukiukwaji wa haki za binadamu na demokrasia.

Hata hivyo, ametaka serikali za Afrika kuondoa adhabu ya kifo kwani inakiuka haki ya binadamu ya kuishi.
 
Back
Top Bottom