Mkutano wa Wajane Afrika kufanyika Juni 2024, Tanzania kuwa Mwenyeji, wadau wadokeza mada zitakazojadiliwa

Nyakijooga

Senior Member
Dec 9, 2018
123
202
Tanzania inatarajiwa kuwa mwenyeji katika mkutano wa mwaka wa wajane wa Bara la Afrika ambao unatarajiwa kufanyikia Zanzibar kuanzia Juni 20 hadi 22, 2024 maandalizi ya awali ya mkutano huo tayari yameanza huku mkutano huo unaotarajiwa kufanyika ukiwa ni wakwanza kuandaliwa na umoja huo.

Akizunguza mkutano huo Katibu wa umoja wa wajane Afrika Rose Sarwatt, ambaye pia ni Mkurugenzi mwanzilishi wa taasisi ya Tanzania Windows Association (TAWIA) akiwa ameambata na ujumbe maluum kutoka kwenye umoja huo ngazi ya Afrika, amesema kuwa Tanzania inatarajiwa kuwa mwenyeji na tayari Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar imeridhia mkutano huo kufanyika huko ikiwa ni sehemu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Amesema kuwa mkutano huo unalenga kuwaleta pamoja wajane mbalimbali kutoka Afrika pamoja na wadau kutoka taasisi mbalimbali za Kitaifa na kimataifa pamoja na wadau wengine ili kwa pamoja waweze kushiriki katika mijadala na masuala yanayokudiwa kujadiliwa.

Pia Dr Monica Mhoja ambaye ni Mwenyekiti wa masuala ya maudhui katika Kamati ya maandalizi ya Mkutano huo.

Mkutano huo wa kwanza huo ambao unafanyika kuanzia Juni 20 hadi 22, 2024 ni wa kihistoria ni mambo gani tunaenda kuyachambua na kuyajadili, kwanza umuhimu kabisa kuna mikutano mingi ya kikanda na kidunia ambayo imefanyika lakini kwa mara ya kwanza tunakuwa na mkutano wa wajane ambao unafanyika barani Afrika kwahiyo kwa Tanzania na Zanzibar tumetengeneza historia na tunaenda kuangalia mambo gani, tutakuwa tunaangalia masuala matatu muhimu, kwanaza kuwajengea nguvu ya uchumi wajane" ameeleza Dr. Monica.

Akifafanua dhamira hiyo ya kwanza amesema kuwa wajane ni kati ya makundi ya Wanawake katika jamii hususani Afrika ambao wapo nyuma sana.

"Kwahiyo tutaangalia je, hao wajane ambao wananyimwa haki zao ambao kuna mila na desturi zinazowagandamiza ambao wanaonekana kama ni raia daraja la tatu inakwaje waweze kujengewa nguvu ya kiuchumi, kwahiyo maswala hayo yatachambuliwa na kujadiliwa "ameeleza Dr. Monica

Amesema kuwa kutakuwepo na mikutano midogo midogo ambayo itajadili kwa kina maswala hayo.

Aidha amesema kuwa maswala mengine ambayo yanatarajiwa kujadiliwa kwenye mkutano huo ni haki za mirathi, haki za aridhi na mabadiliko ya tabia ya Nchi Afrika.

Ameeleza kuwa watajadili kwa kina mada hizo na kubaini athari za masuala hayo kwa wajane, amesema kuwa watagusia tamaduni mbalimbali ambazo ziwazunguka wajane kwa kuwaona kama sio watu muhimu ambao hawastaili kupatiwa baadhi ya haki kwa usawa.

Dr. Monica amesema kuwa mkutano huo pia utatoka na mapendekezo ya nini kifanyike kulinga na mada usika ambazo zinakusudiwa kujadiliwa kwa kina katika mkutano huo, amesema mapendekezo hayo yanaweza kuwa na mkakati wa namna bora ambavyo masuala husika yanavyoweza kufanyiwa kazi kwa lengo la kuchochea mabadiliko chanya.

"Tunataka wajane wa Afrika wahakikishiwe kupata haki zao za kiuchumi, wanapata haki zao za kumiliki aridhi wanapata haki zao za kurithi, kukiwa na sera na matamko yatakayotolewa na kusaidia utekelezaji katika Nchi zote za Afrika ambao ni wanachama wa Umoja wa Afrika hilo ni suala nyeti ambalo tunaliangalia" amesema ameeleza Dr. Monica

Vilevile kwa upande wa Mwenyekiti wa progmu ya The African Widows Summit 2024', Martina Kabisama ambaye ni Mwenyekiti wa Bodi ya Tanzania Widows Association (TAWIA) amesema kuwa mkutano huo unagusa makundi mbalimbali ikiwemo Serikali za Nchi washiriki, amesema hivyo wanatarajia kuwepo kwa viongozi mbalimbali na wadau kutokana utendaji kazi zao kugusa maeneo yanayowahusu wajane, huku akisema kuwa ni bahati mkutano huo kufanyikia Tanzania.

"Katika Bara la Afrika kuna Umoja wa Wajane (The Union of Africa Widows), na huu umoja una uongozi wake, tunashukuru huu umoja ulikuja na mkakati wa kuandaa mkutano mkubwa unaoitwa 'The African Widows Summit 2024', ungeweza kufanyika kokote kule barani Afrika lakini imekuwa bahati umeletwa Tanzania na utafanyikia visiwani Zanzibar" amesema Martina Kabisama.

Ameongeza kuwa Kamati yao ya maandalizi itashirikiana vyema na Serikali kuhakikisha maandalizi yanaenda vizuri kuelekea mkutano huo wa kwanza.View attachment 2840062

IMG-20231211-WA0018.jpg
 
Sifa za kuwa mjane ni zipi, mbona tunaona wanawake wengi tu wakifiwa na waume zao wanaolewa tena? Inawezekana vipi binti afiwe na mume wake aendelee kuishi bila kupata mume mwingine maishani mwake tena?
 
Tanzania inatarajiwa kuwa mwenyeji katika mkutano wa mwaka wa wajane wa Bara la Afrika ambao unatarajiwa kufanyikia Zanzibar kuanzia Juni 20 hadi 22, 2024 maandalizi ya awali ya mkutano huo tayari yameanza huku mkutano huo unaotarajiwa kufanyika ukiwa ni wakwanza kuandaliwa na umoja huo.

Akizunguza mkutano huo Katibu wa umoja wa wajane Afrika Rose Sarwatt, ambaye pia ni Mkurugenzi mwanzilishi wa taasisi ya Tanzania Windows Association (TAWIA) akiwa ameambata na ujumbe maluum kutoka kwenye umoja huo ngazi ya Afrika, amesema kuwa Tanzania inatarajiwa kuwa mwenyeji na tayari Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar imeridhia mkutano huo kufanyika huko ikiwa ni sehemu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Amesema kuwa mkutano huo unalenga kuwaleta pamoja wajane mbalimbali kutoka Afrika pamoja na wadau kutoka taasisi mbalimbali za Kitaifa na kimataifa pamoja na wadau wengine ili kwa pamoja waweze kushiriki katika mijadala na masuala yanayokudiwa kujadiliwa.

Pia Dr Monica Mhoja ambaye ni Mwenyekiti wa masuala ya maudhui katika Kamati ya maandalizi ya Mkutano huo

Mkutano huo wa kwanza huo ambao unafanyika kuanzia Juni 20 hadi 22, 2024 ni wa kihistoria ni mambo gani tunaenda kuyachambua na kuyajadili, kwanza umuhimu kabisa kuna mikutano mingi ya kikanda na kidunia ambayo imefanyika lakini kwa mara ya kwanza tunakuwa na mkutano wa wajane ambao unafanyika barani Afrika kwahiyo kwa Tanzania na Zanzibar tumetengeneza historia na tunaenda kuangalia mambo gani, tutakuwa tunaangalia masuala matatu muhimu, kwanaza kuwajengea nguvu ya uchumi wajane" ameeleza Dr. Monica

Akifafanua dhamira hiyo ya kwanza amesema kuwa wajane ni kati ya makundi ya Wanawake katika jamii hususani Afrika ambao wapo nyuma sana

"Kwahiyo tutaangalia je, hao wajane ambao wananyimwa haki zao ambao kuna mila na desturi zinazowagandamiza ambao wanaonekana kama ni raia daraja la tatu inakwaje waweze kujengewa nguvu ya kiuchumi, kwahiyo maswala hayo yatachambuliwa na kujadiliwa "ameeleza Dr. Monica

Amesema kuwa kutakuwepo na mikutano midogo midogo ambayo itajadili kwa kina maswala hayo.

Aidha amesema kuwa maswala mengine ambayo yanatarajiwa kujadiliwa kwenye mkutano huo ni haki za mirathi, haki za aridhi na mabadiliko ya tabia ya Nchi Afrika.

Ameeleza kuwa watajadili kwa kina mada hizo na kubaini athari za masuala hayo kwa wajane, amesema kuwa watagusia tamaduni mbalimbali ambazo ziwazunguka wajane kwa kuwaona kama sio watu muhimu ambao hawastaili kupatiwa baadhi ya haki kwa usawa.

Dr. Monica amesema kuwa mkutano huo pia utatoka na mapendekezo ya nini kifanyike kulinga na mada usika ambazo zinakusudiwa kujadiliwa kwa kina katika mkutano huo, amesema mapendekezo hayo yanaweza kuwa na mkakati wa namna bora ambavyo masuala husika yanavyoweza kufanyiwa kazi kwa lengo la kuchochea mabadiliko chanya.

"Tunataka wajane wa Afrika wahakikishiwe kupata haki zao za kiuchumi, wanapata haki zao za kumiliki aridhi wanapata haki zao za kurithi, kukiwa na sera na matamko yatakayotolewa na kusaidia utekelezaji katika Nchi zote za Afrika ambao ni wanachama wa Umoja wa Afrika hilo ni suala nyeti ambalo tunaliangalia" amesema ameeleza Dr. Monica

Vilevile kwa upande wa Mwenyekiti wa progmu ya The African Widows Summit 2024', Martina Kabisama ambaye ni Mwenyekiti wa Bodi ya Tanzania Widows Association (TAWIA) amesema kuwa mkutano huo unagusa makundi mbalimbali ikiwemo Serikali za Nchi washiriki, amesema hivyo wanatarajia kuwepo kwa viongozi mbalimbali na wadau kutokana utendaji kazi zao kugusa maeneo yanayowahusu wajane, huku akisema kuwa ni bahati mkutano huo kufanyikia Tanzania.

"Katika Bara la Afrika kuna Umoja wa Wajane (The Union of Africa Widows), na huu umoja una uongozi wake, tunashukuru huu umoja ulikuja na mkakati wa kuandaa mkutano mkubwa unaoitwa 'The African Widows Summit 2024', ungeweza kufanyika kokote kule barani Afrika lakini imekuwa bahati umeletwa Tanzania na utafanyikia visiwani Zanzibar "amesema Martina Kabisama

Ameongeza kuwa Kamati yao ya maandalizi itashirikiana vyema na Serikali kuhakikisha maandalizi yanaenda vizuri kuelekea mkutano huo wa kwanza .View attachment 2840062View attachment 2840063
Kuna fedha pahala hazina kazi, zinatafutiwa uhalali. Hapo hakuna mkutano ni maosnyeshso ya kutafuta wanaume [wababu w akizungu].
 
Hivi kila mwanamke aliyefiwa na mume anastahili kuitwa mjane na kusaidiwa? Wanawake wengine wameachiwa ukwasi mwingi hata sifa ya ujane na kusaidiwa hawana. Unakuta mfiwa ana mali nyingi, yeye ndiye anastahili kuisadia wengine. Mjane ni yule ambaye alimtegemea mume wake, mume hayupo na hana kitu amekuwa masikini wa kusaidiwa. Ukute jimama linajiweza linakula na kuvaa vizuri shida halina, hapo utaliitaje mjane? Kwanza hata part time show likitaka linapata kama kawaida. Dhana ya ujane iendane na hali halisi, si kila mwanamke aliyefiwa na mume wake anaweza kuwa na sifa za kuitwa mjane, wengine wanaoleka tena na kuwa na wenza wapya. Wajane wawe ni wale ambao hawaoleki tena na hawana uwezo wa kuendesha maisha yao ya kila siku peke yao bila kusaidiwa
 
Back
Top Bottom