Mkutano wa Sullivan: Al Bashir afananisha waasi na magaidi

Lunyungu

JF-Expert Member
Joined
Aug 7, 2006
Messages
8,854
Points
1,250

Lunyungu

JF-Expert Member
Joined Aug 7, 2006
8,854 1,250
Mkutano wa Sullivan: Al Bashir afananisha waasi na magaidi
Na Daniel Mjema, Arusha

RAIS wa Sudan, Omari Hassan Al Bashir, amesema waasi wanaoendeleza mapigano Jimbo la Darfur nchini humo, baada ya kusainiwa kwa makubaliano ya amani, hawana tofauti na magaidi.


Al Bashir alitoa kauli hiyo juzi jijini Arusha, wakati akitoa hotuba katika Mkutano wa Taasisi ya Kimataifa ya Leon H. Sullivan. Marais sita walitoa hotuba zao akiwemo Rais Jakaya Kikwete.


Alisema Sudan imekuwa na uhusiano mzuri na nchi nyingine za Afrika isipokuwa Chad, ambayo imekuwa ikiendelea kusaidia vikundi vya waasi nchini humo kwa lengo la kuvuruga amani.


"Vikundi hivi vya waasi vinavyoendeleza mapigano, badala ya kuheshimu njia ya mazungumzo kutafuta suluhisho la amani, ni magaidi na tutaendelea kupambana nao kuhakikisha amani inakuwepo," alisema.


Rais Al Bashir alisema, nchi yake itaendelea kutoa ushirikiano kwa Umoja wa Nchi za Afrika (AU), ili uweze kusimamia kikamilifu utekelezaji wa makubaliano ya amani yaliyofikiwa Abuja, Nigeria.


Alisema ukiondoa 'magaidi' hao, wananchi wa Sudan hivi sasa wako katika mshikamano na kusimamia umoja wa kitaifa na kuomba, nchi zilizoendelea kuifutia madeni kutokana na amani iliyopo.


"Hapa tulipofika ni pazuri, hivyo tunategemea vikwazo tulivyowekewa kutokana na mgogoro wa Darfur sasa vinaondolewa. Pia, tutapata msamaha wa madeni na hakika hatutarudi tena kwenye vita," alisema.
 

Susuviri

JF-Expert Member
Joined
Oct 6, 2007
Messages
3,713
Points
1,250

Susuviri

JF-Expert Member
Joined Oct 6, 2007
3,713 1,250
Hivi mmeona jinsi Sullivan ilivyoleta looser presidents with the exception of Paul Kagame and Kufour who I hold in high esteem. Sasa huyu Al Bashir ambaye karibuni atashtakiwa for crimes against humanities tunamwalika wa nini? Alafu eti rais wa Western Sahara akina Polisario... jamani! Huu ni upuuzi mtupu! Kweli hii serikali ni ya Ze comedy! akina Masanja wangeweza kuleta guest list nzuri zaidi.
 

Jamco_Za

JF-Expert Member
Joined
Jul 14, 2007
Messages
1,333
Points
1,225

Jamco_Za

JF-Expert Member
Joined Jul 14, 2007
1,333 1,225
Kwanini walialika maraisi wasiokuwa wa maana, nimeona na raia mmoja wa somalia ambaye ameishi nchini kwa miaka mingi kaalikwa analalamika kuwa kanyimwa uraia.
 

Mtu wa Pwani

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2006
Messages
4,156
Points
1,250

Mtu wa Pwani

JF-Expert Member
Joined Dec 26, 2006
4,156 1,250
hivi Bashiri ni loooser? kivipi wakuu ?

nnasikia kaijenga nchi yake vizuri kama sikosei ni top ten za afrika au looser wake uko eneo gani ?
 

Forum statistics

Threads 1,381,979
Members 526,245
Posts 33,816,175
Top