Mkutano wa Rais Kikwete na TCD: Vyama vya siasa vyatakiwa kuweka utaifa Mbele

MwanaDiwani

JF-Expert Member
Mar 22, 2013
5,536
2,264
Vyaonywa maslahi ya vyama yataiweka nchi pabaya

VIONGOZI wa vyama vya siasa watakaokwenda kukutana na Rais Jakaya Kikwete, wametakiwa kuweka mbele masuala yanayohusu taifa na si misimamo binafsi ya vyama vyao.

Aidha wasomi nchini wamempongeza Rais Kikwete kwa kukubali kukutana na viongozi wa vyamaa hivyo vya siasa kwa kuwa ni ishara nzuri kwa kiongozi wa nchi kutokuwa na ubaguzi hata kwa watu wasiomuunga mkono.

Hatua hiyo imekuja muda mfupi baada ya Rais Kikwete kukubali kukutana na viongozi wa vyama vinavyounda Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD).
Viongozi hao waliazimia kutafuta nafasi ya kukutana na Rais Kikwete kwa lengo la kushauriana naye kuhusu mambo mbalimbali, ukiwemo mchakato wa kupatikana kwa Katiba Mpya, unaoendelea mjini Dodoma. Kikao hicho kinatarajiwa kufanyika hivi karibuni.

TCD inaundwa na vyama vyenye uwakilishi bungeni, ambavyo ni CCM, CUF, CHADEMA, TLP, NCCR-Mageuzi na UDP. Mwenyekiti wa sasa wa TCD ni Cheyo

Cheyo(6)(2).jpg

John Cheyo
Akizungumza na waandishi wa habari mjini Dar es Salaam jana, Kaimu Mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba Tanzania (JUKATA), Hebron Mwakagenda, alisema ni vyema viongozi hao wa vyama vya siasa watakapokwenda kukutana na Rais Kikwete, wabebe maslahi ya taifa na si ya vyama.

Mwakagenda alisema viongozi hao wanapaswa kuweka kando misimamo ya vyama vyao na badala yake waungane pamoja na kwenda kujadili masuala yanayohusu taifa.

Wakati huo huo, Mjumbe wa Kamati ya Uongozi ya JUKATA, George Mollel, amesema hakuna sababu ya kufanyika kwa maandamano ya kutaka kusitishwa kwa Bunge Maalumu la Katiba kwa sababu hayana faida, badala yake watu wengi wasiokuwa na hatia wataumia na wengine kupoteza maisha.

Mollel alisema jana kuwa, badala ya kufanyika kwa maandamano, wanaotaka kuyafanya watumie hoja katika kupinga kuendelea kwa vikao hivyo.

Hivi karibuni, viongozi wanaounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA), walitangaza kuitisha maandamano nchi nzima kupinga kuendelea kwa vikao vya Bunge Maalumu la Katiba mjini Dodoma.

Katika hatua nyingine, Mkuu wa Idara ya Sayansi ya Siasa na Utawala ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk. Benson Bana, amempongeza Raisk Kikwete kwa kukubali kukutana na viongozi wa vyama vya siasa nchini.

Dk. Bana alisema mjini Dar es Salaam jana kuwa, hiyo ni ishara tosha kuwa kiongozi huyo wa nchi hana ubaguzi na ni karama aliyojaaliwa na Mola ya kumsikiliza kila mtu.

Msomi huyo alisema anaamini kikao hicho kitasaidia kufikiwa kwa muafaka iwapo viongozi hao wa kisiasa watakuwa na hoja kwa sababu Bunge walilogomea kushiriki baadhi ya vyama, lipo kwa mujibu wa sheria na Rais yupo kwa mujibu wa sheria.

Kwa upande wake, Mhadhili wa Chuo Kikuu cha Mzumbe, Mohammed Bakari, alisema amefurahishwa na hatua ya Rais ya kukubali kukutana na viongozi hao kwa sababu ameonyesha kuwa ni muungwana na ana dhamira ya dhati ya kutaka maridhiano yafikiwe na hatimaye katiba mpya ipatikane.

Hata hivyo, Mhadhili huyo alitoa ombi kwa UKAWA, ambapo aliwataka kutumia nafasi hiyo vizuri na hatimaye maridhiano yapatikane, lengo likiwa ni kuhakikisha Katiba Mpya inapatikana na mwisho wa siku wasije wakadai kuwa Rais amevuruga mchakato huo.

Wafuasi wa UKAWA walitoka nje Bunge hilo Aprili 16, mwaka huu, baada ya Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba (mjumbe wa bunge hilo) kuhitimisha kuchangia. Katika mchango wake, Lipumba alidai hawawezi kuendelea kushiriki dhuluma dhidi ya wananchi kwa kupitisha katiba ambayo ni kinyume cha matakwa yao.

Baada ya kauli hiyo, Lipumba aliotoka ndani ya Bunge hilo, akifuatiwa na Mwenyekiti wa UKAWA, ambaye pia ni Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia na wafuasi wao.

Chanzo: Uhuru newspaper

Naomba ieleweke kuwa Rais Kikwete hakuombwa kukutana na kikundi kinachojiita UKAWA. Rais Kikwete alishasema hawezi kukutana na kikundi cha watu wenye ajenda zinazobadilika kama upepo.

Rais Kikwete atakutana na Viongozi wa vyama vinavyounda Kituo cha Demokrasia Tanzania(TCD). Viongozi wa Kikundi kinachojiita UKAWA wametokea kuwa ni wanachama wa Kituo cha Demokrasia Tanzania kama ilivyo CCM ambayo nayo ni Mwanachama.

Kuna baadhi ya watu, vyama na viongozi wameanza kutafuta umaarufu kuhusu mkutano huu kwa kutumia mgongo wa nyuma kuhusu uamuzi wa Rais Kikwete kukutana na Viongozi wa vyama vinavyounda Kituo cha Demokrasia Tanzania(TCD) ambacho Mwenyekiti wake ni Mh. John Cheyo.

Wakati wa hotuba yake ya Mwezi Julai, 2014, pamoja na mambo mengine, Rais Kikwete alinukuliwa akisema,
Ndugu Wananchi;
Kinachonishangaza, zaidi ni kwamba, kama hawakuridhishwa na yaliyofanyika, kwa nini wasingetumia mifumo waliyojitengenezea wenyewe kwenye Kanuni kumaliza tofauti zao? Kanuni zinaelekeza kuwa mambo wasiyoridhika nayo yajadiliwe kwenye Kamati ya Mashauriano na Maridhiano. Ukiacha mifumo ya maridhiano ndani ya Bunge ukaenda nje kwa wananchi au vyombo vya habari na mitandao si jawabu la tatizo.

Ndugu Wananchi;
Ndiyo maana nashawishika kuunga mkono wale wote wanaowasihi Wajumbe wa CHADEMA, CUF na NCCR-Mageuzi na wengine warejee Bungeni. Watumie mifumo maalum ya Bunge iliyowekwa na Kanuni kutafuta maridhiano. Hali kadhalika, wasichoke kuwa na mawasiliano na vyama vingine vya siasa na hasa CCM kutafuta maelewano. Mimi niko tayari kusaidia pale watakapoona inafaa kufanya hivyo kama ambavyo nimekuwa nikifanya ziku za nyuma.
 
Ni sawa na 'Mwanadiwani' kusema, 'Nataka kukutana na Mwenyekiti wa CCM ndugu Jakaya Kikwete, sitaki kukutana na Mheshimiwa Rais. Hata kama maneno yatazungushwa namna gani, ukweli haubadiliki kuwa Kikwete atakutana na viongozi wa UKAWA, period! Nyingine zote ni hadithi.

Naomba ieleweke kuwa Rais Kikwete hakuombwa kukutana na kikundi kinachojiita UKAWA. Rais Kikwete alishasema hawezi kukutana na kikundi cha watu wenye ajenda zinazobadilika kama upepo.

Rais Kikwete atakutana na Viongozi wa vyama vinavyounda Kituo cha Demokrasia Tanzania(TCD). Viongozi wa Kikundi kinachojiita UKAWA wametokea kuwa ni wanachama wa Kituo cha Demokrasia Tanzania kama ilivyo CCM ambayo nayo ni Mwanachama.

Kuna baadhi ya watu, vyama na viongozi wameanza kutafuta umaarufu kuhusu mkutano huu kwa kutumia mgongo wa nyuma kuhusu uamuzi wa Rais Kikwete kukutana na Viongozi wa vyama vinavyounda Kituo cha Demokrasia Tanzania(TCD) ambacho Mwenyekiti wake ni Mh. John Cheyo.

Wakati wa hotuba yake ya Mwezi Julai, 2014, pamoja na mambo mengine, Rais Kikwete alinukuliwa akisema,
 
Ni sawa na 'Mwanadiwani' kusema, 'Nataka kukutana na Mwenyekiti wa CCM ndugu Jakaya Kikwete, sitaki kukutana na Mheshimiwa Rais. Hata kama maneno yatazungushwa namna gani, ukweli haubadiliki kuwa Kikwete atakutana na viongozi wa UKAWA, period! Nyingine zote ni hadithi.
Na ieleweke kuwa, kama kikundi kinachojiita UKAWA kingeomba kukutana na Rais Kikwete, Taasisi ya Rais isingepoteza hata muda wa kujibu maombi yao achilia mbali kuonana na Rais Kikwete.

Kikundi kinachojiita UKAWA inabidi kumshukuru Mwenyekiti wa Kituo cha Demokrasia Tanzania(TCD), Mh. John Cheyo kwa kutumia hekima na busara zake katika kuwawezesha viongozi wa kikundi kinachojiita UKAWA kwenda kuonana na Rais Kikwete kwa kutumia mgongo wa Kituo cha Demokrasia Tanzania(TCD).

Kwa lugha nyingine tunaweza kusema, kikundi kinachojiita UKAWA kimepata political lift kwenye gari la TCD kwenda Ikulu.
 
Wanazungusha zungusha ukweli ili kuwazuga Watanzania kwamba Kikwete hakukutana na UKAWA ili kumnusuru DHAIFU asiendelee kuonekana DHAIFU kwa maamuzi yake ambayo hayajali maslahi ya Tanzania na badala yake yanajali maslahi ya chama chake. Bunge la Posho limeshapoteza muelekeo wake na iwapo katiba mpya itashindwa kupatikana basi wa kwanza kubebeshwa lawama za kutopatikana katiba mpya si mwingine bali Kikwete DHAIFU.

Ni sawa na 'Mwanadiwani' kusema, 'Nataka kukutana na Mwenyekiti wa CCM ndugu Jakaya Kikwete, sitaki kukutana na Mheshimiwa Rais. Hata kama maneno yatazungushwa namna gani, ukweli haubadiliki kuwa Kikwete atakutana na viongozi wa UKAWA, period! Nyingine zote ni hadithi.
 
Hakuna jipya hapo,ameona maji yapo shingoni ndio anakuja na mbwembwe zake
Ndugu,
Jipya ndiyo lipi na muonekano wa maji ya shingoni uko vipi?

Rais Kikwete ameombwa na yeye akayakubali maombi kwa sababu yanatoka kwenye official political institute.
 
VIONGOZI wa vyama vya siasa watakaokwenda kukutana na Rais Jakaya Kikwete, wametakiwa kuweka mbele masuala yanayohusu taifa na si misimamo binafsi ya vyama vyao.

Naamini rais Kikwete atatumia ueledi, juhudi, na maarifa yake yote kumshawishi Mwenyekiti wa CCM taifa, chama pekee ambacho kinapingana wazi wazi na maoni ya wananchi yaliyokusanywa na kuandikwa kisheria na tume ya Warioba katika rasimu ya katiba.
Mwenyekiti huyo wa CCM alidiriki kutetea wazi wazi masimamo wa chama chake siku analizindua bunge. Namuomba sana rais Kikwete ajitahidi kumshawishi Mwenyekiti huyo na chama chake waunge mkono maoni ya Watanzania juu ya katiba itakayoongoza taifa lao kwa miaka mingi ijayo regardless ni chama gani kitakuwa kipoa hai, au kinaongoza kwa wakati fulani...
 
Hivi huu Utaifa/uzalendo unoimbwa huwa ni kwa vyama vya upinzani,

Kwa CCM wao utaifa is a foreign vocabulary, Hawa JUKATA mbona wanazunguka mbuyu?! Hivi kuna UTAIFA gani zaidi ya kuheshimu maoni ya wananchi yaliko kwenye rasimu ya katiba?!

Au wao JUKATA kutupilia mbali maoni ya wananachi ndiyo UTAIFA?!

JUKATA semeni tu ukweli kwamba JK na CCM waache U-CCM, wavae UTAIFA kwa kuheshimu maoni ya wananchi ambayo ndiyo msingi ya mamlaka yao.
 
Hapa Tz ni unafiki mwingi hakuna la maana! Najiuliza ni possible kubadili red kuwa njano nikimaanisha kwamba ni yuleyule m/kiti aliyesimama na mwenye kubeba ujumbe wa chama chake kwenye ufunguzi wa BMK na ndo chanzo wa maswala yote haya, hv leo hii syo m/kiti tena? Halafu hawa wahadhiri wa vyuo vikuu hiyo elimu yao waliipata kusifia tu hasa bana yaan yeye kukosoa ni mwiko, tuache unafiki
 
very sucumumbium
Naamini rais Kikwete atatumia ueledi, juhudi, na maarifa yake yote kumshawishi Mwenyekiti wa CCM taifa, chama pekee ambacho kinapingana wazi wazi na maoni ya wananchi yaliyokusanywa na kuandikwa kisheria na tume ya Warioba katika rasimu ya katiba.
Mwenyekiti huyo wa CCM alidiriki kutetea wazi wazi masimamo wa chama chake siku analizindua bunge. Namuomba sana rais Kikwete ajitahidi kumshawishi Mwenyekiti huyo na chama chake waunge mkono maoni ya Watanzania juu ya katiba itakayoongoza taifa lao kwa miaka mingi ijayo regardless ni chama gani kitakuwa kipoa hai, au kinaongoza kwa wakati fulani...
 
Hapa Tz ni unafiki mwingi hakuna la maana! Najiuliza ni possible kubadili red kuwa njano nikimaanisha kwamba ni yuleyule m/kiti aliyesimama na mwenye kubeba ujumbe wa chama chake kwenye ufunguzi wa BMK na ndo chanzo wa maswala yote haya, hv leo hii syo m/kiti tena? Halafu hawa wahadhiri wa vyuo vikuu hiyo elimu yao waliipata kusifia tu hasa bana yaan yeye kukosoa ni mwiko, tuache unafiki
Ukitaka kujua kuwa wewe ni mburula umemuona jk tu kwenye hili lakini ukawa hujawaona sijui kama unajitambua vema.
 
Ni sawa na 'Mwanadiwani' kusema, 'Nataka kukutana na Mwenyekiti wa CCM ndugu Jakaya Kikwete, sitaki kukutana na Mheshimiwa Rais. Hata kama maneno yatazungushwa namna gani, ukweli haubadiliki kuwa Kikwete atakutana na viongozi wa UKAWA, period! Nyingine zote ni hadithi.

Kwahiyo na mh.cheyo naye ni mwana ukawa?
 
Ndugu,
Jipya ndiyo lipi na muonekano wa maji ya shingoni uko vipi?

Rais Kikwete ameombwa na yeye akayakubali maombi kwa sababu yanatoka kwenye official political institute.

Nani asiyejua kuwa John Momose Cheyo (Mwenyekiti wa TCD) ni mdomo wa CCM? Inaelekea baada ya wewe kushindwa hiyo kazi ndio mmeamua kupitia kwa kibaraka wenu John Cheyo na si vingenevyo, lakini bado na huko mtapewa msimamo uleule wa UKAWA mpaka hapo mtakapokubali kujadili rasimu iliyopendekezwa na wanainchi kupitia Tume ya Warioba
 
Kama hii ndiyo hoja, kwa nini kikundi kinachojiita cha UKAWA kimeamua kuhudhuria kikao kilichoombwa na mdomo wa CCM.

Wanaenda kufanya nini kwenye kikao cha CCM kama unavyotaka ieleweke?
 
Acha kiroba wewe MwanaDiwani ...wewe na vyombo vyote vya habari ambavyo viliandika...
KIKWETE: NIPO TAYARI KUKUTANA NA UKAWA KULIKO HALI INAVYOENDELEA BUNGENI........Nani zaidi? emb acha kiroba.....acha kabisa!!!!
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom