PreGE2025 Mkutano wa Heche washambuliwa Igunga, Tabora

PreGE2025 Mkutano wa Heche washambuliwa Igunga, Tabora

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,129
CHADEMA kupitia ukurasa wao wa X(Twitter) wamesema watu waliokuwa na mapanga na visu wamevamia mkutano wao maeneo ya Igunga mkoani Tabora, watu hao walianza kwa kurusha mawe msafara wa makamu mwenyekiti wa chama John Heche.

CHADEMA pia wamethibitisha kujeruhiwa kwa mlinzi wa makamu Mwenyekiti John Heche, aidha wakati hayo yanatokea jeshi la polisi halikuwepo eneo la tukio.

1749549864239.png

1749549730783.jpeg
-288186131.jpg

6789b7c0-3bd3-4311-8c4e-fb6b8303bd1e.jpg

0557361b-bfdc-4641-b118-13bb0ea5f613.jpg

e3ba51f0-9e45-47cc-b109-5a7c00605e03.jpg

Vurugu zimezuka katika mkutano uliokuwa uhutubiwe na Makamu Mwenyekiti wa Chadema, John Heche leo Juni 10, 2025 wilayani Igunga Mkoa wa Tabora, baada ya watu waliokuwa na visu na mapanga kushambulia wanachi waliokuwa katika mkutano huo.

Taarifa kutoka ukurasa wa X (zamani Twitter) wa Chadema na vyanzo vingine zimeeleza kuwa kuwa, mlinzi wa Heche amejeruhiwa baada ya watu hao kurusha mawe msafara wa Heche.

Hata hivyo, watu hao walidhibitiwa na wananchi waliokuwa kwenye mkutano huo.

Imeelezwa kuwa polisi hawakuwepo wakati wa mashambulizi hayo, lakini baadaye walifika wakati vurugu zimeshaisha.

Katika ukurasa wake wa X, Heche ameandika:
"Muda huu hapa Igunga vijana wa CCM wamevamia mkutano wetu wameshambulia mkutano kwa mawe na kuumiza watu kadhaa kwenye mkutanoMkutano wetu ulikua na taarifa kwa polisi, lakini hakuna askari hata mmoja alikua kwenye mkutano kwasababu hili tukio lilipangwa.Hatutaacha kufanya mikutano yetu kwasbabau zozote zile."
Hata hivyo, madai hayo yamepingwa na Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM), Mohamed Kawaida katika mtandao huo akisema, "Hakuna kijana wa CCM alieshiriki katika hayo mambo yenu ya hovyo, vijana wa CCM wanafanya siasa kupitia chama Chao, yanayoendelea kwenye mikutano yenu ni misuguano ya ndani kwenye chama chenu juu ya wale wanaopinga kunyimwa haki yao ya msingi ya kikatiba, hivo musitafute mchawi."
 
Attachments

  • 57476f8c-1fd2-4a02-9a93-2befa0271e67.jpg
    57476f8c-1fd2-4a02-9a93-2befa0271e67.jpg
    101.5 KB · Views: 17
  • 20250610-0842-22.8528234.mp4
    29.1 MB
Imenikumbusha vurugu za uchaguzi mdogo Igunga baada ya rostam aziz kujiuzulu ubunge.

Igunga Kuna nini?
 
chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA wamesema watu waliokuwa na mapanga na visu wamevamia mkutano wao maeneo ya igunga mkoani Tabora,watu hao walianza kwa kurusha mawe msafara wa makamu mwenyekiti wa chama john heche.

CHADEMA pia wamethibitisha kujeruhiwa kwa mlinzi wa makamu mwenyekiti john heche, aidha wakati hayo yana tokea jeshi la polisi halikuwepo eneo la tukio.View attachment 3363059
No reform no election
 
Muda huu hapa Igunga vijana wa CCM wamevamia mkutano wetu wameshambulia mkutano kwa mawe na kuumiza watu kadhaa kwenye mkutanoMkutano wetu ulikua na taarifa kwa polisi, lakini hakuna askari hata mmoja alikua kwenye mkutano kwasababu hili tukio lilipangwa
Duh,
Hao itakuwa ni uvccm wakishirikiana na policcm
 
View attachment 3363062
View attachment 3363066

View attachment 3363068

View attachment 3363071
Vurugu zimezuka katika mkutano uliokuwa uhutubiwe na Makamu Mwenyekiti wa Chadema, John Heche leo Juni 10, 2025 wilayani Igunga Mkoa wa Tabora, baada ya watu waliokuwa na visu na mapanga kushambulia wanachi waliokuwa katika mkutano huo.

Taarifa kutoka ukurasa wa X (zamani Twitter) wa Chadema na vyanzo vingine zimeeleza kuwa kuwa, mlinzi wa Heche amejeruhiwa baada ya watu hao kurusha mawe msafara wa Heche.

Hata hivyo, watu hao walidhibitiwa na wananchi waliokuwa kwenye mkutano huo.

Imeelezwa kuwa polisi hawakuwepo wakati wa mashambulizi hayo, lakini baadaye walifika wakati vurugu zimeshaisha.

Katika ukurasa wake wa X, Heche ameandika:
"Muda huu hapa Igunga vijana wa CCM wamevamia mkutano wetu wameshambulia mkutano kwa mawe na kuumiza watu kadhaa kwenye mkutanoMkutano wetu ulikua na taarifa kwa polisi, lakini hakuna askari hata mmoja alikua kwenye mkutano kwasababu hili tukio lilipangwa.Hatutaacha kufanya mikutano yetu kwasbabau zozote zile."
Hao nyumbu wakishaishiwa hoja hawachokagi kusababisha uzushi.
 
Back
Top Bottom