Kwa kweli mwenyekiti... baada ya kufikiria zaidi naona kama itaundwa task force /kikosi-kazi basi kisitumie kodi za wananchi.Fedha zichangishwa kwa harambee, watu wajitolee. Pia siku hizi kuna teknolojia ya mawasiliano - itumike kupata taarifa.Mikutano ifanywe kupitia tele/video conference kupunguza gharama.Tafiti za kwenye internet zifanyike kukusanya data.
Pia wananchi wenye mapenzi mema walioko China na nchi za karibu wanaweza kupewa usihirikiano na ubalozi wetu na kwa pamoja wakakamilisha kile ambacho kingefanywa na Task force na kutuletea taarifa.Mwisho kabisa nadhani maofisa wetu wa ubalozi wanaweza kutufanyia kazi hiyo maana ndio wanatuwakilisha huko.
Naunga mkono.
Agenda ya kwanza ninayopendekeza ni Jinsi ya Kupambana na ufisadi kwa lengo la kuwa na serkali adilifu yenye usimamizi thabiti na wenye tija.
Asante sana Kijana wetu Kiby,
Hakika unaonyesha una uchungu sana na Nchi hii ya Maziwa na Asali . . . .
Kwa hiyo unachosema ni kuwa "Kiongozi Wa Kuchaguliwa Atakayepatikana Anahujumu au Kuifisadisha Mali ya Taifa, Anyongwe Hadharani Mpaka Afe"?
Sasa hapa pana mgogoro kidogo? hatutakuwa tumevunja haki za binadamu? Wanaharakati mnasemaje kwa hili?
Kuna mfano wowote wa Nchi wanaofanya hivi?
Nakubaliana na wewe WoS. Kwa mamlaka niliyopewa . . . Ooops! Niliyojipa, naomba nikuteue uwe mwenyekiti wa kamati teuli ya JF juu ya suala zima la hukumu ya kifo litakalokuwa na hadidu rejea zifuatazo:
Unatakiwa uteue wanakamati 3 na uzingatie uwiano wa kijinsia na weledi. Report kamili iwe tayari siku ya Jumamosi kabla mkutano haujaisha.
- Kuangalia ni makosa gani ya Kifisadi na kuhujumu uchumi ambayo yatastahili adhabu kali
- Kujifunza kutoka kwa wenzetu Wachina ni nini hasa wanafanya na nini tunaweza kuiga katika kazingira yetu
- Kupata maoni ya Watanzania juu ya ama kuwe na hukumu ya kifo ama la kwa watakao hujumu uchumi na kama la basi adhabu mbadala iwe ipi
- Kuangalia uwezekano wa kuwa na mahakama maalumu itakayoyoshughulikia kesi za uhujumu uchumi na ufisadi kwa haraka badala ya ile ya kisutu ambayo miaka sasa kesi haziishi
- Na mengineyo ambayo kamati itaona yanafaa
Kuhusu masurufu na pesa ya safari, mnaruhusiwa kuendesha harambee na kuchangisha toka kwa wote wenye mapenzi mema.
Jibu lilishatolewa....ina maana hadi sasa tulishapewa position ya serikali kuwa Zanzibar siyo nchi... ni sehemu ya Jamhuri ya Muungano....( japo hata mimi bado nachanganyikiwa maana kama ni sehemu ya Muungano, na hapo hapo ina rais wake, bendera yake, Baraza lake la wawakilishi etc...inakuwaje, lakini coercive instruments of the State kama polisi, jeshi, etc hawana vya kwao)Mi naomba atakayechaguliwa kwanza atuambie hadhi ya Zanzibar ni nchi ama si nchi?:confused2::confused2:
Jibu lilishatolewa....ina maana hadi sasa tulishapewa position ya serikali kuwa Zanzibar siyo nchi... ni sehemu ya Jamhuri ya Muungano....( japo hata mimi bado nachanganyikiwa maana kama ni sehemu ya Muungano, na hapo hapo ina rais wake, bendera yake, Baraza lake la wawakilishi etc...inakuwaje, lakini coercive instruments of the State kama polisi, jeshi, etc hawana vya kwao)
kipaumbele kiwekwe kwenye ELIMU BORA na sio BORA ELIMU, na tungeanzia kwa wawakilishi wetu(wabunge) walau wawe na Shahada ya kwanza, ili kuwawezesha kujadili miswada kwa kina kwa faida ya Taifa