kaka si kweli kuwa cdm haipatani na waislamu na haya yaliletwa na ccm na watu wajinga wachache wameyashika unakumbuka jumbe za cm 2015? Tuwe waangalifu mwingine atakuuliza swala la kejer kuwa kwann mikutano ya kaf tunawaona waislamu tu? Kitu hichi mm na kataa c kweli wapo wakritu kafu vile vile wapo waislamu cdm haya yote ni matunda ya ccm
Heri ambao wamekuelewa, naamini wengi watatafakari. Iwe ni CDM, CUF au yeyote ukianza kumbeza mwanachama wa chama kingine kwa mtazamo wa kidini huo sio udini bali ni u.pu.m.bavu tu, haijalisha una digrii ngapi jua tu wewe unahitaji kuelimishwa na kukombolewa kifikra.
Hivi inakuwaje kunakuwepo na watanzania wachache wanaamini uongo saaaaana, lakini hawataki kutumia akili zao walizojaliwa na Mwenyezi Mungu tena bure kuchanganua mambo, wanakubali tu kula kila kitu pumba, maaragwe, tope, n.k. Hivi kweli macho yenu na akili zenu hazioni waislamu na wakristo wakiunga mkono vyama vyao mbalimbali wanavyo vipenda, CDM, CUF, NCCR, TLP, CCM, n.k. nani anawaloga akili zenu nyie vipofu mnaanza kugeukia umbea wa watu wazembe wa fikra na wasiotaka kujibidiisha kuleta mawazo mapya yenye changamoto mpya, BADILIKENI acha kuwa wazembe wa kufikiri.
Hebu tuelimike, tusiwe ma-boya ya kueleaelea tu kila kona na kulishwa matapishi, tujaribu kutumia busara na akili zetu vizuri kwa kufanya mijadala yenye maana na kuleta hoja zenye kutupeleka mbele sio huu upuuzi wa dini, dini, dini, dini,.....hata na shetani ana dini zake nyingi tu kwani unafikiri kubeza dini ya mwenzio ndio kunakufanya uwe muumini mzuri au uwe karibu na Mungu. Unaweza ukafaanya yote hayo na bado Jehanam ukaenda tu haijalishi ni Mwislamu au Mkristo au nani.