Mkutano wa CUF katika viwanja vya Jangwani

MATESLAA

JF-Expert Member
Aug 11, 2011
1,246
74
Wakuu,

Nimeshuka hapa kituo cha Jangwani naelekea moja kwa moja mpaka kiwanjani, napishana na defender ikiwa na askari watatu...

Nitazidi kuwapa update
Kuna mtu anazungumza sasa hivi anasema zamani CUF ilikuwa na kaulimbiu ya 'Jino kwa jino' na sasa ni Mchaka Mchaka hadi 2015 Prof. Lipumba atakapoingia Ikulu.
Anasema CDM kwa kushirikiana na CCM wametumia vyombo vya habari kuwa CUF ni CCM B
Mzungumzaji anasema vijana wa CUF wako tayari kwa lolote na wakati wowote
Anasema wamejipanda kuondoa CCM madarakani na wenzao wa vidole Viwili ambao majuzi wametuhumiwa kula rushwa bungeni
Kambaya ndie anazungumza kwa sasa. Anasema CUF ndio waanzilishi wa viwanja wa Jangwani. Anadai CHADEMA wamepageuza kwa kupaita Chadema Square
Anadai kuwa CHADEMA ilimfuata Kikwete 2005 agombee kupitia CHADEMA endapo asingepitishwa na CCM
Sasa CUF wako jangwani na wanawachana wau wa CDM ati hawana hazina ya viongozi kwa hoja kuwa kila mwaka wa uchaguzi ukifika wanaenda kuomba watu wa CCM wagombee kama ilivykuwa kwenye ishu ya kumuomba JK agombee urais kama asingechaguliwa ndani ya CCM.

Pia wanasema CDM wao hawana hazina ya viongozi maana Mwenyekiti wao hana elimu zaidi ya kujua elimu ya biashara ya kupiga disko.

Wanasema CDM ni sawa na CUF maana hata kada tajiri wa CCM anawasaidia CDM badala ya CUF.
Hajj Duni anawapa pole watanzania kwa mauji ya Mwangosi, anasema hivyo ni vita vya muda mrefu.

Anaendelea kwa kusema hakuanza kufa muandishi huyo bali walianza kufa CUF kwa makundi.
Wanaimba wimbo wao unasema "CCM ikifa, mimi siwezi kulia; nitaitupa Kagera iwe chakula cha mamba"
Prof. Lipumba anasogea kwenye mic anacheka cheka kisha anaanza kwa kusema:

"Wanaumeeeeee!!! Wanawakeeeee!!!!! CCM kwisha kwisha ndembe ndembe kifo cha mende"
Huyu ni Makamu Mwenyekiti wa CUF taifa, amewataka waislamu wote kujiunga na CUF, kwa vile CCM na CDM haviwataki.

Je, hajathibitisha madai ya siku nyingi kuwa CUF ni chama cha kidini?

PICHA kwa hisani ya Blog ya Mjengwa:

attachment.php

attachment.php

attachment.php

attachment.php
 
Naombeni mliopo jangwani mtupe updates maana TBC hawaeleweki hamna sauti naona vibagalashia tu
 
Wakuu kuna mchongaji anasalisa sasa ni zamu ya imamu
 
Ndio kwanza TBC wanarudi hewani mda huu.. Na sasa naona ndio mkutano unaelekea kuanza.
 
mbona mitambo ina kata kata sana!hawa tbc,mbona mitambo yao ni ya kuunga unga sana!
 
Katibu mkuu Maalim Seif yuko Marekani kudai kiti cha Zanzibar kwenye balara la Umoja wa mataifa!
 
Kuna mtu anazungumza sasa hivi anasema zamani CUF ilikuwa na kaulimbiu ya 'Jino kwa jino' na sasa ni Mchaka Mchaka hadi 2015 Prof. Lipumba atakapoingia Ikulu.
 
Mkutano wa CUF umeanza:Mbwembwe kibao na kukana "jino kwa jino"
-Mchungaji mhh..anaweza kuwa feki..Kaanza kama wachungaji wengine ila kmalizia kama Padri kafanya ishara ya msalaba kama mkatoliki, wakati anashuka jukwaani kagongeana na watu waliokua jukwaani,kwa style y akupongezwa kuwa kaweza igizo.Napata wasiwasi kam si mwigizaji.
-TBC wanakatakata, sijui wanarusha bure?
 
Aliye kuwa mbunge wa tandaimba anammwagia sifa njingi sana lipumba kwamba anadigrii 3 na vijana wa caf watakupeleka ikulu kwa mchakamchaka chinja
 
Back
Top Bottom