Mkutano wa CHADEMA Njombe na Matukio yake

Mkutano wa CHADEMA Njombe na Matukio yake

Ndio Mzee tunaelewa shida kila mara kura za maamuzi yetu magumu hazitoshi ndio maana bado CCM inatesa
 
Kama walishindwa kumuelewa Kolimba, kuna kitu wataelewa. Ndio maana Dr. anawapa siri, anajua hawataelewa.
 
Chadema kimemshinda angetoa huu ushauri huko kwanza kwamba kishughulikie matatizo yake ya ndani kwa sasa
 
Ccm hawajielewi wanapambana na kivuli badala ya kitu halisi, humu jf wameweka vijana wenye ID kibao! Yaani wana hofu isiyo ya kawaida!!
 
Bahati mbaya hili somo si jipya. Akihutubia mkutano huko Njombe jana (juzi?) kawaeleza ccm ukweli kuwa kwa nini wasishughulike na kero za wananchi hadi waone chadema ndio kero? Kwamba hata umati unaoonekana kwenye mikutano ya cdm isingekuwa mikubwa hivi. Hapa kuna somo kubwa sana kwamba ccm haijui matatizo ya wananchi wake tangu enzi na enzi. Ccm inapigana vita isiyoijua. Ccm inahangaika na matawi badala ya kugundua kuwa mizizi ndio tatizo.

Haya yameanza tangu vyama vingi viliporudishwa tena 1992. Nccr walisambaratishwa na ccm. Cuf wakafuatia, sasa ccm inahangaika kukisambaratisha chadema. Yaliyoko kwenye ilani ya ccm ni danganya toto maana wanasema wametekeleza ahadi wakati kila siku hali ni mbovu. Hawana vipaumbele. Hawajui ni wakati gani washike maji au barabara au kilimo. Mwisho wa siku wanaharibu na kuona adui yao ni vyama vya upinzani. Ccm haitaki kumaliza kero za wananchi kwa kuwa wanajua kero ndio mtaji wao kinapofika kipindi cha uchaguzi. Hata wakimaliza kero zote bado kuna tabia ya binadamu kupenda kitu tofauti. Sasa hawataki kumaliza kero za wananchi wala kutoka madarakani.

Kauli ya Dk Slaa inaonyesha ni jinsi gani chadema imechoka na kusumbiliwa na vyombo vya Dola hadi kuamua kuusema ukweli rasmi. Pamoja na ukweli huu bado ccm hawawezi kuuona ukweli kwa kuwa Mungu keshaifanya mioyo yao kuwa migumu.

Na wananchi muamke! Nini msichokijua kuhusu ccm? Ni chama adui wa demokrasia. Ni chama adui wa maendeleo. Ni chama adui wa changamoto. Ni chama adui wa mabadiliko. Adui wa ccm ni watendaji wake kama kina Maghembe ambao wanaleta Bungeni mifumo ya proposal zao za kuombea fedha za miradi kutoka kwa wazungu wakidhani itapita tu.

Ndio maana tunasema CCM ni chama cha mashetani.
 
kwani watoto waje kuna kina daimond apo, hao ni wapiga kula tu

Kumbe na hawa ni "watoto wachache wa mitaani"? Unachekesha! CCM sasa mnashindwa kudanganya kwa sababu ushahidi uko wazi. Hata ile video ya wanafunzi kule Arusha inaiumbua Serikali ya mkoa wa Arusha kwa sababu inao ushahidi wa kutosha kuwa aliyesababisha ghasia ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha. Mtudanganye hadi lini? Nasikia Polisi wanaisaka kwa udi na uvumba. Hapo ndipo palipo na kichekesho. Eti wanaisaka! Wanaisaka wapi? Mbona iko kila mahali duniani? Na kama iko kila mahali lakini polisi wetu hawawezi kuipata ni kituko cha mwaka.

SAM_1499.JPG
 
Longo longo kibao za nini kama siyo kujaza maneno yasiyokuwa na maana yoyote. si ungeandika tu hayo maneno matatu kama hapo kwenye RED na ukaeleweka vizuri.

Halafu acha kujipa madaraka ya kuwa msemaji wa wana njombe wengi. usipende kuwaweka watu wote kwenye box la fikra zako. Kama unataka kuwa msemaji wao katika maendeleo, kagombee ubunge 2015 kuliko kujipa matumaini ya hisia ambazo zimejaa kwa watu waliobarikiwa fikra finyu.

Longo longo kibao za nini. Si ungetumia maneno machache tu kama yaliyoko kwenye bluu hapo?
 
Slaa huyu huyu aliyepora mke wa mtu au mwingine
Mtazalisha ID na kuandika off points kibao ili Lumumba wakawalipe lakini hizo Id zenu nyingi nyingi kila mmoja za kusupport pumba zenu hazina uwezo wa kubhadili ukweli kwamba sasa ccm kwa heiri! Wewe umejiandikisha hapa jf tarehe 17 April na umeshaandika mara 116. Pole sana. Ila naomba ujitambue. Ukombozi wa Tanzania utakuweka huru hata wewe. Hautategemea makombo ya mafisadi, ushinde na ukesha hapa jf ili wakupe hela za vocha.Tanzania ikikombolewa, utaishi maisha huru na hta ndugu zako ambao huwezi kuwatupia hivyo vimakombo unavyodondoshewa, nao pia wataishi maisha safi. Tumia uhai wako vizuri. Kumbuka kwamba ukiwatetea wanyonge na kuwahurumia maskini utakuwa unamkopesha Mungu. Hatakuacha. Lakini ukijifanya chizi na kushabikia kwa gharama yoyote umwagaji damu wa maisha ya Watanzania, huku ukijua, ukabadili na kuzalisha IDs ili mwonekane mko wengi, Mungu atawatetea Watanzania bila mchango wako lakini kumbuka una kesi ya kujibu kwa Mungu ambaye uko karibu naye kulikok unavyodhani. Na kwa maisha unayoishi, sidhani hata kama unahakika ya kuruka viunzi vya athari ya ufisadi wa ccm ili angalau uwe na tumaini la kuishi maisha salama kama hao mafisadi unaowatetea katika uovu wao kwa gharama ya damu ya ndugu zako. Jitambue ndugu yangu. Siombi laana hapana. Nakushauri urudi katika utu wako ambao Mungu alikuumba nao, utende mema. Mungu hatakusahau. Unajua kabisa tatizo la utawala mbovu wa ccm linamaliza watanzania kuliko ugonjwa wowote ule hapa nchini. Lakini unajifanya hulioni hilo. Unasaliti ndugu zako kwa ajili ya vimakombo unavyotupiwa? Kama walimkolimba Kolimba, usidhani wewe unathamani kwao kuliko yeye. Wanakutumia kama sabuni na mshumaa. Uwamulikie lakini wewe unateketea. Funguka macho yako, na usipoteze muda kutenda dhambi mbaya hii makusudi. Ungana na Watanzania kuikomboa nchi yetu kutika katika ukoloni wa ccm.
 
Slaa huyu huyu aliyepora mke wa mtu au mwingine

Kaangalie nini maana ya kupora kwenye kamusi ya kiswahili kisha urudi utupe jawabu,fikra za miaka 47 hazitufai kizazi cha digital'CDM'.Ni LAZIMA TUKAMATE MADARAKA YA DOLA BY 2015 KWA NGUVU YA UMMA.MTU YEYOTE ASIYE NA PHYLOSOPHIES ATEGEMEE KAUMIA,LELEMAMA CCM NDIYO HII AMBAYO MWL.J K NYERERE ALIITABIRI IE.HANDSOME AENDE KWENYE DANGULO NA SI IKULU.
 
Back
Top Bottom