Mkutano wa CHADEMA Kasulu mjini wafanyika, lakini...

Mkutano wa CHADEMA Kasulu mjini wafanyika, lakini...

Baada ya dr.slaa kuparamia jukwa ,wanainchi wa kasulu kuka stand bye kwakumsikiliza,gafla mabango yakapandishwa hewani na vurugu kwasana.dr akawaomba wanainchi kutulia ili aweze kusoma mabango ilishindikana nahatimaye watu wasio fahamika wakaanza kurusha mawe,polisi hawakuchewa kurusha mabomu ya machozi,watu wakatoweka eneo la tukio,walipo rudi kuendelea na vurugu dr.slaa jukwaani hayupo tena na wafuasi wake wameondoko.mkutano hakufanyika.kwasasa anaelekea kigoma sipati picha itakuwaje!
.

Kigoma ndo Kambi haswa ya Mh. ZZK bila shaka huko hapatatosha, kilikuwa kituko kweli etianawatuliza watu wenye hasira zao na sijui lile jiwe moja lililo mpata usoni atakuwa na hari gani?. Sasa kama hakuhutubia Kasulu anafikiri Kigoma mjini atasikilizwa?
 
Zitto lazima amwagwe tu, mvimbe mpasuke hatuwezi kuvaa suruali yenye mchwa ndani!!
 
...

.....watu wa Kigoma hawatawaliwi kwa umaarufu wa mtu ndo maana nyomi kama kawa!!!
 
Dr.Slaa Anategemea Kudra za Polisi ili kufanya mkutano Kigoma.
 
Si anazishe kigoma all stars yake? Lazima awepo CDM????
 
Tangu mwanzo wa sakata hili nilisema humu Chadema ina upungufu wa busara ambayo ilihitajika kidogo tuu ya level ya mhitimu ea darasa la saba!. Hii inayotumika sasa ni level ya Chekechea!. Yaani watu wapange kumuua mtu kwa sumu ya panya, kulipo shindikana ikatafutwa sababu ikapatikana, hivyo kabla ya kufuta uanachama kwa maonevu unaamua kuwaendea kwanza watu wake kuwakejeli ukitegemea watakuchekea!.
Pasco

Pasco bana!
Na wewe umetumia busara ya level gani kuandika umbea huu?
 
Ni sahihi kabisa, kama kweli si muhusika wa mabango angewakana hao vijana. Lkn amekaa kimya, that means anafurahia yanayokea.

mbona wao walifurahi walipomvua uongozi na kumbambika maneno ya shombo eti mnafiki
 
Dr.Slaa Anategemea Kudra za Polisi ili kufanya mkutano Kigoma.

Kama jana alishindwa kuhutubia Kasulu, unadhan Kigoma mjini atafanikiwa?, tutarajie majanga zaidi ya yale yaliyotokea jana Kasulu. Jiwe moja lilimpata usoni huko yatakuwa mengi zaidi
 
Si anazishe kigoma all stars yake? Lazima awepo CDM????

habari ndio hiyo msikalie kujipa faraja eti anafanyiwa fujo na CCM_Kigoma sio wanafiki kama KLM , chama chenu mnakipa 5% then maandamano na ubwege mwingine Kigoma-kwanini msiende kujenga huko mlipopata kura chache11
 
Acha kuwa taahira, Tanzania hii sasa hakuna mtu asiyejua kuwa Zitto anatumika wenye busara wanajua na huwa tunasema "time will tell" lakini anguko la Zitto ndo limeshafika atawatumia vijana wasio jitambua kwa mda mfupi sana lakini mwisho watakuja kukumbuka na kujitambua.

Wengi mtakubaliana nami kuwahatma ya ZZK ndani ya CDM ilishafahamika kitambo, na hii imekuwa ikijidhihirisha kutokana na kauli mbalimbali zimezokuwa zikitolewa na viongozi mbalimbali waandamizi ndani ya Chama na kupokelewa kwa ushabiki mkubwa na baadhi ya watendaji ambao kwa namna moja au nyingine Siasa na Misimamo ya ZZK kwao wao imekuwa shida kubwa katika kujitimizia malengo yao binafsi.

Muda wasiku 11 ziliztolewa imefika mahala watu wameona ni kiini macho na unafiki kwani muda huo ulilenga kukiwezezesha Chama zaidi kupima upepo wa wanachama kufuatia azma hiyo ambayo iliyolengwa kutekelezwa hivi karibuni na sio kumuwezesha ZZK kutolea ufafanuzi hoja zilizowasilishwa kwake.

kumekuwa na maswali mengi pia kwanini SLAA kalazimisha kufanyika kwa ziara ya kile alichokiita ujenzi waChama kwa mikoa iliyoanishwa na Kurugenzi ya Habari ya CDM na kwanini pamoja na tahadhari nyingi amezokuwa akipewa kutoka kwa uongozi wa Chama Mikoa, hasa Mkoawa Kigoma bado ameendelea kung'ang'aniza uwepo wa ziara hiyo? swali ndilo lililonisukuma hasa kuanzisha uzi huu kwani sehemu nyingi lilipoulizwa Swali hili na maswali mengine mengi yenye kufanana na hili nimeona yakijibiwa kiujanjaunja.

Ukweli ni kwamba SLAA kaagizwa kwenda Kigoma kutest zari, mfano wa yule mpelelezi wa kikoloni, watu waHistoria mtanikumbusha nadhami alikuwa akiitwa (Karl Peter) kuona mwitikio wa watu wa Kigoma ni vipi wanaupokea uamuzi wa CCya CDM kumvua uongozi ZZK na suala la kumvua uanachama lililopangwa kutekelezwa hivi karibuni, hii inatokana na ukweli kwamba CDM ilijijengea wanachama waaminifu na waadilifu sana mkoani Kigoma kupitia ZZK tofauti na sehemu nyinginezo ambapo masilahi binafsi yamekuwa mbele zaidi. Mfano katika Uchaguzi wa mwaka 2010 SLAA alipata 40% KIGOMA ikilinganishwa na Kilimanjaro ambapo alipapata 5% pamoja na kwamba ndipo chama hicho kilipoasisiwa( HAPA NDIPO UTAONA ILE DHANA YA SHAMBA KUWA MBALI NA NYUMBANI ilipotekelezwa kwa vitendo na wana Kilimanjaro)

Wana Kigoma kwa umoja wetu tumempa ujumbe mzuri sana SLAA kwamba sisi sio WAJINGA kama wamevyokuwa wakijidanganya, isipokuwa watu wa Kigoma ni WAAMINIFU na WAADILIFU na hilo la uaminifu ndilo limelokuwa likiwasumbua sana dhidi ya ZZK. Habari ya kuwa tunakipenda CHAMA na sio MTU tumekwambia kwa vitendo kuwa NO ZITTO =NO CHADEMA KIGOMA, wanachotufanyia CDM ni DHIHAKA yakutupima uelewa wetu watu wa KIGOMA. SLAA (a.k. a Karl Peter) nenda kawaambie waliokutuma kuwa hivvyo ndivyo tulivyo watu wa KIGOMA na wala sio CCM wala nini kama mmevyokuwa mkijifariji, mimi mwenyewe nilieandika uzi huu ni mwanachama wa CDM-kazi kwenu, mkitaka mfukuzeni na mkitaka fanyeni mnavyotaka.

Lakini kadhia hii imetufungua macho Watanzania wengi juu ya Unafiki wenu. Kwanini Lema/ Chama mumchukie ZZK kwa kukataa posho? mumuchukie kutaka kutekelezwa kwa dhana ya Demokrasia kwa vitendo kwa kuendesha chaguzi ndani ya Chama kwa uwazi, matumizi ya fedha za Watanzania kwa uwazi(MAMBO AMBAYO YANGESAIDIA KUKITOFAUTISHA CHAMA HIKI NA VILE VILIVYOONEKANAKUUKUMBATIA UFISADI?) Acheni hizo, watu wanajitambuasana siku hizi kuliko mnavyokuwa mkidhani, tumefika mahala KURUGENZI YA HABARIKUWEKA PICHA ZA UONGO na SLAA kugonga LIKE , Kweli huku ndiko tulipotaka Chamakifike kweli-mmekuwa tayari kukiua Chama kuliko ninyi kukosa masilahi yenukweli? Kweli akina ARFI, DR . KITILA,Prof BAREGU na wengine wengi wote hawjitambui na ni wazandiki na MSIGWA, LEMA,LISSU ndio wenye machungu na wanaojitambua? Ndugu zangu hatuwezi kuiendelezanchi hii kwa misingi hiyo
 
Kigoma ndo Kambi haswa ya Mh. ZZK bila shaka huko hapatatosha, kilikuwa kituko kweli etianawatuliza watu wenye hasira zao na sijui lile jiwe moja lililo mpata usoni atakuwa na hari gani?. Sasa kama hakuhutubia Kasulu anafikiri Kigoma mjini atasikilizwa?

Jamani acheni uongo na mwogopeni Mungu!! Hivi mnadanganya kwa faida gani? Ili iweje? Dr. Slaa kahutubia hadi kamaliza, Heche akahutubia hadi akamaliza, baadaye ndiyo vijana wanajitokeza na mabango na kuanza kurusha mawe. Polisi waliwadhibiti na mwenyekiti wa wilaya akafunga mkutano. Sasa huo uongo mnaopamba wa nini?
 
zito wa sasa sio yule wa zaamani ...aende zake anzishe chake kama wengine.
mumfuate si anawafuasi wengi tabu ipo wapi ?
 
sasa huo ni ujinga au ushamba,siasa za kurushiana mawe yanamuongezea nini zitto kama sio Kumpunguzia heshima,zitto ongea na mdogo wako aache kuratibu the type of hooliganism we are experiencing...umekuwa ukipreach kwamba wewe ni muumini wa siasa safi,sasa imekuaje leo wapambe wako wanakuaribia sifa na wewe usemi kitu
 
Hamuwezi kuonyesha ubabe wenu kwenye chama ambacho kilianzishwa na watz na chama ambacho mulikikuta na ni chama ambacho kimemutangaza Zitto mpaka amefika hapo alipo.Kama munamuona Zitto ni zaidi ya CHADEMA na ana uwezo kuliko CHADEMA iliyo mukuza ni vema zaidi mukamushauri kuanzisha chama chake na wafuasi wake mukamfuata huko kuliko kung'ang'ania kwenye chama ambacho munaamini kuwa hakimutendei haki.CHADEMA ni chama cha wtz wanakigoma ni wtz kwa hiyo CHADEMA itaendelea kuwepo kigoma kwani ni sehemu ya Tz.
 
Back
Top Bottom