Mkutano wa CCM kuzuiwa na Polisi?

Mkutano wa CCM kuzuiwa na Polisi?

Kweli mku mpaka sasa jeshi la polisi halina taarifa kuwa kutakuwa na mkutano mkuu wa ccm hivyo mkutano utafanyika kama kawaida kwani intelijensia yao haijapata fununu za mkutano huo vinginevyo ungesha sikia makaripio muda huu wa kuwaambia watakao kaidi watakabiliana na vyombo vya dola. Tena huo ndio utakuwa mkutano mkubwa kabisa kuliko hata hii waliyoisambaratisha kwani wa kwao unahudhuriwa na viongozi au wajumbe kutokana kila kona ya nchi. Tusubiri tusikie utetezi wa polisi wa kwanini mkutano huo ni halali.
Hii nchi ni zaidi ya kina museven
 
Watasema hawakuwa na taarifa za huo mkutano kama yale maandamano ya Ccm Mwanza RPC alisema hana taarifa kama walifanya maandamano.
Ila kwa UKAWA huwa inajulikana mwezi kabla.
 
Kweli jeshi letu sikivu na la kizalendo linalo hakikisha demokrasia inatamalaki hapa nchini watazuia huo mkutano wa ccm kutunza amani ambayo intelejensia yao inaonyesha inaweza potea kwa shughuli za kisiasa ...
mkuu kwan CCM ni chama cha siasa Tanzania? hiki cdhani kma ni chama!!!
 
Nitakwenda Mkuu wala usijali, Jibu kwanza hoja!!
Kwa ufupi hawana huo ubavu wa kuzuia huo Mkutano wa CCM. Hata wewe unajua hivyo na uelewe Mkutano huo ndio Amiri Jeshi anakwenda kabidhiwa Chama
 
Nashauri vyama vya upinzani vifanye mikusanyiko siku hiyo hiyo ya mkutano wa CCM, tena ikibidi ukumbi uliopo karibu na wa CCM
 
Ukiwa mnatia huruma sana, Polisi watatulinda kuhakikisha Mkutano wetu unaanza salama na kuisha salama.
 
Mikutano ya vyama vya siasa nchini na maandamano vyote vimepigwa marufuku mpaka hapo hali ya usalama nchini itakapotengamaa, lakini cha kushangaza maandamano ya CCM RUKHSA na mikutano ya CCM ni RUKHSA kwao hawa CCM hali ya usalama nchini ni shwari kabisa, ila hali ya usalama haijatengemaa inapokuja kwenye vyama vya UKAWA.
Double standard......polisi wanajua hata uminye haki za watanzania kiasi gani wataishia kunung'unika tu mioyoni pasi na kuchukua hatua zozote.
 
Tunalipenda Jeshi letu sikivu, Jeshi lenye Nidhamu na hivyo tunaliomba liendelee na msimamo wake ule ule wa kuzuia mikutano ya vyama vya Siasa kama ilivyofanya kwa Chadema na ACT Wazalendo.

Tarehe 23 Julai 2016 CCM nao wametangaza Mkutano wao wa kumkabidhi Mwenyekiti chama, huu ni Mkutano wa kisiasa, ni Mkutano ambao hauna tofauti na ule wa ACT wa ndani ya Ukumbi au ule wa Sherehe za CHASO huko Dodoma Leo. Tunaamini Jeshi letu pendwa litapeleka Magari ya Washa Washa kwenda kuzuia Mkutano ule. Naam ni Mkutano wa Siasa!

Asante Jeshi letu pendwa....

Mazingira ya mkutano wa CCM huko Dodoma yakoje, na mazingira ya mkurano wa ACT Wazalendo na CHASO yakoje? Lengo la mkutano wa CCM ni lipi? na lengo la mkutano wa CHASO na ACT Wazalendo lilikuwa lipi?
 
Wanazalisha mengu mbaya sana ambayo siyo nzuri bora wangewa acha waendeleye ma mahafali yao maana nafsi za wanadamu huwabadilishwa kutokana na matendo ya wanadamu wenye uwezo wa kufanya uonevu wadhaifu wakishaoteshewa dhuluma ndani ya nafsi zao huleta madhara kwa jamii ombi langu kwa watawala wasipende kutumia nguvu sana sehmu ambayo haina ulazima maana wanaweza otesha mbegu ya chuki ambayo ni mbaya san kwa jamii
 
hatutaki mikutano ya kisiasa..
kama wa mahafali tu ya wanafunzi tumevamia na risasi za moto mkononi basi na huo tunapiga marufuku na tutauzuia kwa mizinga...
kudadadek..
wakosoe wao wasikosolewe wao..
watende wao wasitende wenzao..
hapa njaa tu
hapa mfumuko wa bei tu
hapa CCM tu UPINZANI marufuku hata kuongea..
 
Back
Top Bottom