yussufhajj
Member
- Mar 24, 2016
- 27
- 8
Mkutano wa berlin ulifanyika siku ya jumapili 15/ November /1884 hadi febuary 1885.
Mkutano huu ulijumuisha wajumbe wa nchi 14 za ulaya na wajumbe kutoka USA.
Mkutano huu uliitishwa na aliekua kansela wa ujerumani wa wakati huo chncl Olto von Bismark na ulifanyika katika jiji la berlin nchini Ujerumani
MALENGO YA MKUTANO WA BERLIN :-
1) Kuligawa bara la Afrika kwa njia ya amani.
2) kuzungumzia mgogoro wa eneo la congo basin na niger basin.
3) kupanga mikakati ya kuhakikisha mataifa ya ulaya yatakayo kua na koloni lake afrika yasichukuliwe na mataifa mengine.
4) kujadili maeneo ambayo mataifa ya ulaya hawana makoloni.
5) kupanga mikakati ya kuondosha biashara ya utumwa.
MAAZIMIO YA MKUTANO WA BERLIN
1) Mataifa yote ya ulaya yaliohudhuria mkutano walimtambua mfalme leopad II wa ubelgiji kuwa mmiliki halali wa kongo basin.
2) Taifa lolote la ulaya litakalo chukua koloni Afrika lazima litoe taarifa kwa wengine.
3) Taifa lolote la ulaya litakalo wahi kuchukua koloni katika mwambao wa bahari linaruhusiwa kuingia ndani zaidi ya pande la ardhi.
4) Mataifa yote ya ulaya yatoe sapoti katika kuondosha biashara ya utumwa.
5) Biashara ya utumwa ilitangazwa rasmi kuwa ni biashara haramu .
6) Makundi ya watu wa ulaya watakao kwenda kulistaarabisha bara la Afrika yapatiwe ulinzi bila ya kujali utaifa.
7) Eneo lote la mto niger litakua ni eneo huru la kibiashara.
8) Taifa lolote la ulaya litakalo ingia mikataba na viongozi wa Afrika mikataba hio itatambulika.