Viongozi wa Ulaya wanajadili bajeti ya muda mrefu

Viongozi wa Ulaya wanajadili bajeti ya muda mrefu

carbohydates

Member
Joined
Oct 13, 2026
Posts
23
Reaction score
47
Viongozi wa Umoja wa Ulaya wanajadiliana kuhusu bajeti ya muda mrefu katika mkutano wa kilele mjini Brussels, kukiwa na shinikizo la kufikia makubaliano kabla ya uchaguzi wa Ufaransa uliopangiwa kufanyika mwaka ujao.

Katika mkutano huo wa kilele, Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa aliwataka viongozi wenzake wa nchi wanachama kufikia makubaliano kuhusu bajeti mpya ya Umoja wa Ulaya kabla ya Krismasi mwaka huu.

Macron alionya kuwa mazungumzo hayo yanaweza kuwa magumu zaidi kuanzia mwanzoni mwa mwaka ujao kutokana na chaguzi muhimu zinazotarajiwa kufanyika katika nchi kadhaa za Ulaya, hususani nchini mwake ambako chama cha mrengo wa kulia kinachoongozwa na Marine Le Pen kinaonekana kupata uungwaji mkono mkubwa.

Bajeti hiyo yenye thamani ya karibu euro trilioni mbili itatumika kuongoza matumizi ya Umoja wa Ulaya kati ya mwaka 2028 hadi 2034, kugharamia sekta mbalimbali ikiwemo kilimo, ulinzi, ushindani wa kiuchumi, maendeleo ya kikanda na sera za uhamiaji.

Hata hivyo, mkutano huu unakumbwa na tafauti kubwa za msimamo. Ujerumani na mataifa yanayojulikana kama "Frugals", zikiwemo Uholanzi na Uswidi, yanataka kupunguzwa kwa mamia ya mabilioni ya euro kwenye bajeti hiyo.

Lakini Ufaransa inapinga kupunguzwa kwa kiwango kikubwa cha matumizi na ikisisitiza kuwa Umoja wa Ulaya unahitaji fedha zaidi kukabiliana na changamoto za sasa za kiuchumi, kiusalama na kisiasa.

Nchi nyingine zinazojiita "Marafiki wa Mshikamano" zinataka fedha zaidi ziende katika kilimo na maendeleo ya maeneo mbalimbali ya Ulaya.

Kutokana na tofauti hizo, Kansela wa Ujerumani Friedrich Merz amesema mazungumzo hayo yatakuwa magumu sana na bado nchi wanachama ziko mbali kufikia mwafaka.
Chanzo : Dw swahili

Macron.webp

​
 
Back
Top Bottom