Mkutano soko kuu Mtwara- muendelezo wa gesi.

Mkutano soko kuu Mtwara- muendelezo wa gesi.

Ni upuuzi, hawajui adui yao nani..

Ni nani unaweza kutinongoneza? Maana huyo ndiye mwakilishi wao bungeni ila Raisi kampenda zaidi kampa majukumu mengine, sasa kwanini wakilala mika mwakilishi hawatendei haki wewe unasema ni upuzii?
 
Ni nani unaweza kutinongoneza? Maana huyo ndiye mwakilishi wao bungeni ila Raisi kampenda zaidi kampa majukumu mengine, sasa kwanini wakilala mika mwakilishi hawatendei haki wewe unasema ni upuzii?

Ni madai ya kipuuzi ambayo Ghasia hajayaunga mkono, usifikiri majority haikosei, isue ya gas kupatikana mtwara wasiione hiyo ndo loophole ya kuexercise ubinafsi wao.
 
...tutaanza kuwachunguza uraia wa hao wamakonde! isije ikawa watu wa nchumbiji ndo wanatusumbua! halafu nasikia PanAfrica Energy wana mkono wao pia!... gesi itatoka tu! hao ngoja wapumue pumue maana midomo ni yao Mungu kawapa!
:target::target::target:
mwaka huu ndo mtajua kama wamakonde au wamawiha!
 
Hapa kuna mkutano agenda kuu ni kuhus kusafirisha gesi kwenda dar es salaam hapa wanasema kikwete amechokoza moto hawata rudi nyuma. wanasema gesi haitoki liwalo na liwe. nawasilisha. na zaidi wanamlaani hawa ghasia wanamwita msaliti.

Baada ya Almas, Dhahabu na Tanzanite kutuachia mashimo sasa ni zamu ya gas kusambaza laana. Bomba linafungwa kutoka Mtwara hadi Dar kuunganisha na gesi za Zanzibar, Mkuranga nk. kuchota kila kitu. Ni series ya Natural Resources Curse. Laana kali ya rasilimali. Kuna wakati huwa najuta sana hadi nalia. Why can't we even think a little bit? Yaani kweli viongozi wa CCM na Serikalli wameishiwa huruma kiasi hiki? Come on Nape Nnauye
 
Last edited by a moderator:
wanasema mkuu wa mkoa hawamtaki walimpa siku 14 sasa zimebaki siku 5 asipoondoka maanadamano ya kumshinikiza kuondoka. Du mvua inaharibu mkutano hapa lakin hotuba zinaendelea.

mkuu wa mkoa ni gamba, wangesema moja kwa moja hawataki magamba
 
Kipindi kile walikua na kinjekitile ngwale..sasa hivi wana nani? Walikua na madai ya msingi sasa hivi madai yao ni nini? Hawa watu wa mtwara wanalishwa maneno hawajui wanachodai
Hoja yao ni gesi ianzie kutumika Mtwara kwanza kabla ya kupelekwa popote ndani au nje ya nchi.

Wanauliza kwanini ichimbwe Mtwara halafu ipelekwe Dar/Bagamoyo kwanza na sio kubaki Mtwara kwanza?
 
Kipindi kile walikua na kinjekitile ngwale..sasa hivi wana nani? Walikua na madai ya msingi sasa hivi madai yao ni nini? Hawa watu wa mtwara wanalishwa maneno hawajui wanachodai

yupo THE BIG SHOW
 
Last edited by a moderator:
hawa watu wana hoja ya kudai maendeleo .... Serikali iwe makini sana katika kushughulikia haya madai maana upande wa pili nafikiri kuna uchochezi pia, serikali iangalie sana hiyo kampuni ya pan african energy ....sehemu nyingi duniani zenye machafuko ukichunguza utakuta ni wenyeji wanatoana macho kwa ufadhili wa wawekezaji wa magharibi
 
hawa ghasia ana wakati mgumu sana. mzungumzaji mmoja anasema ametembea kata zote za mtwara vijijini wananchi hawamtaki hawa ghasia.

Huyu Hawa Ghasia nakumbuka mwaka jana (2012) alitunukiwa na taasisi fulani (nimeisahau jina) heshima ya kuwa mfano bora wa mwanamke wa kiislamu huko serikalini. Kwa "heshima" hiyo, nilitegemea angekuwa pia na utumishi uliotukuka kwa wapiga kura wake lakini inaonekana kuwa kinyume.
 
Hao viongozi wa huo mkutano wakae chonjo watakamatwa na watawaulimboka woote hao wanaojifanya vinara wa mikutano ya gesi!
 
Hata mbuyu ulianza kama mchicha wadharauni tu mtaona mwisho wake
 
Duh, haya mambo si ya kuyapuuzia na kuleta siasa za kibabe, wajiulize nini kilitokea Nigeria!
 
Wanaoratibu mikutano hii wawe wazi kwa Wananchi,haiwezeakani gas isiende Dar ila la kupigania hapa ni kuwa kabla haijaenda angalau serikali ihamasishe wawekezaji walete viwanda Mtwara,Lindi.
Angalia Kilwa,gas imekwenda Dar lakini la maana walilopata ni kuwekewa umeme toka kituo kidogo cha Somanga.
Kwanini pasingejengwa hata kiwanda kidogo cha cement na kuboresha bandari.
Serikali itoe vivutio kwa wawekezaji ili kusini pawe na maendeleo.

kwenye red, ndo maana wanataka Processing ifanyike mtwara/Lindi Ili investors wavutiwe kujenga karibu na resources!!! nadhani hiyo ndo mojawapo ya madai ya msingi.......jst thinking loud
 
Niger Delta hiyooo MASKINI HANA CHA KUPOTEZA
 
Kwa mtazamo wangu, ambao sio wa kisomi, ni kwamba serikali iachane na "one track mind". Kwa wakati tulionao ni vema tukubaliane kwa hoja moja ya msingi: serikali ni ya wananchi. Kwa mantiki hiyo, ni wajibu wa serikali kuweka bayana imeyafikiaje maamuzi yake na siyo kutoa majibu ya jumla jumla. Haieleweki. Matokeo yake ni matumizi ya mabavu ili kuonesha au kuhalalisha maamuzi yake. Tulipofikia sasa ni lazima serikali ikubali kwamba mwajiri wake haridhiki na utendaji wake. Hoja ijibiwe kwa hoja na si vinginevyo. Majanga kwa serikali yamezidi na kulipuuzia hili ni sawa na kutia kidole kwenye feni linalozunguka mwendo kasi. Amini usiamini watu watasahau mazuri yote kwa mwenendo huu wa kuwadharau walio wengi eti "sisi tunajua tunafanya nini" waache wapige kelele "watanyamaza tu, kwa njia moja au nyingine". Sauti ya "sasa basi" inapopaazwa, hapatatosha.
 
  • Thanks
Reactions: ral

Huyu Hawa Ghasia nakumbuka mwaka jana (2012) alitunukiwa na taasisi fulani (nimeisahau jina) heshima ya kuwa mfano bora wa mwanamke wa kiislamu huko serikalini. Kwa "heshima" hiyo, nilitegemea angekuwa pia na utumishi uliotukuka kwa wapiga kura wake lakini inaonekana kuwa kinyume.

Hiyo heshima alipewa kwaajili ya kuvaa hijabu muda wote.
Mavazi sio matendo ndugu.
 
Back
Top Bottom