BEFORE KUFIKA HAPA NILIPO (VIMBWANGA VYA ULINZI USIKU)
Bhanaaa hiiii dunia ina wababe sanaaa, ukiwa mjanja katika harakati za maisha biashara, shuleni, nguvu , kipesa , mamlaka n.k ila kuna wajanja na wababe sekta zingine.
Katika purukushani na hustling, niliamshwa sehemu katika maswala yetu haya ya kazi.
Kama ilivyo ada, muda wa silaha kuchukua ukafika, nikasonga eneo la tukio na kuchukua mzigo full loded (njugu 30).
Tukaanza kuimalisha ulinzi wa mipaka ya kituo na mazingira yanayo zunguka.
Ilifika usiku kila mtu alikuwa hana amani siku hiyo, maana zilisikika sauti zinatokea njia ya moja kwa moja ( eneo makini). Hakuna mti wala chochote katika njia hiyo, lakini wazungumzaji hawaonekani.
Tulikuwa gizani muda wote, hapo tunaweza kuona vitu kwa clear kabisa na watu hawawezi kutuona kutokana na mavazi n.k
Lakini hapo tulifeli kuona watu hao, huku wakiongea kwa kujitutumua kuwa wanakuja upande wetu kutuonyesha watala wa usiku ni wakina nani.
Baada ya muda kidogo, wenzangu naona wakalala wote, lakini mimi usingizi hautaki kuja, amani hakuna hata nusu.
Sauti zile zilipo karibia usawa wa gizani zilikata . Nilichoamua, nikasema hiii ni game ngoja tuicheze, zikisikika nitazijibu nione mwisho wake.
(Baada ya dk kama 15)...Zilisikika, wenzangu nawashtua hawashtuki, eti kamandaaaa leo tuone ukamanda wako (hiii ilikuwa sauti kike ikisema na sonyoo hatari).
Nikasema hawa hawajaja na lengo la kuniua ila kucheza na akili yangu tu, ngoja twende sawa, nikaenda kwenye taaa.
Nikatukana, nikasema ukitaka kuona ukamanda jitokezeni nirengeshe kilengeo , ebwanaaa. Dk 5 nyingi nilianza ona mwili unaisha nguvu hatari nikakaaa chini, huku kwa mbali naona mtu anahangaika kuvuta silaha yanguu , halafu anacheka, image yake niliona kwa mbali sana , tulikutana asubuh niliona mtu anakwepa nilihisi yule yule.
(Inshort ni hiii nilisumbuka sana night)
USIKU HUUU WAO NDIO WALISANDA SANA.
Hapa tukiwa eneo la ulinzi, tuliwahi kamaat mara mbili watu tuliojiaminisha kuwa washirikina.
1. Tukiw ulinzi sehemu ya ghala la silaha, mida usiku mnene, tuliona kitu kinatua uwanjani, na mtu anatoka na mizigo yake, haeleweki, toa usalama, koki silaha tukamweka chini ya ulinzi.
Alikuwa kapigwa butwaaa muda wote huyu mama.
Kumuhoji, ni nani ,katoka wapi, anafanya nini pale.
Maelezo mengi aliyatoa kwa doso, ila inshort alikuwa anatembea kukusanya damu kwa watu walio katika vituo vya ulinzi na sehemu zingine.
Huyu alikula kazi usiku kucha hadi asubuhi.
HIZI KAZI ZINA RISK SANA.
2. Katika ulinzi, eneo limezungukwa na mageti na fensi sehemu nyingi, lakini, tulishangaaa kuona maza mmoja anaishia kwa mbaali anaondoka kutoka katika zizi la ng'ombe.
Kuhoji anasema katoka hospital kapita wapi hasemi, mavazi hayasomeki.
After kumlish mzigo alisema anatembelea sehemu zenye mifugo anachukua maziwa , anafanyaga hivi.......
Nitakuja na kufeli kwangu, na majanga yaliyo nikuta kuyaona kwa wenzangu..........