Mkusanyiko wa matukio ambayo yameshawahi nitokea

Mkusanyiko wa matukio ambayo yameshawahi nitokea

Duu mkuu umejitengenezea chance.... Ukitaka..... Unamwita tu hana kipingamizi... Tena gharama kwake.... Hahahahaha.

Lkn mkuu uwe na kumbukumbu maana hata hiyo isha ntokea kuna baadh ya watu hata askar wakiniona wanajua mimi n mwenzao lumbe hataguu pande sijui.... So take care
Hahha kuwa makini, mkuuu
 
KWA MARA YA KWANZA USO KWA USO NA CHATU.

Kipindi kidogo kama 2015 hivi, nilikuwa asigned duty fulani hivi ambayo ilikuwa far kidgo na mji mbali sana, mikoa yenye pori kidogo na mambo ya uswahili sana

(plus ushirikina hili nitakuja lihadithia).

Reason ya kupelekwa huko ni kama adhabu ya tukio fulani nililofanya na nalijutia hadi leo.

Task niliyopewa kwa mazingira ya kule ilikuwa ngumu kidgo, ila ikabidi nifanye.

Nafika siku ya kwanza sina mwenyeji wala rafiki, ila nilipokelea na mdada mmoja alikuwa mkarimu na kuweza kupata makazi kwake, next rooom anakaa yeye.

Sasa ile sehemu ukianchilia mbali na duty nilizo kuwa nafanya, mazingira yale yalikuwa na nyoka wengi sana, esp CHATU.

Kupunguza story ndefu, kuna siku huyu sist alipeleka wanafunz shamba ( maana ni ticha na shule ipo nyuma tu hapo)

Madogo wameanza kulima, ghafla chatu akaonekana akaingia kwenye chaka moja dogo, wanafunzi wanapiga kelele, wakaja walimu wa kiume wakaonyeshw dude ndio linaendelea kuzama., ila hawakuwa na reaction yeyote.

Sasa huyu sista akasema tumuue huyu chatu, majamaa wakasema tumulishie mawe akimbie, lakini hapa kuna wanafunzi, makazi ya watu na hostel, atarudi na kuleta madhara siku moja.

Muda huo chatu bado kaacha sehemu ya mkia nje, nikasikia kelele zimezid nikatoka geto, yule sist akasema afadhari umetoka KAMANDA (sikujua reason ya kuniita hivi) akanambia njooo tusaidie.

Nikaenda waka ni brief, kuangalia mkia, bonge la dude , nikaligusa na jiwe likazama kwenye lichaka.

Baada kuona majamaa waoga, nikasema nyote kaeni huko, mchokonoen aje kwangu , au mim nimfulumushe aje kwenu mumuue. Waka chagua option ya kwanza.

Nikaomba jembe , wakamfulumusha, kitu kinakuja wangu wangu nilipo kuwepo. Nikiwaza hapa nikikimbia itakuwa story na dharau

(advantage kubwa chatu hana Sumu, mate harushi)
Pia nikasema hawezi nimeza huyu namuona huyu, hapa nitakwepa ukaribu na contact asije nidandia wajinga wakanikimbia hawa.

So nikamruhusu aje huku, namkata na jembe kichwani na kuhama position fasta , ana muscle ngumu sana, but nilipo piga mapigo 4 ya fasta, na jembe lile butu, akabadili huelekeo kurudi kwa wengine.

Baada ya kunipa mgongo, nikamaliza mchezo , hapo nilichukua point 3, za msingi pale kijijina kwa wazee na mabinti.

Ila ukijifanya shujaaa inaweza kukucost wakati mwengine, maana mistake ndogo nisinge kuwa hapa naandika...

Ila kutokana na kazi ya kule , na ku brow my cover, na matukio kama haya ya Chatu nilipata maadui wa chini chini hapo ikaja michezo ya USIKU

( nita wagusia kidogo ila ambaye haamini huwepo wa hayo mambo , akiyaona atabadili mawazo )
 
Aisee kamanda andika kitamu
 
Ha ha ha ha new year eve nzur sana kwa mikasa kama hii
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom