FIRST TIME NAPATA HOFU...
Kutokana na ku mess up na watu na kupangiw Duty huku, Nilia jiapia kuwa sitakuja ku date na binti yeyote.
Nikawa na train mind yangu, nijione fate inanitaka nitumikie taifa, kama wafanyavyo watawa wao wanawezaje, mimi nishindwe??
( mimi ni mkristo , lakini baada ya kipindi fulan,nikaja kuona kwa watawa kuna mengi nyuma ya pazia, hila hii sio ishu).
Nikawa cool, tukio la chatu, likanipa grade flan pale bush, vibinti shazi , salam na kujichekesha sana...
Kuna siku nilikuwa sina mishe wala nini, nimetoka kufatilia INFO fulani, sehemu fulani, nikiwa ndani ya Rain buti , Cape, na traki.
Karibu na ninapo kaa, nika mkuta maza mtu mzima kabisa (niseme ni mbibi) analima, nika msabahi, na kumuomba kuzungumza nae, huku nikijenga mazingira rahisi kufanya zangu.
Alinihadithia kuhusu yeye kulima, maan wanaye wanapuyanga tu, kuuza mkaa na hawampi sapoti kivile.
Nikashika jembe, nimsaidie, piga jembe kama masaaa matatu, kisha nikaaga baada ya shukrani.
Kufika geto, nimechafuka, nika mkuta yule ticha nje na rafiki, zake, akaanza kutoa statement s like tuna kitu beyond urafiki then akasema nimpatie nguo zile afue.
(Sikutaka kumdisapoint mbele ya wenzie, nikaitikia)....Kifupi binti alijenga mazoea, yakuleta menu, kuja kupiga story mida mikali ya usiku. She was Hot, anaita, but sikutaka vunja mipango niliyo jiwekea.
Basi, kesho yake nikaenda asubuhi, kumsaidia yule bibi kama nilivyo muhaidi, kumalizia. Mida ya saa nne au saa tano hivi baada ya mitikasi nikazuka nikamaliza.
Bana, huyu bi maza aliletewa msosi na binti yake ni mzuri aiseee, binti alikuwa anafanya kazi mjini na kule alikuwa likizo
(Tuka jikuta tunaanza ukaribu na huyu mdada )
HAPA NDIO HOFU ILIPO ANZA TOKEA
Binti alinielekeza kwao, nikanza kwenda usiku mida ya saa tatu, niwe kule. Nilifika namtext nazama room kwake, kutembea usiku kule yataka moyo sana, kuna harakati nyingi za upande wa pili wa dunia. Hila kila nilipo taka kurudi, binti aliniambia nichume jani la mhogo, au alinipatia tawi la mbaazi kuwa then nilitupe nikifika tu geto.
Sikuwa najua lengo lake haswa, ila kuna day nikalitupilia njiani
Kwenye hii njia, kuna sehem kuna bonde lefu kwa umbali, then upande kuna mto, nikuwa nikifika hapo, nywele zinasimama hatari.
Hasa siku hiyo, nikakutan moto wa kuni umewashwa kama wa watu wanapokuwa mbugani, then kuna mtu kavaaa nguo nyeusi anauzunguka ule moto, nikagundua ni jinsia KE.
Hapa nikakumbuka ABC , nijifanye sijamuona kabisa ingawa ilikuwa karibu. Alinikata jicho hilo, then mimacho yake ilikuwa kama ina waka hivi kutokana na reflection ya mwanga.
Nikasonga mbele, washa tochi, ina mulika hatua kama ishirini mbele, lakini huwezi amini, nikashnagaa mbele mtu yupo karibu na uso wangu.
Mavazi yake ; Alikuwa kavaa jinsi chakavu, mchafu. Kabeba ndoo mbili, sikujua zina nini, hana ndala, wala taa yeyote .
Hatukusemeshana, but moyo ulipiga sana. Nikageuka kumcheki, siku muona kabisa. Nikasema mwanaume sikimbiii ngoja nisonge front. Kugeuke niendeleee na safari, naona bonge la paka jeusi, macho yanawaka, pumzi kama zinatoa moshi hivi.
Lile paka likaanza kunifata kutaka kuni atack, nikaanza kumsomesha namba za viatu, nduki nilitoka, lipo nyumaaaa, kila nikigeuka, naliona linazidi kuwa kubwa.
Wakati nageuka, nilijikwaaa kwenye mzizi wa mti, chini nilienda, paka anakuja wangu wangu. Nikachomoa kisu kidogo nilikifunga mguuni ,huku nikiwa narudi kwa kusota na mgongo, siwezi kufa nikiwa nimepiga magoti.
Khaa, nashangaaa paka, kasimama ghafla na kugeuza, nikajiuliza huyu kiumbe wa ajabu kaogopa nini, kugeuka namuona yule binti niliye toka kwao.
Hapa ndiyo mbilinge zilianza aiseee, kafikaje pale??, wew unge fanyaje?? Binti laini umetoka kumwacha kwao umbali kadhaa, unakimbizwa na lipaka la ajabu then lipaka laonekana linamuogopa binti yule...Ungeweza lala usiku? Binti alifanyaje baada ya hayo, anajieleza kwangu....