Mkurugenzi wa TBC Bw. Tido Mhando umechemka BIG TIME!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mkurugenzi wa TBC Bw. Tido Mhando umechemka BIG TIME!!

Discussion in 'Sports' started by Brooklyn, Jun 7, 2010.

 1. Brooklyn

  Brooklyn JF-Expert Member

  #1
  Jun 7, 2010
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 1,453
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Kwa masikitiko makubwa na kwa mara ya kwanza kwa zaidi ya miaka 16, watanzania wengi (hasa walalahoi) hawatopata nafasi ya kuangalia michuano ya fainali za Kombe la Dunia linalotarajiwa kuanza Ijumaa hii nchini Afrika Kusini.

  Hii ni kutokana na uongozi wa TBC kuwatangazia watanzania kwamba TBC1, inayoonekana karibu nchi nzima kwa antena za kawaida itakuwa ikikatisha kurusha matangazo ya Kombe la Dunia ili kurusha matangazo ya moja kwa moja ya vikao vya Bunge linalotarajiwa kuanza siku chache zijazo mjini Dodoma.

  Taarifa hiyo imezidi kueleza kwamba ni kwa wale tu watakaokuwa na ving'amuzi vya StarMedia vinavyouzwa katika mikoa mitatu tu yaani Dar, Dodoma na Mwanza ndio watabahatika kuangalia michuano hiyo kupitia channel mpya inayoanzishwa na TBC ya TBC2 itakayopatikana kupitia king'amuzi hicho tu.

  Hili ni pigo kubwa kwa watanzania wengi ambao hawana uwezo wa kununua ving'amuzi hivyo vinavyouzwa kwa bei ya kati ya Tsh. 75,000 hadi Tsh. 90,000 na malipo ya kila mwezi ya Tsh. 9,000.

  Ingawa uongozi wa TBC umepewa haki ya kurusha matangazo ya Kombe la Dunia bure na FIFA, swali je kwa nini wao wawauzie huduma hii watanzania ambavyo ni kinyume na matakwa ya FIFA inayowataka kurusha matangazo hayo free of charge????

  Je kwa nini warushe matangazo ya mpira katika channel ambayo haina coverage kubwa nchini (TBC2) badala ya TBC1 yenye coverage kubwa?

  Kwa nini waligombea kurusha matangazo ya Kombe la Dunia wakati walijua michuano hiyo ingeingiliana na vikao vya bunge? Si wangeacha michuano hiyo irushwe na ITV, Star TV au hata Channel 10?

  Naamini huu unaweza ukawa ni mradi mwingine wa kifisadi unaotaka kuwalazimisha watanzania wanunua ving'amuzi vya StarMedia kwa nguvu!!

  Binafsi naona ni bora TBC wangerusha michuano ya Kombe la Dunia kwenye TBC1 mechi zote bila kukatizwa katizwa na vikao vya Bunge, kwani vikao hivyo si vinaonyeshwa na STar TV.

  Above all, binafsi naona vikao vya Bunge havina kitu kipya, ni bora watanzania tuangalie michuano ya Kombe la Dunia kuliko "kupoteza muda" kuangalia vikao vya Bunge.

  Hapa ndipo naona yale malalamiko yanayotolewa na media zingine kwamba uongozi wa TBC unatumia vibaya kodi za wananchi na hivyo kuleta unfair competition kwa private media ni kweli kabisa.

  Katika hili Tido Mhando umechemka BIG TIME!!
   
 2. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #2
  Jun 7, 2010
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Je wa sisi wa Mikoa ya Rukwa ambako bado Matangazo ya Digital hayazaanja? Maana hivo ving'amuzi ni kwa mikoa ambayo imeanza kurusha matangazo ya Digital tena katika Coverage ya 50 km radius, maana si kwa Mkoa Mzima wa Mwanza, wala Arusha wala Dar!
   
 3. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #3
  Jun 7, 2010
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Tatizo la waTZ mnapenda sana vya bure na bure ni ghari jamani.
   
 4. Brooklyn

  Brooklyn JF-Expert Member

  #4
  Jun 7, 2010
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 1,453
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Mkuu hata TBC wamepewa bure, kwa nini walikontest kurusha matangazo wakati walijua fika kwamba kuna vikao vya bunge??
   
 5. JoJiPoJi

  JoJiPoJi JF-Expert Member

  #5
  Jun 7, 2010
  Joined: Aug 8, 2009
  Messages: 2,458
  Likes Received: 1,331
  Trophy Points: 280
  Ahsante mkuu kwa kuliona hilo, hapa kwa kweli TBC wamechemka sana
   
 6. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #6
  Jun 7, 2010
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Lazima shirika lijiendeshe kibiashara zaidi sio kutegemea ruzuku serikalini kama unauwezo nunua hicho kifaa kama huna uwe unavizia kwenye bar zenye dstv unaangalia.
   
 7. Brooklyn

  Brooklyn JF-Expert Member

  #7
  Jun 7, 2010
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 1,453
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Issue si uwezo wa kununua, issue ni kwamba TBC wamewadanganya watanzania, kwa kipindi kirefu sana wamekuwa wakitangaza kwamba wataonyesha matangazo ya kombe la dunia. Alafu ghafla tu wameanza kuleta hadithi ya TBC2 ambayo ni channel ya kulipia.

  Hapa ndipo wadau tunapolalamika.......wangekuwa wamewaambia wadau mapema way back kutoka walipoanza kujitangaza kuonyesha kombe la dunia mwaka jana mwezi wa sita wakati wa michuano ya confederation cup!!

  Issue nyingine ni coverage ya hivyo ving'amuzi vyao..........sio siri TBC wanatia kichefuchefu!!
   
 8. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #8
  Jun 7, 2010
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135

  Mkuu mimi nko Rukwa nitawezaje kulipia?
   
 9. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #9
  Jun 7, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,798
  Likes Received: 157
  Trophy Points: 160
  Mkuu,

  Huwezi kupata haki ya kurusha matangazo ya Kombe la Dunia BURE!
   
 10. T

  Tsetse Member

  #10
  Jun 7, 2010
  Joined: Feb 22, 2010
  Messages: 7
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hii mijitu inayofaidikia na ufisadi wa CCM (mfano Fidel80) wanakera sana!!

  Mtoa mada halalamikii kukosa kuangalia dezo ila umafia wanaoufanyaga TBC....wao wana ruzuku toka serikalini na wanapo-bid wana-bid dau kubwa sana matokeo yake kichefuchefu kama hichi!!! ratiba ya bunge na mpira zilijulikana muda mrefu uliopita,kwa nini wafanye hivyo???

  Mimi wa Tanga, nina pesa yangu ya kulipia hicho king'amuzi niangaliea huo mpira lakini nitaukosa au kuangalia kwa mizengwe kwa sababu ya TBC!! As long as wao wamepewa right bure na FIFA kwa nini wamfaidishe huyo mchina wao in expense ya walalahoi wa Tanzania? Worse enough hata hiyo miko iliyopata hiyo bahati si mkoa mzima utakuwa covered ila ni mijini tu (50 km radius)...why????

  Kimsingi nchi hii ni 'individual survival' tu...hakuna wa kumtetea mnyonge hata kwa jambo lililo wazi kutetewa!!!
   
 11. Shakazulu

  Shakazulu JF-Expert Member

  #11
  Jun 7, 2010
  Joined: Feb 23, 2007
  Messages: 940
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Watu kama hawa wakiwa viongozi mnategemea nini?
   
 12. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #12
  Jun 7, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,798
  Likes Received: 157
  Trophy Points: 160
  Mkuu,

  Huwezi kupata haki ya kurusha matangazo ya Kombe la Dunia BURE!
   
 13. Brooklyn

  Brooklyn JF-Expert Member

  #13
  Jun 7, 2010
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 1,453
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Kweli inasikitisha sana! Huu upuuzi wa TBC si wa kutetewa, issue ni simple tu kwa nini wawastukize wananchi kununua hicho king'amuzi ambacho hata Kibaha hikifiki?
   
 14. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #14
  Jun 7, 2010
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,632
  Trophy Points: 280

  Mkuu umemaliza kila kitu nchi yetu ukijaribu kufuatilia kila jambo liko shabalabagala.
   
 15. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #15
  Jun 7, 2010
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Naamini DSTV inapatikana hapo wahi mapema ulipie kabla hujakumbana na foleni ndefu.
   
 16. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #16
  Jun 7, 2010
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,613
  Likes Received: 825
  Trophy Points: 280
  Ndiyo maana hata siku moja sichungulii TBC1. Ni upuuzi mtupu, wako kichama zaidi. Nataka nutrality zaidi. Je huko kwa Mangi hakutaka kuonyesha au ni vipi? Maana awali Mangi alikuwa anarusha na wazalendo walisuuzika roho zao.

  Hawa FIFA wangeipa a private TV channel na si hii ya chama tawala. Sasa wale ambao si wanachama wa chama tawala wao wananyimwa haki ya kufurahia kombe hili!!!!!!
   
 17. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #17
  Jun 7, 2010
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Dah pole mkuu ndo ilivyo lazima ubadilike kulingana na upepo.
  Jamaa walivyo fanya utafiti wakagundua kuwa kile king'amuzi kitauzika sana basi wamefuata upepo na watu wananua sana kama njugu, maana ni bei chee ukilinganisha na DSTV, pole mzee kama umeumia vya dezo.
  hahahaha nikiwa kiongozi tegemea kuwa nitawafanya watu mjitegemee zaidi sio kusubili dezo dezo.
   
 18. H

  Haika JF-Expert Member

  #18
  Jun 7, 2010
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,318
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  sipati picha unavyotia watu kichefuchefu!!
  ila kuchemsha wamechemsha,
  watangazaji wao wengi hawajui kinachoendelea, wanatoa matangazo yasioeleweka, wakiulizwa wanajibu upuuzi, wakati waku wako serious!

  inaleta kero sana.
  Labda kuna kipindi maalum wataweka kututaka radhi kwa kutuchanganya kwa conflicting msgs zao kwny TV na radio.

  LAKINI HUO NDIO UBEPARI TULIOUTAKA JAMANI, AU TUMECHOKA? IF SO TUNAFANYA NINI, MIMI NA WEWE?
   
 19. H

  Haika JF-Expert Member

  #19
  Jun 7, 2010
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,318
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  Kwa mimi yote sawa tu,
  sipendi bungew wala soka, naon ayanapoteza muda tu wa tamthiliya zetu za kulia lia
   
 20. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #20
  Jun 7, 2010
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Naamini wale walokole ndo wanao ona kichefu chefu lakini wale mabingwa wa totoz hapo ndo pakutokea home unaaga unaenda kuangalia mpira bar maana hakuna local chanel itakayo onyesha lazima ufunge safari bar na kitu chako moto au baridi naamini wengi wananiunga mkono lakini hawataki kuweka wazi walio wengi ni fraha kwao wachache ndo huzuni.
   
Loading...