Mkurugenzi wa TBC Bw. Tido Mhando umechemka BIG TIME!!

this is soo not fair! kwanini waliwadanganya wananchi kuwa wataonyesha kisha sasa wanasema hawaonyeshi?

angalau basi watu wangesema wapema wakajipanga......................hivi akina mama wenye watoto wadogo nao pia wende wakajipange bar kutizama mpira? au hawana haki?

sawa tbc inataka kwenda kibiashara...........lakini biashara pia lazima uitangaze na umwambie mteja mapema. hvi kushtukizwa hivi kuwa lazima ununue vifaa mbavyo vinapatikana mikoa mitatu tu ni sawa?

kisha mnataka kujifanya tz mnapenda sana soka kiasi cha kupoteza mamilioni ya pesa kuleta brazil.
 
kila mtanzania ni mzuri akifanya kazi nje ya nchi lakini akirudi tz ni fisadi tu.tido alikuwa bbc nafikiri aliogopa wazungu sasa ndio anajenga tutakoma ubishi mpaka alingane na chenge.
 
Jameni soko huria na hawa mijamaa lazima wakae kimasilahi zaidi ama sivyo kodi zetu watakula kama ruzuku
 
Je wa sisi wa Mikoa ya Rukwa ambako bado Matangazo ya Digital hayazaanja? Maana hivo ving'amuzi ni kwa mikoa ambayo imeanza kurusha matangazo ya Digital tena katika Coverage ya 50 km radius, maana si kwa Mkoa Mzima wa Mwanza, wala Arusha wala Dar!

Unaweza kuipata pia kwa njia ya sattellite sehemu yoyote hapa nchini ila utapaswa pia ununue dish lao.
 
lazima shirika lijiendeshe kibiashara zaidi sio kutegemea ruzuku serikalini kama unauwezo nunua hicho kifaa kama huna uwe unavizia kwenye bar zenye dstv unaangalia.

tuliambiwa kuwa serikali imejitoa kwenye biashara na hiyo ndo sababu ya kuuza mashirika ya umma, au kuna u turn kwenye policy ya nchi?
 
...Hii inawezekana Tanzania tu.
...Kwanza TBC ilijinadi sana kwamba wao pekee ndio watakaooonyesha World Cup.
...Ghafla hapo katikati kukaingia suala la Decorder.
...WAO WENYEWE TBC wakatutoa wasiwasi kwamba TBC one ingeonyesha mpira na TBC two ingekuwa kwa ajili ya mfumo wa Digital.
...WAO WENYEWE TBC ndio walituhakikishia kuwa tungeona mpira kwa kutumia aerial zetu za 'chadema'
...Ghafla wao wenyewe TBC wakaanza kujikanyaga kanyaga huku kila mtangazaji akitupiwa swali kuhusu hili anamtumpia mpira mwingine!
...Ghafla WAO WENYEWE TBC wanatuambia kuwa hatuwezi kuona mpira bila kuwa na Decorder/Malipo ya shilingi 80,000/=
...Suala hapa sio watu kupenda Dezo. Suala ni kwa nini hawakusema mapema??
...Suala hapa ni kwamba hata hizo Decorder zao hata baadhi ya sehemu za mkoa wa Dar hazifiki sembuse Mikoani??
...Suala hapa ni makampuni ya Biashara ambayo yamtoa hela zao nyingi ili kutangaziwa biashara zao halafu mwisho wa siku matangazo ya biashara zao yanaishia kuonwa na ROBO tu ya watazaji watakaoangalia michuano hiyo kupitia Decorder za TBC zinazoishia Kibaha tu!!
...Suala hapa ni kwamba ingekuwa nchi nyingine makampuni haya yaliyolipia matangazo yangeweza kushitaki kwa vile yalilipia matangazo yao ili yaone na watu wengi inavyowezekana na sio ROBO ya watu kutokana na wengine kudhibitiwa na Decorder zisizofika hata Kibaha tu!
...Tatizo ni kuwa Makampuni haya yataogopa kufanya kile yanachopaswa kufanya ambacho si Pungufu ya kuondoa matangazo yao TBC na kuomba kurejeshewa Walicholipa kwa sababu TBC imevunja mkataba kwa kuwaahidi kuwa matangazo yao ya biashara waliyolipia bei kubwa tu yataonekana nchi nzima wakati ukweli sasa ni kwamba yataonekana kwa watu wachache sana!
...Suala hapa ni kwamba hatuna haja ya kutafuta wachawi na mafisadi wa maendeleo yetu kwa sababu katika hili, TBC wamejunga na kundi la Wachawi na mafisadi wanaokwamisha Maisha Bora kwa Kila Mtanzania!!
...Suala hapa ni kwamba ili kulinda heshima yake na kuzuia kuonekana kwamba anshirikiana na Mafisadi kukwamisha ndoto ya kila Mtanzania kuwa na maisha Bora, Tido Mhando anatakiwa kujiuzulu huku akifarijika kuwa Waziri Mkuu wa Japan amejiuzulu wiki iliyopita kwa vile tu ameshindwa kuondoa kambi ya Jeshi ya Wamarekani kwenye Visiwa hivyo kama ALIVYOAHIDI!!
...Tido Mhando aliahidi kuwa Kila mtanzania mwenye Televisheni angeona Mechi Zote 64 za kombe la Dunia bila kulazimika kuwa na Decorder wala nini, anapogeuka na kutuambia kuwa hatuwezi kuona mechi hizo bila Decorder za Wachina zisizofika hata Kibaha tu, Anapaswa kujiuzulu!
...Tatizo ni kuwa hatuna Utamaduni huo!
...Tatizo ni kuwa Watanzania ni Kondoo!
...Tatizo ni kuwa kila Mtanzania ni Mbinafsi, Mradi yeye na watoto wake wana uwezo wa kununua Decorder wengine wote watajijua wenyewe!
...Tatizo ni mambo kama haya ndiyo yanayofanya tukwame tulipo maana tunagawanywa ili tutawaliwe vizuri.
...Hili linawezekana Tanzania tu.
 
"Bora maisha kwa kila mtanzania".Si lazima wote tuone kombe la dunia kama ilivyo si wote lazima tuone mechi ya Taifa na Brazil.Tutajiju mwka huu.
 
Duh hapo kweli kalikoroga inabaki kulinywa tu.hiyo ndio Tanzania bwana kwani mlikua hamjui?ohoo?watu wamewekeza kula tujipe pole wajameni
 
Unaweza kuipata pia kwa njia ya sattellite sehemu yoyote hapa nchini ila utapaswa pia ununue dish lao.

Duh! Kaazi kweli kweli sasa mimi nyumba yangu ya Nyasi leo niweke dish la TBC, kesho Dish la Syar tv, kesho kutwa Dish la ATN, ITV nao watakuambia uweke Dish lao sasa hapo itakuweje
 
Lazima shirika lijiendeshe kibiashara zaidi sio kutegemea ruzuku serikalini kama unauwezo nunua hicho kifaa kama huna uwe unavizia kwenye bar zenye dstv unaangalia.
Unajua fidel comment zako zinafanana sana na hyo avatar.....Mi huwa unanivunja mbavu tu. Tuvizie dstv sio teh teh teh...
 
FIFA huwa wanatoa Upendeleo wa Matangazo ya TV kwa National TVs only..Kuwaachia wengine kama STAR TV OR ITV ingekuwa ni makubaliano ya TBC NA HIZO TV..Ila FIFA wameweka masharti kuwa hawataki matangazo yao yanayorushwa hapa nchi yavuke mipaka ya Nchi ndo maana TBC wakafanya hivyo.Binafsi hutumia channel nyingine za Nchi kupata burudani za mpira na michezo mengine TBC wacha waendeleze vipind vya utamaduni kama ngoma zetu na kilimo kwanza!!..Lipia Supersport Premium( SS!-SS231) kwa burudani za kumwaga sio soka tu!!
 
Mkuu kweli inauma mi niko Arusha na hivyo ving'amuzi tuliuziwa tukaambiwa watakuwa hewani kuanzia tarehe tano juni, leo ni tarehe 7 hakuna kitu. Sijui wametutapeli au la
 
Kwa mimi yote sawa tu,
sipendi bungew wala soka, naon ayanapoteza muda tu wa tamthiliya zetu za kulia lia
bora wewe,kwa ujumla sipendi vyote hivyo,pamoja na channel zenyewe vilevile tena zooote na vipindi vyooote,bora mda wangu wa ziada nijipigie laga kisha ni kwenda kuangusha masebene:drum: tu,na mzuka ukipanda ni uno kama nimelipwa vile.raha jipe mwenyewe
 
Msilalamike sana jamani. Huu ni mwaka wa uchaguzi, na ninawaambia kuwa hii ni moja ya strategy za kuvutia kura, nyie tulalamikee, iki-heat sana JK atatangaza kwenye hiyohiyo TBC kuwa serikali imeamua kurusha matangazo ya mpira bure ili wananchi wajifunze toka kwa wenzetu, halafu tutarukaruka na kusema JK oyeee! October kura zetu zooooote kwa CCM.
 
Asante kwa kutujulisha, nashauri tuache mazungumzo ITV na STAR TV wawatumie wanasheria wao haraka sana watume pingamizi FIFA ili hili swala liweza kurekebishwa mara moja.

Dada yetu Joyce ni mzoefu kwenye mapambano kama haya, na sisi wananchi tuende tume ya fair competiton kama walivyofanya Serengeti Breweries wana JF tunaweza ku saini petition tukajumisha sahihi zetu na majina yakatumika kupinga hili hawa kina TIDO tusiwachekee hawana akili kichwani ni vituko vitupu wanavovifanya.

Nakubali kabisa kwamba bunge halina kitu limeshatupotezea muda kiasi cha kutosha.
 
Back
Top Bottom