BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,376
- 8,120
DAR: Watumishi 4 wa akiwemo Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha wafanyakazi wa Serikali za Mitaa Tanzania (TALGWU) akiwemo Mkurugenzi Mtendaji, Jackson M. Ngalama, Emmanuel G. Mdoe (Mhasibu), Pamela M. Sellemia (Mkuu wa Idara ya Mikopo), Timothy P. Mashishanga (Dereva) wamefikishwa Mahakamani kwa Ubadhirifu wa Tsh. 133,584,000.
Washtakiwa wote kwa pamoja wamekushtakiwa kwa Matumizi Mabaya ya Madaraka, Kusaidia Kutenda Kosa na Ufujaji wa Fedha, makosa ambayo ni kinyume na Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa na Sheria ya Uhujumu Uchumi.
Baada ya kusomewa mashtaka, Washtakiwa walikana makosa yote na kurejeshwa Mahabusu kwasababu wanakabiliwa na kesi nyingine ambayo haina dhamana. Kesi imeahirishwa hadi Februari 14, 2024 kwaajili ya kusomwa hoja za awali.