Mkurugenzi wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete tafadhali ona hili...

Kwani wewe unadhani wagonjwa hawafanani siku za kukaa hospitali au siku za kufariki au siku za kutolewa au kuingia?usilazimishe watu wote wawe wamepata huduma kama uliyopata wewe.
Hapa tunasema kilichotukuta ili wengine wasaidiwe,acha ushetani,unaonekana unapenda damu,mbuzi we.

Huko siko! Unahangaika sana rudi kwenye mada hili sio eneo la matusi na mipasho! Dhambi ya uongo huwa haimuachi mtu salama.
 
Unajua huwezi ukakurupuka tu kama kichaa kuanza kulaumu Manesi bila sababu, kwanini nisiwalaumu Madokta,? Mbona ma dokta wanafanya kazi zao vizuri tu sana pale? , mpaka kufika kuandika uzi huu ni mengi nimeyaona pale, huwezi kuandika kila kitu humu, chanzo kilianza tulifika kumwona mgonjwa tukakuta drip alilokuwa ametundikiwa mgonjwa limekwisha mpaka Damu imepanda kwenye ule mpira, tukamwita Nesi tukamuuliza, ina maana hamjaona hili, Mbona inaonekana ni Muda Mrefu limeisha tukamwambia in charge akasema kweli ni makosa, wakaja wakaondoa, Siku nyingine tumeingia pale saa saba mchana, tukakuta dawa zipo juu ya Meza pale, Bahati nzuri Doctor alikuwa anapita round, muda ule nikamuuliza doctor hizi dawa ni za mgonjwa wangu mbona zipo hapa? Doctor kawaita Manesi hizi dawa vipi? Eti hee tulisahau kumpa Doz ya tokea asubuhi hiyo. .Jamani? Doctor kabaki anashangaa tu Sasa hii ya chakula ndo ili nitibua kabisa....Jamani nyinyi acheni tu
Inauma sana sana....Na wapo mle ndani 24 hours kweli jamani
Mambo mengi sana pale nyinyi acheni jamani. ..jaribuni waulizeni wagonjwa waliolazwa pale, au ndugu zao pale ndo mtajua mengi pale. ..Na wengi hawatoi taarifa wanaogopa mgonjwa wao anaweza pengine asihudumiwe kabisa, ila ukiwauliza ukweli watafunguka mpaka utashangaa....Ukiwa na mgonjwa utajua mengi haki ya Mungu,.....
 
Kwa nilivosoma post zote nimeona kitu kimoja kua kuna wengine walienda wakapata huduma nzuri na wakaconclude kua huduma yao iko vizuri while kuna wengine walienda wakapata huduma mbovu na wakaconclude kua huduma yao sio nzuri.


Si vizuri kumshawishi mwenzako akubali unachokiamini wewe ila ni busara kuheshimu na kusikiliza mawazo ya mwenzako mana we all got different experience katika haya mambo
 
Mtu akipata stroke anakua useless kama ulikua haujui na tena stroke ni mbaya sana omba isikupate unakua disabled kufanya chochote usipokufa unashukuru Mungu
Najua ni mbaya, na nilishaipata nikashururu Mungu. Kama mtaalamu comment sio profeshanli kabisa. Kila ugonjwa una madhara yake, na stroke inapona kabisa.
 
Ukweli mtupu,na sio muhimbili tu hata hospitali nyingine kubwa za rufaa kuna BAADHI ya manesi wanaboa sana mpaka kuna mda wanagombana na madaktari maana hawatoi huduma kama wanavyoelekezwa mwishoni daktari ndio anaonekana mzembe.Ingawa wapo pia baadhi wanaofanya majukumu yao vizuri
 
Kwenye mbao za matangazo kuna namba za simu za Janabi mwenyewe chukua umpigie ni mwelewa sana yule mzee
 
Back
Top Bottom