Mkurugenzi wa Shule ampiga Mzazi na kitako cha bastola baada ya kuomba uhamisho wa mwanaye

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Dec 11, 2012
5,897
10,358
kitako.jpg

Jeshi la polisi mkoani Iringa linamshikilia Mkurugenzi wa shule ya Sun Academy, Nguvu Chengula, kwa tuhuma za kumpiga na kumjeruhi Alifa Mkwawa, ambaye ni mzazi, kwa kutumia kitako cha bastola baada ya kuombwa uhamisho wa mtoto anayesoma katika shule hiyo.

Kamanda wa Polisi mkoani humo Allan Bukumbi, amesema tukio hilo limetokea majira ya saa 6:00 mchana maeneo ya shule hiyo iliyopo mtaa wa Mawelewele ambapo chanzo cha tukio hilo ni mzozo uliotokana na mtuhumiwa kugoma kutoa uhamisho wa mtoto wa mlalamikaji kwa kile kinachodaiwa kuwa hajalipa ada ya mtoto huyo.

Chanzo: EATV
 
MZAZI WEB .jpg

Alifa Mkwawa, Mzazi aliyepigwa na kitako cha Bastola

Kamanda wa Polisi mkoani humo Allan Bukumbi, amesema tukio hilo limetokea majira ya saa 6:00 mchana maeneo ya shule hiyo iliyopo mtaa wa Mawelewele ambapo chanzo cha tukio hilo ni mzozo uliotokana na mtuhumiwa kugoma kutoa uhamisho wa mtoto wa mlalamikaji kwa kile kinachodaiwa kuwa hajalipa ada ya mtoto huyo.

Katika hatua nyingine jeshi hilo kwa nyakati tofauti limefanikiwa kukamata watuhumiwa watano na kuharibu mashamba matatu ya bangi iliyolimwa kwa mchanganyiko wa mahindi na maharage katika Kata ya Image wilayani Kilolo ambapo wakulima hao wanatumia mbinu ya kulima vishamba vidogo vidogo mtawanyiko na kupanda bangi kati ya mashina 20 hadi 60 kwenye maeneo ya misitu na makorongoni.

Chanzo: EATV
 
Hapa huruma zinaenda kwa mzazi na kusahau kuwa yeye ni sababu ya mgogoro in the first place. Unamhamishaje mtoto kwenda kwingine huku unadaiwa ada? Ni sawa asome bure?
Hata kama anadaiwa violence has never been a solution anywhere. bora angemsamehe maana sasa polisi watakula zaidi ya alizokuwa anadai za ada na ikibidi atadaiwa amfidie mzazi kwa kumuumiza.
 
Back
Top Bottom