Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali, Steven Katemba, alipewa heshima ya kutoa salamu za rambirambi wakati wa ibada ya mazishi ya Padre Vitalis Bamuhiga wa Jimbo Katoliki la Kayanga.
Hata hivyo, baada ya kutoa salamu, alijaribu kuzungumzia masuala ya kisiasa, kinyume na msimamo wa Kanisa Katoliki ambalo linakataza siasa kuingizwa madhabahuni. Kitendo hicho kilipingwa na viongozi wa ibada, na alionywa hadharani.
"Mhe. Baba Askofu, tunatambua nimesimama hapa nikiamini watu wote wakijua kwamba mimi ni Kiongozi wa Kisiasa, kwamba mwaka 2012 mpaka 2017 nimekuwa Kiongozi wa Chama Cha Mapinduzi kama Mjumbe wa kamati Kuu CCM Taifa, kwahiyo mbali na Utumishi wangu mwingine sehemu mbalimbali, Ofisi ya Rais na Ukurugenzi sehemu mbalimbali natambua hilo, kwahiyo sitasita kidogo kuongelea hilo na kuhusisha maisha na ya kiongozi wetu Bamuhiga pamoja na matukio yatakayotokea mwaka huu wa Uchaguzi"
Katemba alionekana kupuuzia onyo hilo, hali iliyopelekea kutakiwa kumaliza na kuondoka mara moja. Tukio hilo lilimsababishia aibu mbele ya waombolezaji na viongozi wa Kanisa.
Kanisa Katoliki lina msimamo thabiti kuhusu kutotumika kwa madhabahu kama jukwaa la kisiasa. Uongozi wa Kanisa umeendelea kusisitiza kuwa mtu anapopewa fursa ya kutoa salamu madhabahuni, anapaswa kuitumia kwa heshima na kwa mujibu wa taratibu za ibada.