Mkurugenzi wa JamiiForums, Maxence Melo apata tuzo ya International Press Freedom Award ya CPJ

Hongera sana Maxence Melo

Washindwe na walegee, wale "wanao-wish" malaika ashuke toka mbinguni ili aje aifunge mitandao na wale wote adui zetu wa freedom of expression
 
Ndugu zangu,

Kwa niaba ya Bodi, Wakurugenzi na Watendaji wa JamiiForums nampongeza Mkurugenzi Mkuu Maxence Melo kwa kutangazwa kuwa mshindi. Kwa mara nyingine kwa mwaka huu, JamiiForums tunampongeza Mkuu Maxence kwa kupata tuzo katika eneo la Uhuru wa Kujieleza na Uhuru wa Habari na kupata Taarifa. Maxence ametajwa kuwa mshindi wa tuzo ya Kimataifa ya (International Press Freedom Award 2019) inayotolewa na ‘The Committee to Protect Journalists (CPJ)’.

View attachment 1155037

Maxence amekuwa mstari wa mbele kupigania haki ya Watanzania kupata na kutoa taarifa kwa zaidi ya miaka 13 kupitia JamiiForums na hata kupelekea kukabiliwa na changamoto za kikazi, kuchafuliwa jina na baadhi ya watu wenye agenda zao binafsi na zaidi kukabiliwa na kesi ambazo zinazoendelea hadi sasa.

Kila mwaka CPJ hutoa tuzo kwa wadau wa habari ambao wamepitia vikwazo vya kisheria kama kesi, mashambulizi ya kimwili, vitisho, kukamatwa kutokana na kazi zao. Tuzo hizi ni mahususi kwa ajili ya kutambua watoa habari wenye ujasiri na dhamira ya dhati kuliko wote duniani na mchango wao katika kuhabarisha jamii zao hata ikibidi kuweka maisha yao kwenye mstari kila siku. Maxence amekuwa Mtanzania wa kwanza kushinda tuzo hii tangu zianzishwe mwaka 1996. Washindi watapewa tuzo zao katika sherehe za CPJ za mwaka ambazo zinatarajiwa kufanyika Jijini New York baadae mwaka huu 2019.

Kwa wale ambao tumebahatika kuwa katika kila hatua ya safari hii kwa kushuhudia na kupitia mitihani mingi ambayo Max amekuwa akipata na kuhimili; ushindi huu unatupa faraja na nguvu ya kusonga mbele na kutokata tamaa bila kujali vitu ama watu wenye lengo la kuondoa jitihada kwenye mstari. Maxence ameweza kuwa nahodha thabiti asiyeyumbishwa wala kutolewa kwenye mhimili wa kutumikia watanzania kadri ya uwezo wetu. Tunampongeza na kumshukuru kwa hilo.

Tunachukua fursa hii kumuombea kila la heri katika kutuongoza katika harakati za kuendelea kupigania haki ya kutoa na kupokea taarifa. Tunamuahidi kuwa timu yote ya JamiiForums itakuwa nae bega kwa bega katika safari hii. Insha’Allah Mwenyezi Mungu asimame nasi.

Nitumie hii nafasi pia kuishukuru taasisi ya CPJ kwa kumpatia tuzo hiyo, kuwashukuru Bodi na Watendaji wote wa JamiiForums kwa kuchangia wepesi wa shughuli zetu za kila siku. Na zaidi shukrani tele kwa Wadau na Watanzania kwa support ya kila namna mnayotupatia na Imani mliyoijenga kwetu na kuifanya JamiiForums iwe 'JamiiForums'.

Mwenyezi Mungu atubariki sote, Mwenyezi Mungu aibariki Tanzania.

Kwa niaba ya timu ya JamiiForums,

Asha D. Abinallah
Asante

View attachment 1155036
Mungu akujalie afya njema ya Mwili,ya Roho na ya Akili.Yeyote atakayetaka kukufanyia mabaya yampate mwenyewe
 
Tunashukuru kwa Taarifa hii njema, hongera sana Kwake na Kwenu Uongozi mzima wa Jamii Media Company ( Wamiliki wa Mtandao huu wa JamiiForums ) kwani kiukweli kwa Kazi anayoifanya Ndugu Maxence Melo akishirikiana nanyi anastahili hiyo Tuzo na hata zingine nyingi za haya Masuala ya Uhuru wa Habari nchini.

Labda Ushauri wangu tu Muhimu Kwake ni kwamba pamoja na kwamba anapata hizi Tuzo ila ajue kuwa kuna ambao wanaumia na kuchukia kabisa huku wakiombea hata huu Mtandao ufungwe kabisa kama siyo kupotea kwani unawaharibia mambo yao mengi ukijumlisha ya kwamba hapa JamiiForums Watu huwa wanafunguka vilivyo kuliko mahala pengine kokote kule.

Namwomba sasa Mshindi wetu wa hii Tuzo aanze pia Kulifanyia Kazi suala la Usalama wake mwenyewe Binafsi japo najua kwakuwa anafanya Kazi kubwa na nzuri ya Kuupigania Uhuru wa Watu Kujieleza hivi Mitandaoni hasa katika huu Mtandao wake / wenu basi hata Mwenyezi Mungu nae anamlinda na atamlinda ila anahitaji tu nae kuwa makini na mwangalifu na Maadui zake ambao kwa bahati mbaya Kwake na nzuri Kwao ni kwamba wapo wengi huku baadhi yao wakiwa kama Yule aliyeanza Kutumika Kumchokonoa na Kumchafua.

Hongera mno Kwake na namtabiria Tuzo zingine nyingi tu huko mbeleni. Mwenyezi Mungu ampiganie na awapiganie pia.
 
Hureeeeeeee leo lazima kieleweke, tukashangiliepo ushindi mweeehh!!!
Asha D Abinallah, naomba uniitie Zinduna, aje na cacico, snowhite, Preta, Kaunga wawaite na Madame B, @amu waanze kuandaa ukumbi. Mwambie Kipaji Halisi, ampitie Kaizer, na Asprin waende kwa Jiwe Linaloishi wakaandae ndafu. Ndahani, Nyani Ngabu, Kiranga, na @rutashubagumya waandike ushairi.
Mimi nakuja na Kongosho na King'asti kuserebuka. Tuzo hii mwambie Invisible aifanye ndio logo yetu. pasco Mayalla andaa kabisa kipindi Cha TV ili Kama bunge laivu hatuoni Basi tuone jinsi jf inavyo pata recognition ulimwenguni
 
Back
Top Bottom