Mkurugenzi wa JamiiForums, Maxence Melo apata tuzo ya International Press Freedom Award ya CPJ

Asha D Abinallah

Senior Member
Apr 5, 2015
138
1,000
Ndugu zangu,

Kwa niaba ya Bodi, Wakurugenzi na Watendaji wa JamiiForums nampongeza Mkurugenzi Mkuu Maxence Melo kwa kutangazwa kuwa mshindi. Kwa mara nyingine kwa mwaka huu, JamiiForums tunampongeza Mkuu Maxence kwa kupata tuzo katika eneo la Uhuru wa Kujieleza na Uhuru wa Habari na kupata Taarifa. Maxence ametajwa kuwa mshindi wa tuzo ya Kimataifa ya (International Press Freedom Award 2019) inayotolewa na ‘The Committee to Protect Journalists (CPJ)’.

6A3A062C-092F-450F-8904-EA81B4C2E504.jpeg


Maxence amekuwa mstari wa mbele kupigania haki ya Watanzania kupata na kutoa taarifa kwa zaidi ya miaka 13 kupitia JamiiForums na hata kupelekea kukabiliwa na changamoto za kikazi, kuchafuliwa jina na baadhi ya watu wenye agenda zao binafsi na zaidi kukabiliwa na kesi ambazo zinazoendelea hadi sasa.

Kila mwaka CPJ hutoa tuzo kwa wadau wa habari ambao wamepitia vikwazo vya kisheria kama kesi, mashambulizi ya kimwili, vitisho, kukamatwa kutokana na kazi zao. Tuzo hizi ni mahususi kwa ajili ya kutambua watoa habari wenye ujasiri na dhamira ya dhati kuliko wote duniani na mchango wao katika kuhabarisha jamii zao hata ikibidi kuweka maisha yao kwenye mstari kila siku. Maxence amekuwa Mtanzania wa kwanza kushinda tuzo hii tangu zianzishwe mwaka 1996. Washindi watapewa tuzo zao katika sherehe za CPJ za mwaka ambazo zinatarajiwa kufanyika Jijini New York baadae mwaka huu 2019.Kwa wale ambao tumebahatika kuwa katika kila hatua ya safari hii kwa kushuhudia na kupitia mitihani mingi ambayo Max amekuwa akipata na kuhimili; ushindi huu unatupa faraja na nguvu ya kusonga mbele na kutokata tamaa bila kujali vitu ama watu wenye lengo la kuondoa jitihada kwenye mstari. Maxence ameweza kuwa nahodha thabiti asiyeyumbishwa wala kutolewa kwenye mhimili wa kutumikia watanzania kadri ya uwezo wetu. Tunampongeza na kumshukuru kwa hilo.

Tunachukua fursa hii kumuombea kila la heri katika kutuongoza katika harakati za kuendelea kupigania haki ya kutoa na kupokea taarifa. Tunamuahidi kuwa timu yote ya JamiiForums itakuwa nae bega kwa bega katika safari hii. Insha’Allah Mwenyezi Mungu asimame nasi.

Nitumie hii nafasi pia kuishukuru taasisi ya CPJ kwa kumpatia tuzo hiyo, kuwashukuru Bodi na Watendaji wote wa JamiiForums kwa kuchangia wepesi wa shughuli zetu za kila siku. Na zaidi shukrani tele kwa Wadau na Watanzania kwa support ya kila namna mnayotupatia na Imani mliyoijenga kwetu na kuifanya JamiiForums iwe 'JamiiForums'.

Mwenyezi Mungu atubariki sote, Mwenyezi Mungu aibariki Tanzania.

Kwa niaba ya timu ya JamiiForums,

Asha D. Abinallah
Asante

5CE4F3A6-FB59-4CCF-BB52-179882B52DD8.jpeg
 
For the English Audience
CPJ’s International Press Freedom Award 2019 (IPFA2019) to Maxence Melo, ED

On behalf of the Board, Management and all the JamiiForums team, we would like to congratulate our Executive Director, Maxence M. Melo who has been awarded the ‘International Press Freedom Award 2019’ by the Committee to Protect Journalists (CPJ) today.

Maxence has been at the forefront of fighting for and protection of Online Freedom of Expression and Digital Privacy in Tanzania. He has used JamiiForums.com to provide a secure, credible and as the most reliable and whistle-blowing platform in Tanzania.

Maxence has played an enormous role in making JamiiForums platform revolutionize online and mainstream media through Freedom of Expression, pushing for political accountability, transparency and good governance.

This esteemed award is provided each year by CPJ to Journalists that have excelled and are going through legal constraints, physical attacks, threats, arrests from their work and keeping their lives in line every day. Maxence Melo is the first Tanzanian to receive this award since they were first launched in 1996. Earlier this year, he was also acknowledged as the ‘Distinguished Human Rights Defender of Online Freedom of Speech in Tanzania through Jamii Forums platform’, an award presented by The Coalition of Human Rights Defenders (THRDC).

At an international level, Maxence has been recognized by the African Union as one of the Leading African Innovators for Change in 2018 and H.E President Muhammadu Buhari of Nigeria acknowledged him for strengthening the viability of whistleblowing policy tools.

Quoting Maxence Melo recently when he issued a statement at JamiiForums to explain the matter of ‘privacy and protection’ of our clients: ‘There is a high cost we pay for the work we do. We face a lot of internal and external challenges. We will not despair nor will we give up on standing up for the rights for Freedom of Expression and Freedom of Privacy for our clients’.

It is an honor for the JamiiForums team to take each step with Maxence, for his commitment, his resilience, his leadership, his courage and most of all un-wavered integrity to standing up for the Digital Rights at large is astounding. We wish him nothing but the best in the struggle for a society with inclusive development, free to express themselves so as to contribute to transparency, accountability and good governance.

We extend our heartfelt ‘THANKS’ to the Committee to Protect Journalists (CPJ) for giving him this recognition, which we see as our victory too. This is a marking stone and inspiration, that no matter how hard it is, we are in the right track and we should keep moving.

THANK YOU!

On behalf of JamiiForums,

Asha D. Abinallah

Programs and Operations Director

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom