Mkurugenzi wa JamiiForums, Maxence Melo apata tuzo ya International Press Freedom Award ya CPJ

Ndugu zangu,

Kwa niaba ya Bodi, Wakurugenzi na Watendaji wa JamiiForums nampongeza Mkurugenzi Mkuu Maxence Melo kwa kutangazwa kuwa mshindi. Kwa mara nyingine kwa mwaka huu, JamiiForums tunampongeza Mkuu Maxence kwa kupata tuzo katika eneo la Uhuru wa Kujieleza na Uhuru wa Habari na kupata Taarifa. Maxence ametajwa kuwa mshindi wa tuzo ya Kimataifa ya (International Press Freedom Award 2019) inayotolewa na ‘The Committee to Protect Journalists (CPJ)’.

View attachment 1155037

Maxence amekuwa mstari wa mbele kupigania haki ya Watanzania kupata na kutoa taarifa kwa zaidi ya miaka 13 kupitia JamiiForums na hata kupelekea kukabiliwa na changamoto za kikazi, kuchafuliwa jina na baadhi ya watu wenye agenda zao binafsi na zaidi kukabiliwa na kesi ambazo zinazoendelea hadi sasa.

Kila mwaka CPJ hutoa tuzo kwa wadau wa habari ambao wamepitia vikwazo vya kisheria kama kesi, mashambulizi ya kimwili, vitisho, kukamatwa kutokana na kazi zao. Tuzo hizi ni mahususi kwa ajili ya kutambua watoa habari wenye ujasiri na dhamira ya dhati kuliko wote duniani na mchango wao katika kuhabarisha jamii zao hata ikibidi kuweka maisha yao kwenye mstari kila siku. Maxence amekuwa Mtanzania wa kwanza kushinda tuzo hii tangu zianzishwe mwaka 1996. Washindi watapewa tuzo zao katika sherehe za CPJ za mwaka ambazo zinatarajiwa kufanyika Jijini New York baadae mwaka huu 2019.

View attachment 1155130

Kwa wale ambao tumebahatika kuwa katika kila hatua ya safari hii kwa kushuhudia na kupitia mitihani mingi ambayo Max amekuwa akipata na kuhimili; ushindi huu unatupa faraja na nguvu ya kusonga mbele na kutokata tamaa bila kujali vitu ama watu wenye lengo la kuondoa jitihada kwenye mstari. Maxence ameweza kuwa nahodha thabiti asiyeyumbishwa wala kutolewa kwenye mhimili wa kutumikia watanzania kadri ya uwezo wetu. Tunampongeza na kumshukuru kwa hilo.

Tunachukua fursa hii kumuombea kila la heri katika kutuongoza katika harakati za kuendelea kupigania haki ya kutoa na kupokea taarifa. Tunamuahidi kuwa timu yote ya JamiiForums itakuwa nae bega kwa bega katika safari hii. Insha’Allah Mwenyezi Mungu asimame nasi.

Nitumie hii nafasi pia kuishukuru taasisi ya CPJ kwa kumpatia tuzo hiyo, kuwashukuru Bodi na Watendaji wote wa JamiiForums kwa kuchangia wepesi wa shughuli zetu za kila siku. Na zaidi shukrani tele kwa Wadau na Watanzania kwa support ya kila namna mnayotupatia na Imani mliyoijenga kwetu na kuifanya JamiiForums iwe 'JamiiForums'.

Mwenyezi Mungu atubariki sote, Mwenyezi Mungu aibariki Tanzania.

Kwa niaba ya timu ya JamiiForums,

Asha D. Abinallah
Asante

View attachment 1155036
MEI 3 ya kila mwaka ni Siku ya Kimataifa ya Uhuru wa vyombo vya habari, Mimi Pascal Mayalla, kwa niaba yangu kama mwanahabari na kwa niaba ya kampuni yangu ya PPR as chombo cha habari, niwatakie wanahabari wenzangu wote, maadhimisho mema ya siku hii, huku nikidurusu, niliwahi kusema nini kuhusu uhuru wa habari Kwa media za Tanzania yetu.

Nawatakia uhuru wa habari mwema.
Paskali.
 
Back
Top Bottom