Mkurugenzi TWAWEZA: Siku hizi kuna 'Fisi wa Kidigitali' wanaiba Taarifa Binafsi na kuzitumia vibaya

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,309
5,464
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya TWAWEZA, Aidan Eyakuze amewasii wadau kulinda taarifa binafsi za wateja wao huku pia akiwataka Wananchi kuwa makini wanapotoa taarifa zao ambapo amedai kuwa siku hizi kuna 'Fisi wa Kidigitali' ambao uchukua taarifa za watu na kuzitumia kwa madhumuni yao bila lidhaa ya wahusika.

"Siku hizi kuwa Fisi wa Kidigitali wanaweza kuiba data zako wakazichakate wakakuletea mambo ambayo hayakufai kabisa kwa mfano taarifa za mikopo ya kausha damu," amesema Aidan Eyakuze.

Amesema fisi hao wanaweza kuchakata taarifa hizo na kuwafuatilia wahusika kisha kuchakata maudhui yanayolenga kuwarubuni wahusika. Ametolea mfano akisema kuwa 'fisi' hao wakiona umekuwa mdau mikopo basi wanakutumia maudhui yanayonekana mazuri kuhusu mikopo.

Ameongeza kuwa fisi hao ni hatari zaidi kwa kuwa wanaweza kuchakata taarifa binafsi kumfahamu mtu anahitaji nini baada ya kugundua wanamtumia maudhui ya kurubuni kulingana na dhamira yao.

Ameyasema hayo Oktoba 31, 2023 kwenye maadhimisho ya miaka 15 ya Shirika lisilo la Kiserikali la Equality for Growth (EFG), ambalo ushughulika na masuala ya Wanawake kiuchumi ambayo yamefanyika katika Ukumbi wa Maktaba ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).

Hata hivyo, Aidan Eyakuze amewataka Wananchi kuwa makini wanapoombwa au kushawishiwa kutoa taarifa zao ambapo amewataka kama wanayo mashaka na aina ya taarifa wanazoombwa ni bora waache kutoa hizo taarifa.

Amewakubusha zaidi Wadau ambao wanahusika kukusanya taarifa kuwa kwa sasa hipo Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi ambayo tayari imeanza kutumika, hivyo amewataka kutunza taarifa wanazokusanya ili kuondokana na changamoto zinazoweza kujitokeza ambapo ametolea mfano kuwa yapo baadhi ya mataifa ambayo baadhi ya watu wamekumbana na madhara makubwa yanayotokana na kushindwa kutunza ipasavyo taarifa binafsi.

Ameyasema hayo mbele ya Wanawake zaidi ya 200 ambao ni sehemu ya wanufaika programu 'Sauti ya Mwanamke Sokoni' ambao wengi wao wamekuwa wakitoa taarifa binafsi kwa wadau mbalimbali hususani katika michakato ya kuomba mikopo ya kibiashara.

Itakumbukwa Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi ilipitishwa rasmi kutumika Mwaka 2022, Jamiiforums ikiwa sehemu ya Wadau wa karibu waliofanya uchechemuzi kufanikisha uwepo wa sheria hiyo, ambayo inaweka masharti kuhusu misingi ya ulinzi na uchakataji Taarifa Binafsi, kuanzisha Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi, kuimarisha ulinzi wa taarifa binafsi zinazochakatwa na Vyombo vya Serikali na vyombo binafsi na masuala mengine yanayohusiana na hayo.
 
Back
Top Bottom