Mkurugenzi na mkewe wafa maji Mpwapwa

Mkurugenzi na mkewe wafa maji Mpwapwa

beth

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
3,881
Reaction score
6,377
Kaimu mkurugenzi wa taasisi ya utafiti wa mifugo kanda ya kati, Dk Harun Chawala na mkewe, Neema Mwasanganga wamefariki baada ya gari walilokuwa wamepanda kusombwa na maji wakati wakivuka daraja la Shaaban Robert mjini Mpwapwa, Dodoma.

Kaimu Mkurugenzi mkuu wa taasisi ya utafiti Tanzania, Dk Jonas Kizima amesema leo Jumamosi Machi 6, 2021 kuwa tukio hilo limewasikitisha kutokana na kupoteza nguvu kazi ya Taifa na taasisi ya utafiti Tanzania.

Amesema Dk Chawala alikuwa anampeleka mkewe kazini kwenye hospitali ya wilaya, lakini walipo fika kwenye daraja hilo maji yaliwazidi na kusombwa.

Dk Kizima amesema tukio hilo limetokea jana saa 2 usiku baada ta gari hilo aina ya Nissan lenye namba za usajili T483 BRR kusombwa na maji kwenye daraja hilo lililopo mita chache kutoka ilipo ofisi ya mkuu wa wilaya.

Kutoka gari ilipotumbukia hadi ilikokutwa miili ni umbali wa karibu kilomita 18 na ilikuwa katika maeneo tofauti.

Mashuhuda wanasema mwili wa mwanamke ulikutwa kitongoji cha Kwamshango kilomita 15 kutoka walipotumbukia wakati mwili wa Dk Chawala ulikutwa kitongoji cha Isinghu umbali wa kilomita 18.

Miili yote imepatikana imehifadhiwa katika hospitali ya Mpwapwa ikisubiri taratibu za ndugu na Serikali.

Chanzo: Mwananchi
 
Gari kwenye maji sio la kuamini kabisa,halina nguvu yoyote,Pole kwa wafiwa

Madereva wengi tunapata leseni bila kupitia mafunzo sahihi..

Wakati nasoma NIT, nakumbuka niliambiwa usipite kwenye maji yanayotembea kabisa mpaka yaishe yasiguse tairi.. sababu tairi ni mpira uliojaa upepo,, yaani ni kama boya kwenye maji.. gari na uzito wake wote wa juu limebebwa na tairi ambalo ni boya kwenye maji.. sasa boya lazima lisombwe na maji tu, bila kujali uzito gani lilobeba,,, uoni hata binadamu kibonge akipewa boya anaelea tu bila kujali uzito wake,,

Hata gari liwe limebeba mzigo mzito kama copper ama kontena la mawe. Ila kwenye maji yanayotembea linasombwa na maji tu sababu matairi ni kama maboya
 
Back
Top Bottom