kilagalila
JF-Expert Member
- Nov 8, 2018
- 320
- 154
Na.amiri kilagalila
mc.amiri/mr.mtaani
Taasisi ya Kuzuia na kupambana na Rushwa Mkoani Njombe inawashikiria Watumishi wa Tano Wa Halimashauri ya Makete akiwemo Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Bw Francis Namaumbo kwa Ubadhirifu mkubwa wa Fedha zaidi ya Milioni 500 Za Kitanzania.
Akizungumza na Waandishi wa Habari Kamanda wa Takukuru Mkoani Njombe Chalse Nakembetwa amesema kuwa Upotevu wa Fedha hizo umetoka katika Makusanyo ya Mwezi July hadi Semptemba ambapo Makusanyo yake yalikuwa ni Zaidi ya Bilioni moja huku Taarifa zikionyesha kuwa zaidi ya Millioni 500 zimepotea na Wahusika wakishindwa kutoa Maelezo yakutosha baada ya Kuhojiwa na Taasisi hiyo.
Katika uchunguzi wake Takukuru imebaini wizi na ufisadi unaofanywa na baadhi ya watendaji wa halmashauri ya wilaya ya Makete jumla ya Tshs 569,537,02/(milioni mia tano sitini na tisa laki tano na thelathini na saba elfu na sabini na mbili) sawa na asilimia 46% zilizokusanywa kwa utaratibu wa POS kwa kipindi cha julai hadi septemba 2018 hazijulikani zilipo.
Makusanyo haya yalikuwa ni sehemu ya Tshs 1,245,632,633(bilioni moja milioni mia mbili arobaini na tano laki sita thelasini na mbili elfu na mia sita thelasini na tatu) yaliyokusanywa katika kipindi tajwa, alisema kamanda.
Aidha taarifa za kibenk na za kimfumo wa kompyuta zinaonyesha kuwa fedha zilizoingizwa benk katika kipindi hicho kina bakaa kubwa na hakuna maelezo yoyote kutoka kwa wahusika kuonyesha fedha hizi zilipelekwa na kwa madhumuni gani.
Kutokana na uchunguzi huo Takukuru mkoa wa Njombe inawashikiria baadhi viongozi na watendaji wa halmashauri ya wilaya ya Makete kwa ajili ya uchunguzi. Baadhi ya viongozi hao ni pamoja na.
1:bwana Francis Namaumbo
Mkurugenzi wa wilaya ya makete
2:bwana Edward Mdagachule
Mweka hazina wa wilaya ya Makete
3:bwana Edonia mahenge
Afisa biashara wilaya ya Makete
4:Goden Mbilinyi
Mtaalam wa Tehama Makete
5:Isaya madock
Mhasibu wa mapato Makete
Huku watuhumiwa wengine wakiendelea kutafutwa.
Katika hatua nyingine kamanda wa Takukuru mkoa wa Njombe Cherls Nakembetwa amesema kuwa watuhumiwa wote hapo juu wanashikiliwa kwa uchunguzi kwa makosa yafuatayo.
1.Matumizi ya nyaraka kumdanganya mwajiri K/F 22 cha PCCA/2007
2.Ubadhilifu na ufujaji K/F 28 cha PCCA/2007
3.Wizi chini ya kifungu cha 273 cha sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai (penal code)
4.Kujipatia manufaa K/F 23 cha PCCA/2007
Pamoja na makosa mengine yatakayobainishwa na uchunguzi.
Aidha takukuru kama chombo cha uchunguzi na mashtaka kinategemea kuchukua hatua kali kwa watakaobainika kuhujumu mapato ya serikali mara uchunguzi utakapokamilika ikiwa ni pamoja na kufungua kesi mahakamani.
MWISHO