Nishati Lutheran (DKK) Investment ya Ijangala, Makete Yaingiza Umeme KW360 Ktk Gridi ya Taifa

bagamoyo

JF-Expert Member
Jan 14, 2010
21,318
24,218

MRADI WA UMEME WAKAMILIKA​

Wakazi 4,500 kunufaika na umeme wa gridi Makete, Njombe Tanzania. Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Nishati Lutheran (DKK) wakati wakiwasha mitambo ya umeme wa mradi huu uliokamilika.
thumb_731_800x420_0_0_auto.jpg

Mradi wa kuzalisha umeme kwa kutumia maporomoko ya maji ya Mto Ijangala, kijiji cha Masisiwe, wilayani Makete, Mkoa wa Njombe, wakamilika .


View: https://m.youtube.com/watch?v=mqQ5NgCkdvw&

HISTORIA YA MRADI WA UMEME:

Tarehe Iliyowekwa: March 23rd, 2023
1694171396222.png

Hayo yamebainika wakati wa ziara iliyofanywa na viongozi wa juu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) wakiongozwa na Mwenyekiti wa Bodi, Janet Mbene, Machi 15 2023 mwaka huu.

Akiwa ameongozana na mmojawapo wa Wajumbe wa Bodi, Florian Haule pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa REA, Mhandisi Hassan Saidy, Mwenyekiti amekiri kufurahishwa na kuridhishwa na kazi nzuri ya utekelezaji wa Mradi huo ambao REA unaotarajiwa kuzalisha kilowati 360 za umeme pindi utakapokamilika.

Pamoja na pongezi, Mwenyekiti ameeleza kuwa anaamini kukamilika kwa Mradi huo unaotekelezwa na Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) na kufadhiliwa na REA pamoja na wadau wengine, kutatoa hamasa na kuchochea makundi na asasi mbalimbali za kijamii kuiga mfano wake hivyo kuwezesha umeme vijijini kuenea kwa kasi zaidi.
1694171329300.png

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu REA Mhandisi Hassan Saidy amekiri kuwa imani aliyoiweka kwa Taasisi hiyo ya Kanisa na kukubali kufadhili Mradi huo haikupotea bure kwani Mradi umetekelezwa kwa wakati na viwango vilivyotarajiwa.

“Katika hali ya kawaida, unatoa hela unaogopa kidogo, lakini niliwaambia matarajio yangu ni kwamba watafanya vizuri katika utekelezaji wa mradi huu wa nishati kama ambavyo wamefanya vizuri katika sekta za elimu na afya. Nawashukuru hawajaniangusha na nimefarijika sana,” ameeleza.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti, Mkurugenzi Mtendaji anayesimamia Mradi huo, Mdiakonia Elikana Kitahenga pamoja na Msaidizi wa Askofu KKKT Dayosisi ya Kusini Kati, Mchungaji Mathayo Sanga, wameishukuru REA kwa ushirikiano na mchango wake mkubwa tangu kuanza utekelezaji wa Mradi huo.

Wamesema, REA imekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha Mradi unatekelezwa siyo tu kupitia ufadhili wa fedha bali pia kwa viongozi na wataalamu wake kutembelea Mradi huo mara kwa mara kujionea maendeleo yake.

Mradi huo utakapokamilika na kuanza uzalishaji, unatarajiwa kuuza umeme huo kwa Shirika la Umeme Tanzania ili uingizwe kwenye gridi ya Taifa ikiwa ni Mkataba maalumu baina ya pande hizo mbili.

REA, ikiwa ni taasisi inayoshughulika upelekaji nishati vijijini, hutumia mbinu mbalimbali za kutekeleza kazi hiyo ikiwemo kufadhili vikundi au hata watu binafsi wanaojihusisha na uzalishaji nishati vijijini ili kutimiza azma ya serikali inayolenga kuhakikisha maeneo ya vijijini yanafikiwa na nishati bora

 
Back
Top Bottom