Mkurugenzi (DED) Masasi DC amvua cheo Mwalimu Mkuu kisa kushindwa kuchangia chochote kwenye ziara ya Mbunge

nez-o

Senior Member
Apr 13, 2019
181
178
Wadau, leo Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Masasi aliamua kumvua cheo Mwalimu Mkuu shule ya Msingi Chiwata tena mbele ya halaiki ya watu kisa kakosa hela ya kutoa harambee ya kuchangia maendeleo ya Kata.

Mkutano huo ulikuwa umeandaliwa na Mbunge wa Jimbo la Ndanda, Cecil Mwambe. Mkurugenzi akaanza kulazimisha watendaji, Mratibu elimu Kata na walimu walioko kwenye mkutano watoe ahadi wanachangia kiasi gani.

Ilipofika zamu ya mwalimu huyo akadai hana hela, ndipo DED mbele ya watu akasema “nakushusha cheo”.

Wananchi wakashangilia “oyoooo”! Ila baada ya Mbunge kumuombea msamaha akamrudishia cheo chake!

Je, wadau huu si udhalilishaji? DED Masasi DC acha ukoloni na umwinyi!
 
Hilo mbona "chamtoto sana" ukizingatia yeye ndiye aliyemteua (DED ndiye mwajiri wa Mwalimu)

Wengine kuuliza swali tu linalochoma au kusema una njaa kikaoni au kucheka au... basi umeyakanyaga!
 
Huyo DED masasi hana akili na limbukeni wa madaraka mkuu wa shule hashushwi cheo jukwaani kuna taratibu zake asiishi kwa mazoea
Kabisa mkuu uongozi hauko ivo sasa mtu kuchelewa kutoa ahadi kwamba atachangia sh flani ndo umshushe cheo kweli kwa mbwembwe nyingi Tena mbele na Wana nchi alafu mwisho anasema nimekurudishia cheo chako mbunge amekuombea msamaha kwa wananchi daa nchi ngumu hii
 
Naomba nijue tu huyu mkurugenzi ni yale mabaki ya magufuli?maana kama ni mabaki ya magufuli lisafishwe
 
Hilo mbona "chamtoto sana" ukizingatia yeye ndiye aliyemteua (DED ndiye mwajiri wa Mwalimu)

Wengine kuuliza swali tu linalochoma au kusema una njaa kikaoni au kucheka au... basi umeyakanyaga!
Itoshe tu kusema huyo mkurugenzi ni mjinga na hajui kanuni za utumishi wa umma ndio tabu ya kuokoteza watu huko na kuwaweka kwenye utumishi wa umma
 
Maisha yenyewe magumu bado unamlazimisha mtu achangie anasema hata eti nakuvua cheo Tena mbele ya wananchi nimemmaindi kinyama Sana leo DED Apollo tindwa huendi mbinguni alafu hicho ni cheo tuuu
Yaani mwl kaadhibiwa kwa umaskini wake duh
 
Kabisa mkuu uongozi hauko ivo sasa mtu kuchelewa kutoa ahadi kwamba atachangia sh flani ndo umshushe cheo kweli kwa mbwembwe nyingi Tena mbele na Wana nchi alafu mwisho anasema nimekurudishia cheo chako mbunge amekuombea msamaha kwa wananchi daa nchi ngumu hii
watanzania wengi wasome au wasisome wanaangukia kundi moja la WAJINGA. Mfano: DED(msomi) anafanya kitendo Cha kijinga kwa misifa,WANANCHI(wasio wasomi) kwa assumption wanaufurahia ujinga wa mjinga mwenzao kwa kushangilia.
Sijui ni lini wanasiasa wataziheshimu taaluma za watu.
Mfano: Kipindi Cha CORONA wanasiasa waliingilia wataalamu wetu wa afya na mwisho wa siku wakawapotosha WANANCHI na kuzua mixed reactions miongoni mwa WANANCHI. Sasa angalia namna wanasiasa haohao wanavopata wakati mgumu kushinikiza watu wachanje chanjo ya covid19.

Kawe:"
Mnachanja au hamchanji....?", Wao:"....tunahatuchanjiiiinjaaaa"

😂😂😂😂😂😂
 
Hawa maded washajisahau Mh raisi naomba uangazie macho kwa hawa wapandisha mabega ikiwezekana waanze kufanya interview badala yakuteuliwa wanapwaya Sana ukizingatia wengi ni wale wale wa enzi za mwendazake
 
Hilo mbona "chamtoto sana" ukizingatia yeye ndiye aliyemteua (DED ndiye mwajiri wa Mwalimu)

Wengine kuuliza swali tu linalochoma au kusema una njaa kikaoni au kucheka au... basi umeyakanyaga!
Nani huteuwa walimu wakuu?
Je ni huyo DEDE?
Kama unamfahamu basi utagundua makosa yapo hapa sio tu mtu kutumbuliwa jukwaani
 
Back
Top Bottom