Mbunge wa CHADEMA ashangiliwa kwenye ziara ya Waziri Mkuu wilayani Masasi

Ramea

JF-Expert Member
Mar 19, 2015
2,146
4,054
Waziri Mkuu wa Jamhuri Ya Muungano wa Tanzania, Mh Kassim Majaliwa yupo kwenye ziara ya siku Tatu mkoani Mtwara ambapo amehutubia wananchi wa Masasi kwenye viwanja vya sabasaba mjini masasi.

Kwenye tukio hilo lililoongozwa na mkuu wa mkoa wa Mtwara bwana Gellasius Byakanwa(Yule mkuu wa wilaya ya Hai aliyeharibu shamba la Mh Mbowe) aliwakaribisha viongozi mbalimbali wa vyama na serikali watoe salamu zao. Akiwemo Mama Hawa Ghasia, mbunge wa Newala ndg Mkuchika, Mbunge Wa Masasi bwana Chua Chua, Mbunge wa Lulindi, Tandahimba Na hatimae akamkaribisha Mbunge wa Jimbo la Ndanda kupitia CHADEMA ndugu Cecil Mwambe.

Umati wa watu ulilipuka kwa kelele baada ya ukaribisho huo wa mbunge wa ndanda kwa tiketi ya CHADEMA jambo lililomfanya DJ azime kelele kwa kuweka wimbo maarufu wa "TAZAMA RAMANI UTAONA NCHI NZURI"

Pamoja na hotuba ya Mhe Waziri mkuu kuvuta hisia za wananchi. Lakini wananchi wa Masasi waliondoka na kiu ya kujua mambo mengi ambayo hayakutolewa majibu kuhusu mustakabali wa maisha ya wanakusini.

Wananchi walikuwa na mabango ya kutosha lakini mhesh Waziri alimaliza kwa kusema mabango yatakusanywa na yatapatiwa ufumbuzi.

Ukiona kiongozi mkubwa wa nchi analetewa mabango yenye jumbe mbalimbali ujue watendaji wa ngazi hiyo hawafanyi kazi ipasavyo. Kilichofanyika kwenye mhadhara huyo kwa asilimia kubwa ni siasa tu. Wanakusini (Lindi na Mtwara) wajitathmini tu. Mtaendelea kulalamika huku wenzenu wanapiga hatua. Wakulima hamjalipwa hela za korosho, umeme unakatika na kuwaka kama indicator za gari wakati gesi ipo kwenu. Kwenye sekta ya Elimu nako viongozi kama mkurugenzi wa Mji Wa masasi Bi GIMBANA NTAVYO (mtoto wa shemeji ake JPM) wanachezea Elimu na kuifanya Mtwara ishike mkia kitaifa.

Matarajio ya wananchi kutoka kwa ziara hiyo ya mhes Majaliwa haijazima kiu yao, pamoja na kwamba kwa Mara ya kwanza nimeshuhudia wananchi wakikusanyika vile wakiwa na tumaini kuu kutoka kwa kiongozi mkubwa lakini wakarudi majumbani mwao wakiwa wamekata tamaa.
 
Naskia pole pole yuko kanda ya kaskazini na atazunguka nchi nzima kuongea na walimu na kuwabembeleza wamuombe rais msamaha na wamwambie kuwa tumebadilika na hatutasapoti tena upinzani.atakaye omba kwa barua atasamehewa deni lake la mkopo wa elimu ya juu anaodaiwa na serikali.kAZI IPO jiandae anakuja kwenu huko mtwara
 
Naskia pole pole yuko kanda ya kaskazini na atazunguka nchi nzima kuongea na walimu na kuwabembeleza wamuombe rais msahama na wamwambie kuwa tumebadilika na hatutasapoti tena upinzani.atakaye omba kwa barua atasamehewa deni lake la mkopo wa elimu ya juu anaodawaiwa na serikali.kAZI IPO
Walimu wenyewe wana hasira sana, tusubiri tuone watabembelezwaje.
 
Vijana wa BAVICHA bana mnafurahisha sana!

Wewe umeona kushangiliwa ndio iwe kichwa cha mada kama vile kushangiliwa ndio suala muhimu lililopelekea uwepo wa mkutano.

Wewe unaona kushangiliwa ni biashara. Mwezako Lowassa alikuwa mpaka anadekiwa barabara huku wadekaji wakikata viuno ili asipate mavumbi lakini ninasikia leo hii wenye CHADEMA wanatafuta njia ya kumuondoa ndani ya chama.

Kesho huyo mbunge akijiunga CCM utakuja hapa na kusema ni takataka.
 
Naskia pole pole yuko kanda ya kaskazini na atazunguka nchi nzima kuongea na walimu na kuwabembeleza wamuombe rais msamaha na wamwambie kuwa tumebadilika na hatutasapoti tena upinzani.atakaye omba kwa barua atasamehewa deni lake la mkopo wa elimu ya juu anaodaiwa na serikali.kAZI IPO jiandae anakuja kwenu huko mtwara
Oyaaa, mbona waanza comedy!
 
Mimi nilikuwepo kwenye mkutano huo,acha kudanganya watu,Cecil Mwambe alizomewa vibaya sana ,hakushangiliwa kama unavyotaka kupotosha
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom