Mkulo apasua jipu la DECI | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mkulo apasua jipu la DECI

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mpita Njia, Jun 18, 2009.

 1. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #1
  Jun 18, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Asubuhi hii mjini Dodoma, Mkulo amekutana na waandishi wa habari na kutokana na yale aliyoyaeleza kuna uwezekano mdogo wa waliopanda Deci kulipwa fedha zai zote. Kwa mujibu wa maelezo ya Mkulo, hesabu zimekaa hivi:

  Katika miezi mitatu ta mwisho kabla ya Deci kufungiwa, zaidi ya watu laki 3 walipanda zaidi ya Sh bilioni 39.

  Sakasaka ya serikali iliambulia zaidi kidogo ya Sh bilioni 1 katika akaunti za Deci.

  Sakasaka majumbani kwa viongozi ikaambulia Sh bilioni kama nane hizi zilizokuwa zimehifadhiwa majumbani (nyingibne kwenye maboksi).

  Sakasaka kwenye akaunti za viongozi wa decci ikaambilia kiasi kingine na kufanya jumla ya fedha zalizshikiliwa na serikali kutoka DECI kuwa kama sh bilioni 14.

  Hapo kuna pengo la zaidi ya Sh bilioni 25 iwapo itatakiwa kuwalipa wale waliopanda miezi mitatu ya mwisho ambao hawajavuna hata mara moja (kumbuka hapa hatujahusisha wapandaji wengine).
   
 2. Next Level

  Next Level JF-Expert Member

  #2
  Jun 18, 2009
  Joined: Nov 17, 2008
  Messages: 3,159
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Nawapa pole sana wote waliopanda mbegu zao huko.....sometimes we learn from mistakes...so tuwe makini the other time tunapotaka kuinvest kidogo tulicho nacho!
   
 3. M

  Mtu B JF-Expert Member

  #3
  Jun 18, 2009
  Joined: Dec 2, 2008
  Messages: 921
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  huu wizi unasikitisha sana. Nashangaa serikali ilikuwa wapi tangu 2007? Maana DECI hawa hawa walishaliza watu huko Kenya na wakatimuliwa. Huu upumbavu wa kuamini kila kinacholetwa kwa mwavuli wa dini utatumaliza!
   
 4. Bazobonankira

  Bazobonankira Senior Member

  #4
  Jun 18, 2009
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 120
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Mkuu,

  Asante kwa taarifa yako. Hata hivyo, pia tungependa kujua iwapo amezungumzia chochote kuhusu taarifa ya Task Force iliyokuwa imeundwa kushughulikia suala hili. Kwa kumbukumbu za haraka haraka ni kwamba timu hiyo ilishakabidhi taarifa yake kwa serikali.

  Au ndio tudhanie tu kwamba aliyowaeleza mkulo leo ndio executive summary ya riport?

  Binafsi, naamini report ya tume iliyoundwa ndiyo itaweza kueleza kinaga ubaga ni wanachama kiasi gani walikuwa wamepanda mbegu zao na bado walikuwa walisubiri 'kuvuna' kwa kipindi chote na si wale tu wa miezi mitatu.

  Mbali na hilo, we go east, we go west, nawatupia lawama sana our intelligence forces kwa kushindwa kung'amua mchezo huu mchafu tangu ulipoanza na kuweza kuvushauri vyombo husika juu ya hatua za msingi za kuchukua kabla ya maelfu ya watanzania wenzetu kuingizwa mkenge na wenzao whachache.

  Naamini kuna watu wanastahili kuwajibika na kuadhibiwa kule usalama wa Taifa pamoja na kamati ya ulinzi na usalama katika baadhi ya mikoa na wilaya.
   
 5. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #5
  Jun 18, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Alichokisema mkulo kimo kwenye ropiti ya serikali iliyoandaliwa kutokana na findings za rask force iliyochunguza suala hili
   
 6. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #6
  Jun 18, 2009
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0
  hiyo ni vijisenti tuu kwa kanisa

  itabidi kanisa ifanye wajibu wake na kuwakwamua hawa DECI maana iliipromote huu upatu sasa its about time ikawalinda kondoo wake
   
 7. M

  Mtu B JF-Expert Member

  #7
  Jun 18, 2009
  Joined: Dec 2, 2008
  Messages: 921
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Wenyewe huwa wanafundisha 'utavuna ulichopanda'. Sasa wamepanda upupu kwa kuwaaminisha waumini wao kuwa DECI ati ina 'upako'! Ni muda wa malipo sasa, wawafidie watu wao maana wao ndio waliowatuma wakapande huko.

  Au walimaanisha upako wa upupu?
   
 8. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #8
  Jun 18, 2009
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,312
  Likes Received: 5,600
  Trophy Points: 280
  DECI mmm naona hapo hata serikali inatakiwa ibebe lawama kabisa ina maana vyombo vyote havikuona hii DECI tangu 2007? Au ndio mumo kwa mumo nao wakubwa wamo??
   
 9. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #9
  Jun 18, 2009
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,589
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Kama hii ndio executive summary basi wamefanya kosa kubwa sana. Kwanini walipoorodhesha pesa walizozikuta kwa viongozi wameishia kwenye liquid capital peke yake. Kuna umuhimu(kama sio ulazima) wa kuorodhesha mali za hao viongozi.Inawezekana pesa waliyoiba wameshaibadilisha kuwa nyumba au shamba au gari au duka etc.
   
 10. StaffordKibona

  StaffordKibona JF-Expert Member

  #10
  Jun 18, 2009
  Joined: Apr 21, 2008
  Messages: 671
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Sawa kuilaumu serikali kwa kutoangalia jambo hili tangu DECI inaanzishwa. Lakini na sisi wananchi kweli uliskia wapi kuna hela za bure? Kuna vi-UPATU vingi vimepita hapa TZ na kuwatapeli watu lakini bado watu hawasikii. Ni upofu wa watu kutokuamini kuwa hakuna kitu cha bure dunia hii. Ulisikia wapi kuwa weka Tsh 200 keshokutwa upate Tshs 400. Hiyo ni kamari yenye kula au kuliwa. Hawa watu walienda wenyewe kuwapelekea DECI pesa hakuna aliyewalazimisha, kwa hiyo wasubiri mahindi yaote au kama yameoza basi wasubiri msimu mwingine wapande tena.
   
 11. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #11
  Jun 18, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Au wameikimbiza nje ya nchi
   
 12. m

  mmaroroi JF-Expert Member

  #12
  Jun 18, 2009
  Joined: May 8, 2008
  Messages: 2,536
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Poleni sana wana DECI mjivunze kufanya kazi na kusubiri vya bure.Kwani hata Mahindi,Maharage nk. ukipanda unapalilia na kutunza samba kabla ya kuvuna sasa hiyo panda ya DECI isiyohitaji kufanyakazi ni ya wapi.
   
 13. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #13
  Jun 18, 2009
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Kanisa ni nini?
   
 14. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #14
  Jun 18, 2009
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Alichosema Mkulo hakiingii akilini.
  Siamini kama serikali iko siriaz kushughulikia suala la DECI.
  Kuwashtaki viongozi wa DECI ni danganya toto tu.

  Kuna kitu kinafichwa hapo. na hilo pengo la pesa isiyoonekana naamini ni usanii tu. kwani serikali haishindwi kitu ikitulia na kutafiti kwa kina....
   
Loading...