Mkuchika: Hakuna Mafao Kwa Waliogushi Vyeti

Mkuchika: Hakuna Mafao Kwa Waliogushi Vyeti

Wafanyazi waliokuwa wamefoji vyeti vya shule walifanya kosa lakini mfumo wa hovyo uliotawaliwa na rushwa ndio wa kulaumiwa zaidi.
Kujuana na upendeleo ndivyo vilivyowapa mwanya wafanyazi hao kughushi hati hizo hasa baada ya kuona hata mabosi wao wanatumia vyeti vya form iv vya marehemu ndugu zao nk.
Uozo ndani ya mfumo wa Serikali umewafanya watu kuchukulia mambo kirahisi mno.
Bado kuna wafanyazi wasio na vyeti halali vya form four katika mfumo wa ajira za umma na hao waliobainika wamefanywa kama scapegoats tu.
Kuna baadhi ya hao waliobambwa kwa kufoji vyeti walikuwa na wachapa kazi wazuri na wamelitumikia taifa kwa muda mrefu. Sawa walikosea kufoji lakini kuna watumishi waliwahi kufanya makosa makubwa zaidi na bado wanadunda.
Kati ya hao wanaodaiwa kufanya kazi kwa kuajiwa kwa vyeti bandia wapo waliokaribia kustaafu na walikuwa wakikatwa kodi ambayo Serikali iliitumia kujenga nchi.
Isitoshe walikuwa wakikatwa michango ya mashirika ya hifadhi ya jamii. Kuwaondoa bila kuwalipa mafao yao ni ukatili mkubwa.
Tayari wamekwisha tumikia adhabu ya kuondolewa kazini. Inatosha. Nawaonea huruma wale waliobakiza miezi michache kustaafu. Unamnyimaje mafao mtu aliyelitumikia taifa kwa miaka 30?! Mkuchika walipeni bwana na baada ya hapo state izibe mianya yote ya kughushi vyeti ndani ya mfumo wa Serikali.
Tatizo limetengenezwa na jamii yenyewe kutokana na utepetevu wa Serikali katika kupambana na rushwa. Pambaneni na misangara ya ufisadi kwanza ndipo mtakuwa na moral authority ya kuwatunishia misuli wafanyazi wanyonge.
Nanyi Watanzania acheni kushabikia kughushi vyeti. Wazazi wahimizeni watoto kusoma kwa bidii ili wapate maarifa na vyeti halali. Hakuna njia ya mkato.
Kuna walioruhusu dhahabu, almasi, tanzanite, gesi, nk. kutoroshewa nchi za ng'ambo bila faida yoyote kwa nchi. Waliowezesha hayo kufanyika wakalisababishia taifa hasara kubwa wapo wanadunda hadi hivi leo wakila pension zao!
 
Inanikumbusha pesa za DECI zilivyozuiwa na serikali hazikuwahi kurudishwa kwa wachangiaji (wahanga wa DECI) mpaka sasa.
 
This is very unfair.

Mtu amewafanyia kazi miaka na miaka, halafu mwishoni mnataka mumdhulumu stahiki yake kwa kisingizio cha cheti. Tena wengine mliwapandisha hadi vyeo kutokana na utendaji wao.

Hao wote awali ya kwanza ilikuwa wawe rumande kwani wamehujumu taifa kipindi chote walichofinyia kazi kwa vyeti feki! Pili kurudisha fedha zote walizokuwa wameziiba kwa njia ya vyeti feki, kama hawana, ni jela maisha!
 
Na kwanini ughushi vyeti...!?

Tena inabidi warudishe pesa zote walizolipwa na serikali....
 
Sasa mlikubali vipi mafao ya mtu asiye na cheti yaingie kwenye mifuko yenu?

Ilikuwa bado kugundulika! Soma maelezo kutoka mwanzo, acha kudandia treni kwa mbele! It had not been known that they had acquired forged certificates, it was presumed that they were genuine qualified employees with proper qualifications! I hope you have understood my friend, acha kuwa limbukeni!
 
Kwa hiyo aliyeteuliwa anaruhusiwa na sheria kughushi vyeti!!!??
Amini usiamini, anaruhusiwa. Badilisha katiba uweke ownership ya wananchi kwenye uteuzi wa viongozi kupitia kuthibitishwa na bunge kama Kenya au US ndio uje uongee hilo.
 
Siwatetei hawa wagushi vyeti Ila niwapongeze wale ambao wameshaliacha hili huko nyuma na sasa wanaendelea na maisha. Wanasema mlango mmoja ukifungwa mwingine unafunguliwa. Makosa yapo yalifanyika ni vyema wakiyakubali. Kwa maoni yangu Hawa wa vyeti feki hukumu yao ilikuwa ni kubwa mno. Kwangu mm kuondolewa Kazini ingetosha. Kuwatelekeza watu waliobakiza mwaka wastaafu, wenye watoto na ndugu tegemezi kwa ghafla bila chochote ni kuhukumu kuliko inavyostahili. Niwape Pole wale ambao kwa kosa hili walilofanya na hukumu waliyopewa wakajikuta kwenye matatizo na hawapo nasi au wameshindwa kuendelea.
 
Amini usiamini, anaruhusiwa. Badilisha katiba uweke ownership ya wananchi kwenye uteuzi wa viongozi kupitia kuthibitishwa na bunge kama Kenya au US ndio uje uongee hilo.
Hahahaaa!!!
Anaruhusiwa na sheria kughushi vyeti,seriously!???????????
 
Mkuchika apigilia msumari malipo ya mafao kwa walioghushi vyeti

Kwa ufupi

Hakuna atayelipwa hata kama alibakiza mwaka mmoja kustaafu

Dodoma. Kwa mara nyingine tena, Serikali imeendelea kupigilia msumari kwa watu walioondolewa kwenye utumishi kutokana na vyeti feki kwamba hakuna malipo yoyote watakayolipwa.

Kauli hiyo ilitolewa leo Bungeni wakati Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Utumishi na Utawala Bora, George Mkuchika ambaye amesema hakuna malipo yoyote wanayodai.

Mbunge wa Viti Maalumu (CCM), Haida Kenani, aliiomba Serikali kufikiria upya ni kwa nini isiwalipe hata watumishi waliobakiza mwaka mmoja kustaafu.

"Tatizo la Serikali mnaangalia vyeti hamuangalii taaluma ya watu na hata wabunge wengine mlifundishwa na hao lakini mnawatosa ni kwa nini,” alihoji Kenani.

Mkuchika alisema katika hali ya kawaida mwajiri alipowaajiri watumishi hao walionyesha kuwa na elimu stahiki na hivyo walipata mishahara kulingana na viwango vyao vya elimu wakati ni kosa.

Alisema sheria haimruhusu mtu kulipwa wakati inajulikana amedanganya.


Chanzo: Mwananchi Online
Waziri amekosea. Mtu analipwa kwa kuwa alitumika.
 
Swali tu la kizushi,hivi mtu akiondolewa serikalini kwa sababu ya kugushi vyeti labda na akarudi uraiani kujiajiri na akaanza kujishangia kwenye mifuko ya jamii nauliza tu ataendelea na namba yake ileile au watamwanzishia upya!Je sheria ya mfao inasemaje mpaka ulipwe mafao?ninachojua ni kigezo cha kugushi cheti hakipo je ni sahihi mtu kutopata stahili zake kama hicho sio kigezo .Just thinking tu
 
Hahahaaa!!!
Anaruhusiwa na sheria kughushi vyeti,seriously!???????????[/QUOTE
Ndio maana nimekuandikia amini,usiamini. Kama unauliza seriously??Na wewe nakuuliza mbona hujaweza kumtoa. Read between my lines.
 
Mkuchika apigilia msumari malipo ya mafao kwa walioghushi vyeti

Kwa ufupi

Hakuna atayelipwa hata kama alibakiza mwaka mmoja kustaafu

Dodoma. Kwa mara nyingine tena, Serikali imeendelea kupigilia msumari kwa watu walioondolewa kwenye utumishi kutokana na vyeti feki kwamba hakuna malipo yoyote watakayolipwa.

Kauli hiyo ilitolewa leo Bungeni wakati Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Utumishi na Utawala Bora, George Mkuchika ambaye amesema hakuna malipo yoyote wanayodai.

Mbunge wa Viti Maalumu (CCM), Haida Kenani, aliiomba Serikali kufikiria upya ni kwa nini isiwalipe hata watumishi waliobakiza mwaka mmoja kustaafu.

"Tatizo la Serikali mnaangalia vyeti hamuangalii taaluma ya watu na hata wabunge wengine mlifundishwa na hao lakini mnawatosa ni kwa nini,” alihoji Kenani.

Mkuchika alisema katika hali ya kawaida mwajiri alipowaajiri watumishi hao walionyesha kuwa na elimu stahiki na hivyo walipata mishahara kulingana na viwango vyao vya elimu wakati ni kosa.

Alisema sheria haimruhusu mtu kulipwa wakati inajulikana amedanganya.


Chanzo: Mwananchi Online
Hivi mtu aliyegushi cheti atalipwaje mafao?You reward a convict for cheating?Hapana jamani,hapa pana-hitajika tu a minimum common sense kujua which is right or wrong.Mkuchika yuko sahihi kabisa,we can't pay convicts.
 
Hivi mtu aliyegushi cheti atalipwaje mafao?You reward a convict for cheating?Hapana jamani,hapa panahitajika a minimum of common sense kujua which is right.Mkuchika yuko sahihi kabisa.
Nakubaliana na wewe kwenye hiyo,lakini kama Bashite alighushi vyeti,(ikiwa ni kweli),je,yeye sheria inampitia kushoto?
Kwa maana nyingine,ni halali kwa mteule wa rais kughushi vyeti na kuachwa tu,kwa sababu ni mteule!???

Sheria zetu zipo bias kiasi hicho kweli!???
 
This is very unfair.

Mtu amewafanyia kazi miaka na miaka, halafu mwishoni mnataka mumdhulumu stahiki yake kwa kisingizio cha cheti. Tena wengine mliwapandisha hadi vyeo kutokana na utendaji wao.
Ni vizuri iwe funzo kwa wote wenye tabia ya kupenda short cuts, hawa watawafundisha watoto wao kuogopa kabisa forgery.
 
Mahakama ya East Afrika inaweza ikawapa tafsi ni wao kuamka tu na kuunda umoja wao ambao utawasaidia kitambulika.
Wasiwe na aibu kwani nao walipambana ktk utendaji wa ndio maana wanatambulika
 
Dhumuni kuu la mifuko ya jamii ni kumsaidia mfanyakazi aweze kuendeleza maisha yake baada ya ajira yake kufikia kikomo ili ASIJE KUWA MZIGO KWA SERIKALI ktk maisha yake ya uzeeni.
Sasa kutowalipa mafao yao (pesa ni za kwao si mikopo), serikali itakuwa imeepuka vipi hiyo mizigo ambayo imejibebesha kwa makusudi kabisa.
Nadhani busara itumike hapa la sivyo tutashuhudia vifo vingi sana vilivyosababishwa na serikali yetu. Mungu hapendi.
Kibaya zaidi wengine unakuta alishabakiza mwaka au miaka isiyozidi 2 astaafu.
Jinsi familia zao zitakavyoteseka ndo laana itakavyozidi kuwakuta wale wote waliohusika ktk maamuzi hayo.
Mungu apishe mbali
Iko siku utakuja utawala mwingine na hao wafanyakazi watalipwa stahiki zao. Tuombe Mungi iwe 2020 au hata awamu ya 2025. Mungu Ibariki Tanzania
 
Sasa mlikubali vipi mafao ya mtu asiye na cheti yaingie kwenye mifuko yenu?
Sio mafao tu, kazi zake bado zinakubalika. Kwa mfano hakimu mwenye cheti feki hakuna hukumu yake iliyotenguliwa. Aliyewahukumu kufungwa bado wanaozea jela!!

Hii kitu inataka busara sana
 
Nakubaliana na wewe kwenye hiyo,lakini kama Bashite alighushi vyeti,(ikiwa ni kweli),je,yeye sheria inampitia kushoto?
Kwa maana nyingine,ni halali kwa mteule wa rais kughushi vyeti na kuachwa tu,kwa sababu ni mteule!???

Sheria zetu zipo bias kiasi hicho kweli!???
Umeshasema kama ni kweli,so you are not sure.This then ends the discussion.
 
Back
Top Bottom