Mkuchika: Hakuna Mafao Kwa Waliogushi Vyeti

Mkuchika: Hakuna Mafao Kwa Waliogushi Vyeti

CHA The GREAT

JF-Expert Member
Joined
Nov 11, 2010
Posts
651
Reaction score
855
Mkuchika apigilia msumari malipo ya mafao kwa walioghushi vyeti

Kwa ufupi

Hakuna atayelipwa hata kama alibakiza mwaka mmoja kustaafu

Dodoma. Kwa mara nyingine tena, Serikali imeendelea kupigilia msumari kwa watu walioondolewa kwenye utumishi kutokana na vyeti feki kwamba hakuna malipo yoyote watakayolipwa.

Kauli hiyo ilitolewa leo Bungeni wakati Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Utumishi na Utawala Bora, George Mkuchika ambaye amesema hakuna malipo yoyote wanayodai.

Mbunge wa Viti Maalumu (CCM), Haida Kenani, aliiomba Serikali kufikiria upya ni kwa nini isiwalipe hata watumishi waliobakiza mwaka mmoja kustaafu.

"Tatizo la Serikali mnaangalia vyeti hamuangalii taaluma ya watu na hata wabunge wengine mlifundishwa na hao lakini mnawatosa ni kwa nini,” alihoji Kenani.

Mkuchika alisema katika hali ya kawaida mwajiri alipowaajiri watumishi hao walionyesha kuwa na elimu stahiki na hivyo walipata mishahara kulingana na viwango vyao vya elimu wakati ni kosa.

Alisema sheria haimruhusu mtu kulipwa wakati inajulikana amedanganya.


Chanzo: Mwananchi Online
 
[emoji419][emoji419][emoji419][emoji419][emoji419][emoji419]
 
This is very unfair.

Mtu amewafanyia kazi miaka na miaka, halafu mwishoni mnataka mumdhulumu stahiki yake kwa kisingizio cha cheti. Tena wengine mliwapandisha hadi vyeo kutokana na utendaji wao.
 
Mkuchika apigilia msumari malipo ya mafao kwa walioghushi vyeti

Dodoma. Kwa mara nyingine tena, Serikali imeendelea kupigilia msumari kwa watu walioondolewa kwenye utumishi kutokana na vyeti feki kwamba hakuna malipo yoyote watakayolipwa.

Kauli hiyo ilitolewa leo Bungeni wakati Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Utumishi na Utawala Bora, George Mkuchika ambaye amesema hakuna malipo yoyote wanayodai.

Mbunge wa Viti Maalumu (CCM), Haida Kenani, aliiomba Serikali kufikiria upya ni kwa nini isiwalipe hata watumishi waliobakiza mwaka mmoja kustaafu.

"Tatizo la Serikali mnaangalia vyeti hamuangalii taaluma ya watu na hata wabunge wengine mlifundishwa na hao lakini mnawatosa ni kwa nini,” alihoji Kenani.

Mkuchika alisema katika hali ya kawaida mwajiri alipowaajiri watumishi hao walionyesha kuwa na elimu stahiki na hivyo walipata mishahara kulingana na viwango vyao vya elimu wakati ni kosa.

Alisema sheria haimruhusu mtu kulipwa wakati inajulikana amedanganya.
 
Wafanyazi waliokuwa wamefoji vyeti vya shule walifanya kosa lakini mfumo wa hovyo uliotawaliwa na rushwa ndio wa kulaumiwa zaidi.
Kujuana na upendeleo ndivyo vilivyowapa mwanya wafanyazi hao kughushi hati hizo hasa baada ya kuona hata mabosi wao wanatumia vyeti vya form iv vya marehemu ndugu zao nk.
Uozo ndani ya mfumo wa Serikali umewafanya watu kuchukulia mambo kirahisi mno.
Bado kuna wafanyazi wasio na vyeti halali vya form four katika mfumo wa ajira za umma na hao waliobainika wamefanywa kama scapegoats tu.
Kuna baadhi ya hao waliobambwa kwa kufoji vyeti walikuwa na wachapa kazi wazuri na wamelitumikia taifa kwa muda mrefu. Sawa walikosea kufoji lakini kuna watumishi waliwahi kufanya makosa makubwa zaidi na bado wanadunda.
Kati ya hao wanaodaiwa kufanya kazi kwa kuajiwa kwa vyeti bandia wapo waliokaribia kustaafu na walikuwa wakikatwa kodi ambayo Serikali iliitumia kujenga nchi.
Isitoshe walikuwa wakikatwa michango ya mashirika ya hifadhi ya jamii. Kuwaondoa bila kuwalipa mafao yao ni ukatili mkubwa.
Tayari wamekwisha tumikia adhabu ya kuondolewa kazini. Inatosha. Nawaonea huruma wale waliobakiza miezi michache kustaafu. Unamnyimaje mafao mtu aliyelitumikia taifa kwa miaka 30?! Mkuchika walipeni bwana na baada ya hapo state izibe mianya yote ya kughushi vyeti ndani ya mfumo wa Serikali.
Tatizo limetengenezwa na jamii yenyewe kutokana na utepetevu wa Serikali katika kupambana na rushwa. Pambaneni na misangara ya ufisadi kwanza ndipo mtakuwa na moral authority ya kuwatunishia misuli wafanyazi wanyonge.
Nanyi Watanzania acheni kushabikia kughushi vyeti. Wazazi wahimizeni watoto kusoma kwa bidii ili wapate maarifa na vyeti halali. Hakuna njia ya mkato.
 
Dhumuni kuu la mifuko ya jamii ni kumsaidia mfanyakazi aweze kuendeleza maisha yake baada ya ajira yake kufikia kikomo ili ASIJE KUWA MZIGO KWA SERIKALI ktk maisha yake ya uzeeni.
Sasa kutowalipa mafao yao (pesa ni za kwao si mikopo), serikali itakuwa imeepuka vipi hiyo mizigo ambayo imejibebesha kwa makusudi kabisa.
Nadhani busara itumike hapa la sivyo tutashuhudia vifo vingi sana vilivyosababishwa na serikali yetu. Mungu hapendi.
Kibaya zaidi wengine unakuta alishabakiza mwaka au miaka isiyozidi 2 astaafu.
Jinsi familia zao zitakavyoteseka ndo laana itakavyozidi kuwakuta wale wote waliohusika ktk maamuzi hayo.
Mungu apishe mbali
 
Mkuchika apigilia msumari malipo ya mafao kwa walioghushi vyeti

Mbunge wa Viti Maalumu (CCM), Haida Kenani, aliiomba Serikali kufikiria upya ni kwa nini isiwalipe hata watumishi waliobakiza mwaka mmoja kustaafu.

"Tatizo la Serikali mnaangalia vyeti hamuangalii taaluma ya watu na hata wabunge wengine mlifundishwa na hao lakini mnawatosa ni kwa nini,” alihoji Kenani.

Chanzo: Mwananchi Online

Huyu mbunge wa viti maalum hapo kwenye "red" sijamuelewa na kwa kweli ameniacha.
 
Makonda tuu peke yake ndie atakaye pata sio?.Mama..eeeeeeeee.
 
Back
Top Bottom